Afisa Masoko Mwandamizi Sido Makao Makuu Christopha Eduwadi Mwakyusa amesema katika kuunga mkono juhudi na jitihada za Dr Samia ifikapo mwaka 2030 watu wote nchini tanzania watumie nishati safi ya kupikia ambako upande wao Sido wanatoa mafunzo ya kutengeneza mkaa mbadala Mkaa huu auchafuhi mazingira .
Pia Sido imewaandaa wataalam wa kutengeneza majiko ambayo yanatumia mkaa mbadala vilevile Sido wanatengeneza mashine na vipuri vya majiko yote Mali ghafi zake zinatoka hapa nchini tanzania .
Sido wameweza kuwafikia Mama Lishe na Baba Lishe kwa kuwapa elimu na mafunzo namna ya kutumia nishati safi ya kupikia ,Taasisi , kampuni,mashuleni,kwenye kambi za jeshi ,polisi na magerezani Sido imeweza kupeleka majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia huku akiwataka watu kutembelea kwenye banda la Sido ili wanunue majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia kwenye viwanja vya Sabasaba Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam katika maonyesho ya 49.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.
No comments:
Post a Comment