Friday, 11 July 2025

TARI YAJA NA MUAROBAINI KWA WAKULIMA


 Dr Filson Kagimbo Mkurugenzi Mkuu wa TARI  Kigoma amesema wakulima wengi walikuwa wanakumbwa na changamoto za kulima bila tija ivyo Taasisi ya Kilimo Tanzania TARI  imeamuwa kufanya tafiti na kuwapelekea teknolojia wakulima.

Moja ya majukumu ya TARI  kufanya utafiti wa Afya ya Udongo,Utafiti wa mazao na Ugunduzi wa mbegu bora,Kulinda mazao yasishambuliwe na wadudu pamoja na magonjwa mbalimbali, Namna ya kuongeza thamani kwenye mazao na kutunza pia wanawafundisha na kufanya utafiti wa za kuifadhi na kusindika mazao pamoja na kuwapelekea teknolojia mbalimbali.

Amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilayani temeke jijini dar es salaam  kwenye  banda la TARI. 

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment