Thursday 21 October 2021

MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI ATANGAZA VITA


 James Mbatia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi amewataka Viongozi wa Serikali ya Tanzania,wanasiasa, Viongozi wa Kidini, Viongozi wa kimira na kijadi na watu wote wawapige Vita na wawapige watu wote wanaoalibu UTU wa Watu. 

kwani kutowapiga Vita watasababisha kuvunjika Kwa Amani na utulivu wa nchi yetu ya Tanzania .

Habari picha na Victoria Stanslaus

MENEJA WA TANROAD AHAIDI MAZITO


 Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD wa Mizani amesema Kwa sasa wanafanya makongamano na semina mbalimbali Kwa wadau mbalimbali wa Usafirishaji namna ya kutumia Mizani ambako wameanza elimu Kwa Mkoa wa Dsm na Pwani na wamefurahishwa na mwitikio mkubwa wa wadau wa Usafirishaji na jinsi walivyopokea Mafunzo haya.

Mikoa mingine watakayoenda Lindi ,Mtwara,Dodoma,Singida ,Morogoro,Tanga Iringa,Mbeya Ruvuma,Katavi,Geita,Mwanza,Arusha na Mikoa mingine. Lengo la semina hizi ni kuwaongezea uwelewa na ufahamu  na umuhimu wa kuzingatia Sheria,kanuni na Taratibu za Mizani.

Ametoa wito Kwa wadau wa Usafirishaji wazingatie Uzito unaotakiwa kwenye magari Yao kwaajili ya kutunza na kulinda barabara na madaraja hili yaweze kudumu Kwa muda mrefu.

Kwani wakizingatia haya tutapunguza gharama za ujenzi wa barabara na madaraja ambako Fedha hizi zitasaidia katika kutatuwa Changamoto ya Afya, Elimu,maji na maeneo mengineyo.

Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD amesema haya wakati wa semina na wadau wa Usafirishaji jijini Dsm.

Habari picha  Victoria Stanslaus

TANROAD YAJIVUNIA


 Mkurugenzi wa Matengenezo ya Mizani TANROAD amesema mpaka sasa wameweza kuiboresha na kuimarisha Mizani ya kupinga Nagari .amewataka wadau wa Usafirishaji wazingatie sheria ,kanuni na Taratibu za Mizani .

Lengo la TANROAD kuweka Mizani ya kupinga magari hili kudhibiti Uzito uliopitiliza ,ambako kutaepusha uhalibifu wa barabara na madaraja.

Amesema moja ya jitihada anazofanya kutoa elimu na kufanya semina mbalimbali Kwa wadau wa Usafirishaji.

Habari picha Ally Thabit

MCHUNGAJI ATAKA WATU KUZINGATIA UTU


 Mchungaji Masanja anawataka Watu Wote Kuzingatia UTU kwani Ndio msingi wa Amani pia amekipongeza Chama cha NCCR Mageuzi Kwa kuzinduwa Kampuni ya UTU .

Ivyo amevitaka Vyama vingine kuunga mkono .

Habari picha na Victoria Stanslaus

ZANZIBAR YAIPA TANO TAFFA


 Kiongozi wa ZAFFA Othumani Musa amempongeza raisi wa TAFFA Edwardi Urio Kwa kazi nzuri anayoifanya za kutatuwa Changamoto za wanachama wake na kuwaunganisha ZAFFA na TAFFA kuwa kitu kimoja.

Habari picha na Ally Thabiti

NIC YAFUNGUWA MILANGO


 Kafiti Kafiti , Principal Business Development Officer anawataka watu kuchangamkia huduma ya bima inayotolewa na NIC kwani bei zao ni nafuu .

NIC ina bima mbalimbali ambako mtu yeyote akijiunga atojutia na bima zao ni nafuu ukilinganisha na Kampuni zingine za bima na NIC Awana ubabaishaji kwenye malipo Kwa wateja wao.

Pia NIC wanawaakikishia wanachama wa TAFFA watapata hudhuma Bora .

Habari picha na Victoria Stanslaus

TAFFA YAJA KIVINGINE


 Mwenyekiti wa TAFFA  Edwardi Urio amewataka wanachama wake kujitaidi kutoa michango na amewaaidi kuwa watapata KAZI nyingi, pia amewataka  wanachama wa TAFFA wafanye KAZI Kwa Uweredi.

