Afisa wa Chuo Kikuu cha CBE Jakrene E Kaaya anawataka watu kujiunga na Chuo cha CBE ambako chuo Kikuu hichi kina matawi Dodoma,Mbeya,Arusha na Dar es salaam ambako mtu anaweza kujisajili na kujiunga na matawi ya chuo Kikuu cha CBE kwenye maeneo yalio tajwa , Viwango mbalimbali vya elimu vinatolewa kwa ngazi ya Cheti, Diploma ,Digree,Master na PHD vilevile Kozi ya ICT inatolewa kwa ngazi zote Ambako inawezesha watu kuendana na teknolojia za kisasa.
Kozi hizi zinatolewa Asubuhi mpaka jioha nawengine wanaingia joini mpaka usiku Pia Chuokikuu cha CBE wanatoa kozi za muda mfupi mfano . Wanashirikiana na Latra kwaajili ya kutoa mafunzo kwa watoa huduma kwenye mabasi na madereva wa bodaboda .
Bi jakrene E Kaaya anawataka watu kutembelea banda la CBE ili waweze kujisajili kwaajili ya kupata elimu Chuokikuu cha CBE ambako chuo hiki kina miaka 60 amesma haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilaya ya temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment