Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TANTRADE Latifa Muhamed amesma ubunifu alioufanya na maboresho alioyafanya ndani ya TANTRADE yamepelekea TANTRADE kuwa mpya na ya kisasa ndio maana inang'ara kitaifa na kimataifa na kupelekea wafabiashara na wawekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali.
Mkurugenzi ZLatifa Muhamed amesema ameamuwa kuweka mifumo ya Tehama kwa watu wanaoitaji huduma za TANTRADE na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kieletronik Lengo fedha ya serikali iingie moja kwa moja serikalini hili kusiwe na ubadhirifu na zisipotee na hili TANTRADE imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Vilevile TANTRADE imefungua matawi Mwanza ,Arusha,Mbeya,Dodoma na Zanzibar Lengo kuwafikia wateja kwa uraisi. TANTRADE ndani ya viwanja vya Sabasaba kutajengwa majengo ya kisasa ambako magari yatakuwa na sehemu ya kupaki,Sehemu ya watoto kucheza na biashara zitakuwa zinafanyika wakati wote.
Latifa Muhamed anatekeleza kwa vitendo farsafa na maono ya rais Dr Samia na huku akimpongeza rais Dr Samia kwa kuiwezesha TANTRADE kufanya mabadiriko amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam .
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment