Dr Mujuni Kabululu Kaimu Mkuu Kitengo cha Kuifadhi Nasaba za Mimea Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania amempongeza rais Dr Samia kwa kuweza kununua ndege kwaajili ya kupambana na kuwadhibiti Viwavijeshi,Kweleakwelea na Nzige .
Ndege hii imekuwa mkombozi kwa wakulima ambao mazao yao yalikuwa yanaaribiwa na vivamizi hata ivyo serikali itaepukana na gharama ya kukodi ndege nchi za nje kwaajili ya kudhibiti kwelea Kwelea,Viwa vijashi , Nzige na Panya .
Dr Mujuni amesema Mamlaka yao inatoa vibali vya kuingiza na kupeleka nje ya nchi mazao vilevile Mamlaka hii inatoa vibali vya kuingiza viwatilifu na kusambaza teknolojia kwa wakulima na wanatoa elimu kupitia Almashauri kwa wakulima namna ya kutumia viwatilifu kwenye mazao yao .
Pia wanatumia redio,TV,Vipeperushi na Mafunzo mbalimbali kwa wakulima anawataka watu wote kufika kwenye banda la Wizara ya Kilimo na kutembelea Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment