Kijana Mwenye Changamoto ya Kuto Ona Ally Thabit Mbungo ameupongeza Uongozi wa Latra Ccc kwa kuweza kuwajali na kuwazingatia watu wenye ulemavu wa aina zote kwa kuandika majarida kwa kutumia maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasio Ona kama inavyoonekana pichani .Ambako sisi tusio ona tunapata elimu na kujifunza maswala ya Latra Ccc kwa njia raisi na nyepesi bila utegemezi .
Pia Latra Ccc wameweka maandishi makubwa kwenye watu wenye Uoni hafifu vilevile watu wenye Uziwi wanapata elimu kutoka Latra Ccc kupitia Lugha ya Alama.
Ni vyema watu wafike kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment