Monday, 7 July 2025

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA AWAMU YA SITA YAVUNJA REKODI NA KUTIA FOLA

 Katibu Mkuu wa  Baraza  la Mitihani  nchini tanzania amesema matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Kidato cha sita yamekuwa yenyekuleta faida na faraja kwa kiasi kikubwa kwa ufahuru kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma  .Uongozi wa rais Dr Samia awamu hii ya sita ya uongozi wake ameweza kufanya maboresho na mabadiriko kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya elimu kwenye ujenzi wa madarasa ,mabweni ,nyumba za walimu ,kidato cha tano na cha sita awalipi ada haya yote yamepelekea wanafunzi waliofanya mitihani ya taifa ya kidato cha sita ufahuru wao kuongezeka na kuwa mzuri.

Ufahuru wa somo la Hisabati umeongezeka ambako asilimia 73 ukilinganisha na miaka ya nyuma , Walio futiwa matokeo ya kidato cha sita ni wanafunzi 70 kwa sababu za udanganyifu na sababu zinginezo na mmoja kafutiwa matokeo kwa mitihani ya Ualimu na kupelekea jumla ya waliofufiwa matokeo  kuwa 71 ambako 70 kidato cha sita na  mmoja ni mitihani ya Ualimu.

Haya ametangaza Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Dr Mohamedi Ally akiwa Zanzibar. 

Habari na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment