Thursday 23 May 2024

WAZIRI WA AFYA ABAINISHA MBINU ZA HEDHI SALAMA

 Ummi Mwalimu Waziri wa Afya amesema ili kuwepo na hedhi salama nchini tanzania ni vyema wadau na serikali kujenga miundombinu rafiki na wezeshi kwenye mashule kwaajili ya wasichana waliopo mashuleni pamoja na kwenye masoko na maofisini lengo wanawake wanapofikia kipindi cha hedhi waweze kujistili huku wakiendelea na shughuri zao za kila siku.

Ametoa wito kwa jamii kuacha mira na destuli potofu pindi mwanamke anapofika kipindi cha hedhi.

Habari na Ally Thabit 

WIZARA YA UVUVI YAGUSWA NA WATU WENYE ULEMAVU


 Mkurugenzi wa  Uvuvi Prof  Mohammed Shekh Kutoka Wizara ya Uvuvi na Mifugo amesema katika wavuvi wadogo ambao mkutano wa kimataifa utafanyika tarehe 5/6/2024 jijini dar es  salaam ni muhimu sana kwani utasaidia wavuvi hawa kupata fursa mbalimbali ,Swala la kuwashirikisha na kuwafikia watu wenye ulemavu kwenye sekta ya uvuvi ni muhimu na lina tija kubwa hivyo wizara ya uvuvi na mifugo wamelibeba na watalifanyia kazi amesema haya jijini dar es salaam  nilipofanya nae mahojiano.

Habari picha na Ally Thabit 

WAZIRI WA UVUVI KUWATAFUTIA WAVUVI WADOGO MASOKO YA KIMATAIFA


 Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega amesema tarehe 5 /6/2024 kutakuwa na mkutano mkubwa wa kimataifa utakao fanyika Dar es salaam  lengo la mkutano huu kutatuwa changamoto walizonazo wavuvi wadogo na kujifunza mbinu za kisasa za kuvua pamoja na matumizi ya teknolojia .

Kwa tanzania wavuvi wadogo asilimia 95% na wameweza kujiajili na kuajili wengine zaidi ya ajira laki mbili therathini na sita elfu na fedha wanazochangia kwa mwaka tilioni 3.4 na kwa fedha za kigeni bilioni tano na tisa, Waziri wa uvuvi na  mifugo Abdallah Ulega  amemshukuru na kumpongeza rais Dr Samia  kwa kukuza na kuimarisha dipromasia ya uchumi ndio maana tanzania ikapewa nafasi ya kuandaa mkutano wa wavuvi wadogo kwa bara  la Afrika.

Mkutano huu utachochea wavuvi wadogo wa tanzania kupata masoko ya kuuza bidhaa zao kimataifa,pia itachochea kuwepo na mabadiriko ya sera na mihongozo kwa wavuvi wadogo watanzania na Afrika kwa ujumla  .pia tanzania itapata fursa ya kuwashawishi watu kuja kuwekeza kwenye sekta ya uvuvi. Amesema haya wakati wa kuzungumza na wanahabari jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

Wednesday 22 May 2024

HER INITIATIVE YAWAKOMBOA WANAWAKE KIUCHUMI


Daniel Robert Head and Communication Officer amesema wameweza kuwakomboa na kuwakwamua wasichana kiuchumi kupitia Digital Platform mfano Panda Chart, Ongea App mpaka sasa Wanawake, Wasichana na Mabinti wapatao 5270 kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Lindi na Pwani wametafutia masoko lakini pia wameweza kuwatengenezea Platform pindi wanapotafuta kazi ikitokea wanatakiwa kutoa rushwa ya ngono watoe taarifa, amsema haya kwenye wiki ya bunifu iliyoandaliwa na COSTECH jiji Dar es Salaam ukumbiwa JNICC.

Habari Picha na Ally Thabiti.  

TAI YAWAKOMBOA WASICHANA


HAIKA MBOYA Human Resource and Administration amesema fanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa elimu ya afya ya uzazi wanawake na wasichana lengo waweze kukabiliana na chanamoto mbalimbali katika makuzi yao na wajuwe namna ya kuweza kujitunza kipindi cha mabadiliko ya kimwili inavyofika kila mwezi.

Ameitaka jamii kukaa karibu na mabinti zao wanapofikia kipindi cha ukuwaji wa kimwili wanamradi wa OKY pia elimu hii ya afya ya uzazi wanatoa mashuleni na mikoa waliyifikia Dar es Salaam pamoja na Arusha kwenye jamii ya wafugaji wa kimasai Haika Mboya amesema pia wamewafikia watu wenye ulemavu wa aina zote amesema haya jiji Dar es Salaam kwenye ukumbi wa JNICC katika wiki ya ubunifu iliyoandaliwa na COSTECH.

Habari Picha na Ally Thabiti 

BARAZA LA ULINZI NA USALAMA LA AFRIKA KUKUTANA TANZANIA MAY 25


Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na kati January Makamba amesema tarehe 25/05/2024 chombo cha baraza la ulinzi na usalama kwa Afrika lenye wanachama nchi kumi na tano 15 watakutana nchini Tanzania jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa JNICC lengo la kukutana kwa baraza hili ni kujadiri migogoro iliyopo kwenye nchi za Afrika.

Na nafasi za wanawake katika uwongozi na namna ya kujikwamua kiuchumi na kufanya maazimisho ya baraza hili la ulinzi na usalama la Afrika ambako lilianzishwa tarehe 25/05/2004 kwasasa limetimiza mika 20 katika mkutano wa baraza hili la ulinzi na usalama Rais Dr Samia Suluhu Hassan atakuwa mwenyekiti wa mkutano huu hii yote inatokana na Tanzania kuwa kitovu cha amani Afrika na Duniani kote.

Pia Tanzania imekuwa ni nchi ya kuongonza harakati za kupigania uhuru kwa nchi za Afrika na kuwa suluhishi wa migogoro kwenye bara la Afrika tangu enzi za Hayati Rias Nyerere, Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete na Rais Magufuri na sasa Rais Dkt Samia.

Waziri wa Mambo nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kati amesema mkutano wa baraza la ulinzi na usalama wa Afrika utauzuliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa amesema haya kwenye ofisi ya wizara ya mambo ya nje zilizopo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Habari Picha na Ally Thabiti

Tuesday 21 May 2024

UN WOMEN BUNIFU ZAO ZATATUWA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE


 Michael Jerry Pogramme Analyst-Women's Economic Empowerment amesema bunifu wanazozifanya zinatatuwa kwa kiasi kikubwa changamoto wanazokutana nazo wajasilia Mali wanawake na wasichana. lengo kubwa ni kuwainuwa kiuchumi wajasiliamali wanawake na wasichana  ambako UN WOMEN imewafikia wanawake Mia moja 100 tanzania bara na Zanzibar kwa kuwapa mafunzo namna ya kutumia teknolojia ya mitandao ili waweze kujinasua katika umasikini .

Michael Jerry amesema kundi la watu wenye ulemavu kupitia bunifu zao awajaliacha nyuma kwani UN WOMEN  wamebuni njia ya sauti kwaajili ya kuwafikia watu wasiiona amesema haya kwenye wiki ya bunifu yalioandaliwa na COSTECH jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit