Majaliwa Kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania amesema maonyesho ya Sabasaba ya 49 ambayo yamefanyika wilayani temeke jijini dar es salaam yamekuwa yenye tija kwa Wajasiliamali,Wafanya biashara wadogo ,Wakati na Wakubwa kwani wameweza kutangaza bidhaa zao kitaifa na kimataifa pia wamepata masoko ndani ya nchi na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema sekta ya utalii imetangazwa vyema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 na yamepelekea kuvutia walii kuja kutaliina kuwekeza ,vile vile ameupongeza uongozi wa TANTRADE chini ya Mkurugenzi Mkuu Bi Latifa kwa ubunifu wake kwa kuyafanya maonyesho ya Sabasaba ya 49 kwa njia ya kidigitali .
Bi Latifa Muhamed amepongezwa na Waziri Mkuu Majaliwa kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa tanzania kwa kuweka mifumo imala ya kiteknolojia kwa waombaji maeneo ya kufanyia biashara zao na kununua tiketi kwa njia ya mtandao amesema haya wakati akifunga maonyesho ya Sabasaba ya 49 yaliofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam kuanzia tarehe 28 mwezi6 2025 na hatimae yamefungwa na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa tarehe 13 mwezi 7 mwaka 2025.
Habari na Ally Thabit Mbungo
No comments:
Post a Comment