Afisa wa Leseni Tume ya Madini Egera Doto amewataka Watu ususani watanzania kuchangamkia fursa za kuwekeza kwenye sekta ya madini , Ambako tume ya madini imeweka mazingira rafiki na wezeshi kwa mtu ama kikundi cha watu anaehitaji kuwekeza kwenye sekta hii.
Leseni mbalimbali tume ya madini inatoa miongoni mwao ni Leseni ya Utafiti wa Madini,Leseni ya uchimbaji wa madini , Uchenjuaji madini, Usafishaji wa madini na zinginezo ambako tume ya madini inatoa Leseni kupitia mifumo ya Tehama Lengo kuondoa urasimu na kuarakisha kupatikana kwa muda mfupi ambako ndani ya mwezi mmoja unapata Leseni.
Egera Doto amewataka watu kufika kwenye banda la tume ya madini ndani ya viwanja vya maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
No comments:
Post a Comment