Kama inavyoonekana Pichani Jiko linalotumia mkaa mbadala pamoja na mkaa wennyewe mbadala kwenye viwanja vya sabasaba maonyesho jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
TIRDO imetoa mafunzo kwenye mikoa 12 juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pia kwa upande mwingine TIRDO inatoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wa aina zote na kuwafanyia hatamizi amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yaliofanyika jijini dar es salaam .
Habari picha na Victoria Stanslaus
Majaliwa Kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania amesema maonyesho ya Sabasaba ya 49 ambayo yamefanyika wilayani temeke jijini dar es salaam yamekuwa yenye tija kwa Wajasiliamali,Wafanya biashara wadogo ,Wakati na Wakubwa kwani wameweza kutangaza bidhaa zao kitaifa na kimataifa pia wamepata masoko ndani ya nchi na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema sekta ya utalii imetangazwa vyema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 na yamepelekea kuvutia walii kuja kutaliina kuwekeza ,vile vile ameupongeza uongozi wa TANTRADE chini ya Mkurugenzi Mkuu Bi Latifa kwa ubunifu wake kwa kuyafanya maonyesho ya Sabasaba ya 49 kwa njia ya kidigitali .
Bi Latifa Muhamed amepongezwa na Waziri Mkuu Majaliwa kasimu Majaliwa Waziri Mkuu wa tanzania kwa kuweka mifumo imala ya kiteknolojia kwa waombaji maeneo ya kufanyia biashara zao na kununua tiketi kwa njia ya mtandao amesema haya wakati akifunga maonyesho ya Sabasaba ya 49 yaliofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam kuanzia tarehe 28 mwezi6 2025 na hatimae yamefungwa na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa tarehe 13 mwezi 7 mwaka 2025.
Habari na Ally Thabit Mbungo
TBA inajenga nyumba rafiki na wezeshi kwa makundi yote kwa watumishi wa serikali wanapangishwa nyumba kwa kiasi cha shiringi milioni moja nawasio wa serikali milioni moja na laki tano . TBA wameweka vutasa janja kwenye milango lengo ni kukabiliana na kuwadhibiti wapangaji ambao awalipi kodi.
Amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es.
Habari picha na Victoria Stanslaus.
Kama Inavyoonekana Kitanda .Mito, Taulo ,Mito ya duara na Vishikizia miguu vyote vinapatikana kwenye TANFOAM LIMITED vilevile TANFOAM wana vitanda pamoja na magodoro ambayo ni rafiki kwa watu wenye changamoto ya uti wa mgongo .
Hivi vyote vinapatikana ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Karume kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam. Pia wanapatikana kwa mawakala wao waliopo nchi nzima tanzania na kwenye maduka yao yote.
Habari picha na Ally Thabit
Daniel Philipo Marko Afisa Mauzo wa Kampuni ya Tonfoam amesema kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 kampuni yao imeleta bidhaa zenye ubora na zenye gharama nafuu kwa wateja wa jumla na lejaleja . Miongoni mwa bidhaa ambazo wamezileta kampuni ya Tanfoam Magodoro,Vitanda,Taulo, Mito na Mashuka .
Afisa Mauzo amesema kulingana na msimu huu wa Sabasaba kuna punguzo la bidhaa zao kwa asilimia 10 kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7 2025 mpaka tarehè 31 mwezi wa 7 mwaka 2025.Kampuni hii ya Tanfoam ina miaka 55 tangu kuanzishwa ,Pia ina maduka yao binausi mfano Masaki,Vingunguti,Tegeta na ina mawakqla tanzania nzima kanda ya Magharibi ,Nyanda za juu kusini,Kanda ya kaskazini,Kanda ya kati ,Kanda ya kati na kanda ya Mashariki.
Licha Tanfoam kufanya biashara vilevile inatoa fursa kwa watu kwa kuwaajili ama kujiajili wenyewe kwa kuwapa bidhaa zao kwa makubaliano ivyo ametoa rai kwa vijana na watu wengineo kutumia kampuni ya Tanfoam ili wajikwamuwe kiuchumi na amewataka kutembelea viwanja vya Sabasaba kwenye banda la Karume watakutana na watoa huduma wa kampuni ya TANFOAM ambako watawahudumia kwa uraisi.
