Kama inavyoonekana Pichani Jiko linalotumia mkaa mbadala pamoja na mkaa wennyewe mbadala kwenye viwanja vya sabasaba maonyesho jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
TIRDO imetoa mafunzo kwenye mikoa 12 juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pia kwa upande mwingine TIRDO inatoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wa aina zote na kuwafanyia hatamizi amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yaliofanyika jijini dar es salaam .
Habari picha na Victoria Stanslaus
Majaliwa Kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania amesema maonyesho ya Sabasaba ya 49 ambayo yamefanyika wilayani temeke jijini dar es salaam yamekuwa yenye tija kwa Wajasiliamali,Wafanya biashara wadogo ,Wakati na Wakubwa kwani wameweza kutangaza bidhaa zao kitaifa na kimataifa pia wamepata masoko ndani ya nchi na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema sekta ya utalii imetangazwa vyema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 na yamepelekea kuvutia walii kuja kutaliina kuwekeza ,vile vile ameupongeza uongozi wa TANTRADE chini ya Mkurugenzi Mkuu Bi Latifa kwa ubunifu wake kwa kuyafanya maonyesho ya Sabasaba ya 49 kwa njia ya kidigitali .
Bi Latifa Muhamed amepongezwa na Waziri Mkuu Majaliwa kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa tanzania kwa kuweka mifumo imala ya kiteknolojia kwa waombaji maeneo ya kufanyia biashara zao na kununua tiketi kwa njia ya mtandao amesema haya wakati akifunga maonyesho ya Sabasaba ya 49 yaliofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam kuanzia tarehe 28 mwezi6 2025 na hatimae yamefungwa na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa tarehe 13 mwezi 7 mwaka 2025.
Habari na Ally Thabit Mbungo
TBA inajenga nyumba rafiki na wezeshi kwa makundi yote kwa watumishi wa serikali wanapangishwa nyumba kwa kiasi cha shiringi milioni moja nawasio wa serikali milioni moja na laki tano . TBA wameweka vutasa janja kwenye milango lengo ni kukabiliana na kuwadhibiti wapangaji ambao awalipi kodi.
Amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es.
Habari picha na Victoria Stanslaus.
Kama Inavyoonekana Kitanda .Mito, Taulo ,Mito ya duara na Vishikizia miguu vyote vinapatikana kwenye TANFOAM LIMITED vilevile TANFOAM wana vitanda pamoja na magodoro ambayo ni rafiki kwa watu wenye changamoto ya uti wa mgongo .
Hivi vyote vinapatikana ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Karume kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam. Pia wanapatikana kwa mawakala wao waliopo nchi nzima tanzania na kwenye maduka yao yote.
Habari picha na Ally Thabit
Daniel Philipo Marko Afisa Mauzo wa Kampuni ya Tonfoam amesema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 kampuni yao imeleta bidhaa zenye ubora na zenye gharama nafuu kwa wateja wa jumla na lejaleja . Miongoni mwa bidhaa ambazo wamezileta kampuni ya Tanfoam Magodoro,Vitanda,Taulo, Mito na Mashuka .
Afisa Mauzo amesema kulingana na msimu huu wa Sabasaba kuna punguzo la bidhaa zao kwa asilimia 10 kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7 2025 mpaka tarehè 31 mwezi wa 7 mwaka 2025.Kampuni hii ya Tanfoam ina miaka 55 tangu kuanzishwa ,Pia ina maduka yao binausi mfano Masaki,Vingunguti,Tegeta na ina mawakqla tanzania nzima kanda ya Magharibi ,Nyanda za juu kusini,Kanda ya kaskazini,Kanda ya kati ,Kanda ya kati na kanda ya Mashariki.
Licha Tanfoam kufanya biashara vilevile inatoa fursa kwa watu kwa kuwaajili ama kujiajili wenyewe kwa kuwapa bidhaa zao kwa makubaliano ivyo ametoa rai kwa vijana na watu wengineo kutumia kampuni ya Tanfoam ili wajikwamuwe kiuchumi na amewataka kutembelea viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Karume watakutana na watoa huduma wa kampuni ya TANFOAM ambako watawahudumia kwa uraisi.
Ametoa wito kwa watu kutumia bidhaa za Tanfoam kwani zina ubora amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 ndani ya viwanja vya Sabasaba wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo