Gonsalva Lungu ni Msichana Mwenye Ulemavu wa viungo ambae amehitimu mafunzo ya Ushonaji Chuo cha Veta Songea ndani ya miaka miwili ambako amefungua ofisi ya ushonaji songea mjini eneo la mshangano Licha ya kuwa mlemavu kwenye ofisi yake ameweza kuajili watu wawili ambao awana ulemavu na kuwalipa posho kila mwezi.
Na yeye mwenyewe ameweza kijitegemea katika maisha yake anaishukuru Veta Songea kwa kumlejeshea tumaini lake la maisha licha yakuwa mlemavu anawataka wazazi na walezi kutowafungia ndani watu wenye ulemavu hivyo wawapeleke shuleni ama kwenye Vyuo vya Veta huku akiwataka watu wenye ulemavu kutokata tamaa .Wafike kwenye Vyuo vya Veta ili wapate mafunzo ya fani mbalimbali kwani Veta ndio kimbilio la watu wenye ulemavu.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
No comments:
Post a Comment