Ametoa wito kwa watu kutumia bidhaa za Tanfoam kwani zina ubora amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 ndani ya viwanja vya Sabasaba wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Ivyoamesema bei zao ni rafiki na nafuu kwa wateja wao na pia kahawa inawawezesha watu kupata ajira amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Kahawa yao aina ya Arabika ina ubora ivyo wanawataka watanzania na wasio watanzania kutumia kahawa yao aina ya Arabika . Chama kikuu cha Wakulima Mkoani MARA WAMACU LIMITED itafanya ka'i ya kufungua masoko jijini dar es salaam na mikoa mingine kwaajili ya kuwafikia wateja wao amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 kwenye banda la Wizara ya Kilimo .
Habari picha na Ally Thabit
Ndege hii imekuwa mkombozi kwa wakulima ambao mazao yao yalikuwa yanaaribiwa na vivamizi hata ivyo serikali itaepukana na gharama ya kukodi ndege nchi za nje kwaajili ya kudhibiti kwelea Kwelea,Viwa vijashi , Nzige na Panya .
Dr Mujuni amesema Mamlaka yao inatoa vibali vya kuingiza na kupeleka nje ya nchi mazao vilevile Mamlaka hii inatoa vibali vya kuingiza viwatilifu na kusambaza teknolojia kwa wakulima na wanatoa elimu kupitia Almashauri kwa wakulima namna ya kutumia viwatilifu kwenye mazao yao .
Pia wanatumia redio,TV,Vipeperushi na Mafunzo mbalimbali kwa wakulima anawataka watu wote kufika kwenye banda la Wizara ya Kilimo na kutembelea Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Moja ya majukumu ya TARI kufanya utafiti wa Afya ya Udongo,Utafiti wa mazao na Ugunduzi wa mbegu bora,Kulinda mazao yasishambuliwe na wadudu pamoja na magonjwa mbalimbali, Namna ya kuongeza thamani kwenye mazao na kutunza pia wanawafundisha na kufanya utafiti wa za kuifadhi na kusindika mazao pamoja na kuwapelekea teknolojia mbalimbali.
Amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilayani temeke jijini dar es salaam kwenye banda la TARI.
Habari picha na Ally Thabit
Maombi ya watu kutaka kuwepo kwa Tembo na Twiga watafanyia kazi kutokana na mazingira ya Ikolojia hata ivyo amewataka watu kufika eneo la Pande lililopo Bunju ambako kuna hifadhi ya wanyamapori ambako kiingilio elfu 11800 .
Habari picha na Victoria Stanslaus
Kama inavyoonekana pichani mazao ya Mpunga na Korosho amesema haya ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye banda la CBE kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Petro amewaakikishia watu kuwa mfumo huu ni salama huku akitoa wito watu wajiunge na Chuo Kikuu cha CBE amesema haya ndani ya banda la CBE lililopo kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilaya ya temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Kozi hizi zinatolewa Asubuhi mpaka jioha nawengine wanaingia joini mpaka usiku Pia Chuokikuu cha CBE wanatoa kozi za muda mfupi mfano . Wanashirikiana na Latra kwaajili ya kutoa mafunzo kwa watoa huduma kwenye mabasi na madereva wa bodaboda .
Bi jakrene E Kaaya anawataka watu kutembelea banda la CBE ili waweze kujisajili kwaajili ya kupata elimu Chuokikuu cha CBE ambako chuo hiki kina miaka 60 amesma haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 wilaya ya temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
Mkurugenzi ZLatifa Muhamed amesema ameamuwa kuweka mifumo ya Tehama kwa watu wanaoitaji huduma za TANTRADE na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kieletronik Lengo fedha ya serikali iingie moja kwa moja serikalini hili kusiwe na ubadhirifu na zisipotee na hili TANTRADE imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Vilevile TANTRADE imefungua matawi Mwanza ,Arusha,Mbeya,Dodoma na Zanzibar Lengo kuwafikia wateja kwa uraisi. TANTRADE ndani ya viwanja vya Sabasaba kutajengwa majengo ya kisasa ambako magari yatakuwa na sehemu ya kupaki,Sehemu ya watoto kucheza na biashara zitakuwa zinafanyika wakati wote.
Latifa Muhamed anatekeleza kwa vitendo farsafa na maono ya rais Dr Samia na huku akimpongeza rais Dr Samia kwa kuiwezesha TANTRADE kufanya mabadiriko amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam .
Habari picha na Victoria Stanslaus
Meneja Mahusiano na Mawasiliano Tume ya Madini Greyson amesema tume ya madini nchini tanzania imewafikia na itaendelea kuwafikia watu wenye ulemavu wa aina zote pia tume ya madini imefungua masoko 43 na vituo vya ununuzi wa madini kwa tanzania 109 Lengo la serikali kufanya hivi ni kutoa usumbufu kwa wauzaji na wanunuzi wa madini.
Leseni mbalimbali tume ya madini inatoa miongoni mwao ni Leseni ya Utafiti wa Madini,Leseni ya uchimbaji wa madini , Uchenjuaji madini, Usafishaji wa madini na zinginezo ambako tume ya madini inatoa Leseni kupitia mifumo ya Tehama Lengo kuondoa urasimu na kuarakisha kupatikana kwa muda mfupi ambako ndani ya mwezi mmoja unapata Leseni.
Egera Doto amewataka watu kufika kwenye banda la tume ya madini ndani ya viwanja vya maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakirishi Zanzibar Dr Hoseni Mwinyi amewapongeza viongozi wa TANTRADE chini ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Ratifa Ali Muhammed kwa kutafasiri kwa vitendo farsafa ya Dr Samia na maono yake ya kukuza biashara ya mtu mmoja mmoja au makundi mbalimbali kwa kuweza kufanya ubunifu kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa kuweka mifumo ya kujisajili kwaajili ya kupata mabanda na ukataji tiketi kwa njia ya mtandao ambako inasaidia fedha ya serikali kuingia moja kwa moja bila kupitia mikononi mwa watu.
Pia wameweza kukamilisha mpango wa ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha maonyesho ya sabasaba .
Uwepo wa ubunifu wa maonyesho wa bidhaa za nchi za kigeni mfano siku China ,Japani huku ni kukuza dipromasia ya Kiuchumi. Rais wa Zanzibar ameiakikishia TANTRADE yeye na rais Samia wataendelea kuwapa ushirikiano wa Ali na mali na serikali ina mikakati mikubwa juu ya TANTRADE.
Rais amezindua Nembo ya Bidhaa za Tanzania ambako hii ni alama ya kutamburisha bidhaa zetu kitaifa na kimataifa amesema haya tarehe 7 mwezi wa 7 2025 ndani ya viwanja vya Sabasaba wilayani temeke jijini dar es salaam wakati alipofungua maonyesho ya sabasaba ya 49.
Habari na Ally Thabit Mbungo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini tanzania amesema matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Kidato cha sita yamekuwa yenyekuleta faida na faraja kwa kiasi kikubwa kwa ufahuru kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma .Uongozi wa rais Dr Samia awamu hii ya sita ya uongozi wake ameweza kufanya maboresho na mabadiriko kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya elimu kwenye ujenzi wa madarasa ,mabweni ,nyumba za walimu ,kidato cha tano na cha sita awalipi ada haya yote yamepelekea wanafunzi waliofanya mitihani ya taifa ya kidato cha sita ufahuru wao kuongezeka na kuwa mzuri.
Ufahuru wa somo la Hisabati umeongezeka ambako asilimia 73 ukilinganisha na miaka ya nyuma , Walio futiwa matokeo ya kidato cha sita ni wanafunzi 70 kwa sababu za udanganyifu na sababu zinginezo na mmoja kafutiwa matokeo kwa mitihani ya Ualimu na kupelekea jumla ya waliofufiwa matokeo kuwa 71 ambako 70 kidato cha sita na mmoja ni mitihani ya Ualimu.
Haya ametangaza Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Dr Mohamedi Ally akiwa Zanzibar.
Habari na Ally Thabit
Kijana Mwenye Changamoto ya Kuto Ona Ally Thabit Mbungo ameupongeza Uongozi wa Latra Ccc kwa kuweza kuwajali na kuwazingatia watu wenye ulemavu wa aina zote kwa kuandika majarida kwa kutumia maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasio Ona kama inavyoonekana pichani .Ambako sisi tusio ona tunapata elimu na kujifunza maswala ya Latra Ccc kwa njia raisi na nyepesi bila utegemezi .
Pia Latra Ccc wameweka maandishi makubwa kwenye watu wenye Uoni hafifu vilevile watu wenye Uziwi wanapata elimu kutoka Latra Ccc kupitia Lugha ya Alama.
Ni vyema watu wafike kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilayani temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
Huku akiwataka abiria kuakikisha kwenye tiketi zao wanaandikiwa taarifa sahihi mwanzo wa safari yake na mwisho wa safari na jina la mmiliki wa basi liandikwe kwa kilefu ili kuepuka kushushwa eneo ambalo ujakusudiwa na ukipata matatizo iweraisi kupata haki zako kupitia kampuni za bima .
Amesema haya kwenye maonyesho ya 49 ndani ya viwanja vya Sabasaba yanayofanyika wilaya ya temeke jijini Dar es salaam. Habari picha na Victoria Stanslaus.
Ametoa wito kwa wamiliki wa mabasi kutekeleza kwa vitendo kanuni ya kutumia tiketi mtandao na kwa abiria wazingatie matumizi ya tiketi mtandao kwani itaepusha kupandishiwa nauli kiolela olela amesema haya kwenye maonyesho ya Sabasaba ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Mwalimu Kintu anaefundisha Watu wenye Ulemavu Chuo cha Veta amesema katika kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu ya fani mbalimbali Veta Dar es salaam ndio wa kwanza kutoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu.
Na yeye mwenyewe ameweza kijitegemea katika maisha yake anaishukuru Veta Songea kwa kumlejeshea tumaini lake la maisha licha yakuwa mlemavu anawataka wazazi na walezi kutowafungia ndani watu wenye ulemavu hivyo wawapeleke shuleni ama kwenye Vyuo vya Veta huku akiwataka watu wenye ulemavu kutokata tamaa .Wafike kwenye Vyuo vya Veta ili wapate mafunzo ya fani mbalimbali kwani Veta ndio kimbilio la watu wenye ulemavu.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Huku akiwataka watu kutembelea banda la Veta kwenye maonyesho ya 49 yanayofanyika wilaya ya temeke jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit
Lengo wajifunze namna ya watu wenye ulemavu wanavyofanya kazi zao na Veta walivyoludisha tumaini la watu wenye ulemavu katika maisha yao .
Habari picha na Victoria Stanslaus
Ameishukuru Veta kwakuweza kuibua matumaini yake ya maisha yake na kukamilika kwa ndoto zake.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watu wenye Ulemavu Veta amesema haya kwenye banda la Veta ndani ya viwanja vya Sabasaba kwenye maonyesho ya 49 Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
Habari picha na Victoria Stanslaus
Habari picha na Victoria Stanslaus.
Pia Sido imewaandaa wataalam wa kutengeneza majiko ambayo yanatumia mkaa mbadala vilevile Sido wanatengeneza mashine na vipuri vya majiko yote Mali ghafi zake zinatoka hapa nchini tanzania .
Sido wameweza kuwafikia Mama Lishe na Baba Lishe kwa kuwapa elimu na mafunzo namna ya kutumia nishati safi ya kupikia ,Taasisi , kampuni,mashuleni,kwenye kambi za jeshi ,polisi na magerezani Sido imeweza kupeleka majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia huku akiwataka watu kutembelea kwenye banda la Sido ili wanunue majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia kwenye viwanja vya Sabasaba Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam katika maonyesho ya 49.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo.
Pia PPRA imeandaa majarida yenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya walemavu wasio Ona na vifaa vya kurekodia sauti zana hizi zimewezesha watu wenye ulemavu kupata elimu na uwelewa kuhusu zabuni na tenda zinazotolewa na PPRA vilevile PPRA inatoa elimu kwa watu wote kupitia redio,tv,magazeti,na makongamano pamoja na semina kupitia taasisi za watu wenye ulemavu.
Josefu Muozi amewataka watu kutembelea banda la PPRA viwanja vya sabasaba maonyesho Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya 49 habari picha na Victoria Stanslaus.
Denisi Simba amesema PPRA wameweka mazingira rafiki na wezeshi kwa makundi yote ikiwemo wanawake ,vijana,wazee na Watu wenye ulemavu Pia amewataka watu watembelee banda la PPRA kwenye maonyesho ya 49 ya sabasaba yanayofanyika jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo