Tuesday, 3 September 2024

WANAFUNZI WAAHIDI MAZITO KWENYE KAMPUNI YA BUDEO NA ECO GREEN


 Christian Mwanafunzi wa Darasa la sita Shule ya Msingi Zanaki anaipongeza Kampuni ya Budeo na Eco Green kwa kuwajengea kizimba cha kutunzia taka kwani kizmba hiki kitawassidia kwa kiasi kikubwa katika kutunza mazingira na itawezesha kwa kiwango kikubwa kuuza taka kupitia kizimba hiki.

Pia kampuni hizi zimewapa elimu ya kutenganisha taka hivyo elimu hii wataipeleka katika jamii lengo jamii iache uchafunzi wa mazingira na jamii itumie taka katika kupata fedha " Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi zanaki anetoa wito kwa serikali ,wadau na jamii kushirikiana na kampuni ya Budeo na Eco Green katika kutunza mazingira na waziwezeshe kifedha ili kukamilisha malengo yao katika kutunza mazingira.

Habari picha na Ally Thabit 

KAMPUNI YA BUDEO YAPATA CHETI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Budeo Khamsini amesema cheti alichokipata kupitia ofisi ya makamu wa rais kinamtambulisha kuwa yeye ni mdau mkubwa na muhimmu katika kutunza mazingira , pia kupitia cheti hichi kitamsaidia kupata fursa mbalimbali. 

Ametoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali waiwezeshe na kuisaidia kifedha kampuni ya Budeo amesema haya kwenye shule za msingi na Secondary Zanaki wakati wa kukabidhi dastibini 30 za kutunzia taka na uzinduzi wa kizimba cha kutunzia taka .

Habari picha na Ally Thabit 

MKURUGENZI WA KAJENJERE AIPONGEZA BUDEO NA ECO GREEN


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajenjere Methiu pia Mwenyekiti wa wakandarasi wa taka amesema ujenzi wa kizimba na ugawaji wa dastibini kwenye shule ya msingi Zanaki na Secondary zanaki utasaidia utunzanzaji wa mazingira na utawezesha shule hizi kupata pesa kupitia taka watakazozikusanya .

Ametoa wito kwa watanzania kuitumia kampuni ya Kajenjere kwaajili ya kukusanya taka zao .

Habari picha na Ally Thabit