Habari picha na Victoria Stanslaus

KATIBU WA JUWAKITA AIHASA JAMII

Khanifa Katibu wa JUWAKITA Kinondoni amewataka wanawake wa Kiislamu kuwapeleka watoto kujifunza dini ,nae Mgeni rasmiMarihamu Ditopile ametoa kiasi cha milioni tano kwaajili ya kuwakatia bima watoto wenye Ulemavu na Watoto yatima .

Amewataka watoto wa Kiislam wachangamkie fursa mbalimbali za kiuchumi , huku akitoa wito kwa Uongozi wa JUWAKITA Taifa kusimamia uweredi , maadiri, na Amani iliyopo Tanzania .

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

Wednesday 20 October 2021

JUWAKITA ATOA NENO KWA WANAWAKE


 Mwenyekiti wa JUWAKITA Marihamu wa Wilaya ya Kinondoni amewataka wanawake kujiunga na JUWAKITA ili waweze kupata fursa mbalimbali amesema haya siku ya kusheherekea siku ya Mahazazi ya Mtume Muhamadi.

Habari picha na Victoria Stanslaus

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPEWA BILIONI 29

 

Damask Ndumbalo Waziri wa Maliasili na Utalii anamshukuru raisi Samia Suluhu Hassan Kwa kuipa Wizara yake Fedha za Kitanzania bilioni 29 Kwaajili ya Kupambana na UVIKO 19.

Waziri Ndumbalo amesema Fedha hizi zitatumika kwenye miradi 5 mfano kutoa elimu Kwa waongoza Utalii,kutengeneza vipeperushi na mabango.

Pia amesema fedha hizi zitatumika kwenye Mikoa 26 Tanzania bara, ametoa onyo Kwa watakaoiba fedha hizi hatua Kali zitachukuliwa dhidi Yao ikiwemo kufukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani.

Habari picha na Victoria Stanslaus

Saturday 16 October 2021

MWENYEKITI WA BARAZA LA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR AHAIDI MAZITO KWA TGNP MTANDAO NA UN WOMEN FUND


 Salma Sahadati Mwenyekiti wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Wanawake Zanzibar amesema Ufeminia alioupata atatumia kikamilifu na vizuri Kwa wakazi wa Zanzibar .

Lengo watu wa Zanzibar waache vitendo vya ukatili wa kijinsia Kwa watoto wakike kuwaodhesha wakiwa na umri mdogo na kutokuwepo na mimba za utotoni pamoja na wanawake kuto nyanyaswa na kutodhalilishwa Kwa vipigo na matusi.

Amesema TGNP MTANDAO na UN WOMEN FUND wasikate tamaa katika kupigania Haki za binadam pia ametoa wito kwa watu wenye Ulemavu kuchangamkia fursa mbalimbali.

Habari picha na Ally Thabiti

TERESIA BELEGE ATOA NENO KWA TGNP MTANDAO NA UN WOMEN FUND


 Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na  Maarifa Kituo cha Mkanbarani Morogoro Vijijini Teresia Belege Amewapongeza na kuwashukuru TGNP MTANDAO NA UN WOMEN FUND Kwa  kazi nzuri ya utoaji elimu ya namna ya kupinga ukatili wa kijinsia .

Teresia Belege ameahidi kuwa atatoa elimu Kwa wakazi wa Morogoro kuusu Ufeminia na yeye atakuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya watu kuondokana na ukatili wa kijinsia.

Habari picha na Ally Thabiti

DOTO YOTHAM AIPONGENZA TGNP MTANDAO NA UN WOMEN FUND


 Mwana harakati pia ni Mwalimu Kitaaluma Doto Yotham amesema Mafunzo aliopewa na TGNP MTANDAO NA UN WOMEN FUND ya Ufeminia yamemjenga na yamempa chachu ya kupambana na maswala ya Ukatili wa kijinsia.

Ametoa wito kwa Wananchi wa Kigoma kuwa kupokee elimu na Mafunzo watakayoyatoa ya Ufeminia ili waweze kuondokana na Mira na deatuli kandamizi na potofu za kuwakandamiza na kuwa nyonya watoto wa kike na wanawake mkoani Kigoma .

