Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakirishi Zanzibar Dr Hoseni Mwinyi amewapongeza viongozi wa TANTRADE chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Ratifa Ali Muhammed kwa kutafasiri kwa vitendo farsafa ya Dr Samia na maono yake ya kukuza biashara ya mtu mmoja mmoja au makundi mbalimbali kwa kuweza kufanya ubunifu kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa kuweka mifumo ya kujisajili kwaajili ya kupata mabanda na ukataji tiketi kwa njia ya mtandao ambako inasaidia fedha ya serikali kuingia moja kwa moja bila kupitia mikononi mwa watu.
Pia wameweza kukamilisha mpango wa ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha maonyesho ya sabasaba .
Uwepo wa ubunifu wa maonyesho wa bidhaa za nchi za kigeni mfano siku China ,Japani huku ni kukuza dipromasia ya Kiuchumi. Rais wa Zanzibar ameiakikishia TANTRADE yeye na rais Samia wataendelea kuwapa ushirikiano wa Ali na mali na serikali ina mikakati mikubwa juu ya TANTRADE.
Rais amezindua Nembo ya Bidhaa za Tanzania ambako hii ni alama ya kutamburisha bidhaa zetu kitaifa na kimataifa amesema haya tarehe 7 mwezi wa 7 2025 ndani ya viwanja vya Sabasaba wilayani temeke jijini dar es salaam wakati alipofungua maonyesho ya sabasaba ya 49.
Habari na Ally Thabit Mbungo.
No comments:
Post a Comment