Daniel Philipo Marko Afisa Mauzo wa Kampuni ya Tonfoam amesema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 kampuni yao imeleta bidhaa zenye ubora na zenye gharama nafuu kwa wateja wa jumla na lejaleja . Miongoni mwa bidhaa ambazo wamezileta kampuni ya Tanfoam Magodoro,Vitanda,Taulo, Mito na Mashuka .
Afisa Mauzo amesema kulingana na msimu huu wa Sabasaba kuna punguzo la bidhaa zao kwa asilimia 10 kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7 2025 mpaka tarehè 31 mwezi wa 7 mwaka 2025.Kampuni hii ya Tanfoam ina miaka 55 tangu kuanzishwa ,Pia ina maduka yao binausi mfano Masaki,Vingunguti,Tegeta na ina mawakqla tanzania nzima kanda ya Magharibi ,Nyanda za juu kusini,Kanda ya kaskazini,Kanda ya kati ,Kanda ya kati na kanda ya Mashariki.
Licha Tanfoam kufanya biashara vilevile inatoa fursa kwa watu kwa kuwaajili ama kujiajili wenyewe kwa kuwapa bidhaa zao kwa makubaliano ivyo ametoa rai kwa vijana na watu wengineo kutumia kampuni ya Tanfoam ili wajikwamuwe kiuchumi na amewataka kutembelea viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Karume watakutana na watoa huduma wa kampuni ya TANFOAM ambako watawahudumia kwa uraisi.
Ametoa wito kwa watu kutumia bidhaa za Tanfoam kwani zina ubora amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 ndani ya viwanja vya Sabasaba wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.
No comments:
Post a Comment