Saturday, 5 July 2025

PPRA YAFUNGUA FURSA KWA WATANZANIA


 Mkurugenzi  Mkuu wa PPRA Denisi Simba amewataka watanzania kuchangamkia fursa  za Uzabuni wa tenda mbalimbali zinazotolewa na PPRA  kwani serikali imetenga kiasi cha tilioni 38  kwaajili ya wale wote wanaopata tenda za serikali .

Denisi Simba amesema PPRA  wameweka mazingira rafiki na wezeshi kwa makundi yote ikiwemo wanawake ,vijana,wazee na Watu wenye ulemavu Pia amewataka watu watembelee banda la PPRA  kwenye maonyesho ya 49 ya sabasaba yanayofanyika jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit Mbungo 

No comments:

Post a Comment