Monday, 7 July 2025

LATRA CCC YATOA SIRI NZITO TIKETI MTANDAO


 Katibu Mkuu Mtendaji wa Latra Ccc Daud Daud ameeleza faida za kutumia Tiketi Mtandao ambako kwa wamiliki wa mabasi inawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata taarifa sahihi za watu waliopanda kwenye mabasi yao  Pia pesa wanakusanya kwa wakati kwa upande wa abiria  wanaepukana na usumbufu wa kuuziwa tiketi mala mbili mbili.

Ametoa wito kwa wamiliki wa mabasi kutekeleza kwa vitendo kanuni ya kutumia tiketi mtandao na kwa abiria wazingatie matumizi ya tiketi mtandao kwani itaepusha kupandishiwa nauli kiolela olela amesema haya kwenye maonyesho ya  Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment