Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPRA Josefu Muozi amesema watu wenye ulemavu katika kupata fursa za tenda za PPRA wamefikiwa kwa kiwango kikubwa huu ni mpango maalum ulioandaliwa na serikali tangu mwaka 2011 na sheria ya PPRA ikafanyiwa maboresho mwaka 2023 ambako maboresho haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye ulemavu wa aina zote kupata zabuni za tenda za PPRA.
Pia PPRA imeandaa majarida yenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya walemavu wasio Ona na vifaa vya kurekodia sauti zana hizi zimewezesha watu wenye ulemavu kupata elimu na uwelewa kuhusu zabuni na tenda zinazotolewa na PPRA vilevile PPRA inatoa elimu kwa watu wote kupitia redio,tv,magazeti,na makongamano pamoja na semina kupitia taasisi za watu wenye ulemavu.
Josefu Muozi amewataka watu kutembelea banda la PPRA viwanja vya sabasaba maonyesho Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya 49 habari picha na Victoria Stanslaus.
No comments:
Post a Comment