Mwalimu Kintu anaefundisha Watu wenye Ulemavu Chuo cha Veta amesema katika kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu ya fani mbalimbali Veta Dar es salaam ndio wa kwanza kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu.
Mwalimu Kintu amesema iliwachukuwa miaka saba kufanya ushawishi kwa Vyuo vya Veta mikoa ya tanzania kuwapokea na kuwafundisha watu wenye ulemavu ambako kwa sasa amejawa na furaha kwa kuona mafunzo ya fani mbali mbali yanatolewa kwenye Vyuo vya Veta vyote nchini kwa watu wenye ulemavu wa aina zote.
Mwalimu Kintu amesema kuwepo kwa sera inayowatambua watu wenye ulemavu kuwa na wao wana haki ya kupata mafunzo kupitia Veta ni jambo zuri.
Habari picha na Ally Thabit.
No comments:
Post a Comment