Habari picha na Ally Thabiti

Wednesday 13 October 2021

MKURUGENZI WA BRIGHT JAMII INITATIVE ASEMA UKATILI WA MITANDAONI INATOSHA


 Areni Fugara ni Mkurugenzi wa BRIGHT JAMII INITATIVE ameitaka jamii iache na ipoge Vita ukatili dhidi ya watoto wa kike unaofanyika kwenye mitandao ya kijamii, pia amewataka wasichana waache kupiga picha za utupu na Kusambaza katika mitandao ya kijamii.

Kwani wajidhalilisha na watajikosesha fursa mbalimbali.

Habari picha na Victoria Stanslaus

SEBASTIANI AIASA JAMII


 Sebastian Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ameitaka jamii kuto tumia vibaya mitandao ya kijamii kwani unafanyika uzalishaji mkubwa Kwa watoto wa kike ivyo ni vyema jamii ibadilike .

Habari picha na Ally Thabiti

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI ATETA NA MKUU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE


 Kama Inavyoonekana Pichani Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya KIGAMBONI Fatima Almasi Nyangasa wakiweka mikakati na Mipango ya kukiboresha chuo hiki na kuendeleza makongamano ya kumuenzi na kunikumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .

Lengo kutoa elimu Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Habari picha na Ally Thabiti

DR PHILLP DANINGA ATOA SIRI YA KUFANA KWENYE KONGAMANO LA MWALIMU NYERERE


 Dr Phillp Daninga Mkuu wa Uongozi na Utawara wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu  nyerere amesema Lengo la kuwepo Kwa kongamano la mwalimu nyerere nikuenzi pamoja nakutoa elimu Kwa jamii namna ya kudumisha umoja,Amani na kupiga Vita ukabira,udini na ubaguzi wa Aina zote.

Kwani mwalimu nyerere alipiga Vita mambo haya pia Kwa upande wa Viongozi waepuke maswala ya rushwa,urasimu,ufisadi,utovu wa nidhamu na wawajali Wananchi. Dr Daninga amewashukuru washiriki wote pamoja na watoa mada.

Habari picha na Ally Thabiti

Monday 11 October 2021

TCU YAFUNGUWA DILISHA LA MWISHO LA UDAHILI


 Prof Charles D.Kihampa  Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania  amesema Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU  inapenda kuwafahamisha Umma na Wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa Udahili katika awamu zote  tatu Kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika taasisi za elimu ya Juu nchini Kwa mwaka wa masomo2021/2022 umekamilika Kwa mujibu wa ratiba ya Udahili iliyoidhinishwa na Tume. 

Kufunguliwa Kwa Awamu ya Nne ya Udahili  Baada ya kukamilika Kwa Awamu zote tatu za Udahili,Tume imepokea maombi ya kuongeza muda WA Udahili kutokana na sababu mbalimbali .

Pia Time imepokea maombi ya kuongeza muda WA udahilikutoka Kwa baadhi ya taasisi za elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika  baadhi ya programs za Masoko Kwa mwaka 2021/2022.

Ili kutoa fursa Kwa waimbaji ambao hawakuweza kudahiliwa au kuweza kuomba Udahili katika awamu tatu  zilizopita  kutokana na sababu mbalimbali , Tume umeongeza muda wa Udahili Kwa kufunguka Awamu ya Nne na ya mwisho ya Udahili inayoanza Leo tarehe 11 Oktoba Hadi 15 Oktoba 2021/2022. Tume inawaasa waimbaji wote watumie fursa hii vizuri ili kupata nafasi ya Udahili.

Tume imetoa Rai Kwa waimbaji wa Udahili na Vyuo kuzingatia utaratibu wa Udahili katika awamu ya Nne .

Habari picha na Ally Thabiti

WIZARA YA AFYA YAITAKA JAMII KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO


 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Jinsia,Wazee na Watoto anawataka watu kutotomeza  maswala ya ukatili wa kijinai Kwa wanawake na Watoto .pia watu waondokane na Mira na deatuli kandamizi dhidi ya wanawake na watoto, ametoa wito kwa watoto na watu wengine kupiga simu ya blue 116 pindi wanapoona ukatili Kwa watoto.

Habari picha na Victoria Stanslaus

STUDIO 19 YATANGAZA FURSA KWA WASICHANA

Sama Jahanpour Mkurugenzi wa STUDIO19 anawataka Wasichana wajifunze maswala ya Mtandaoni pia watu wasitumie mitandao ya kijamii vibaya . 

Habari picha na Ally Thabiti

 

PICHANI WAFANYAKAZI WA NSSF WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA

Watumishi wa NSSF Kuadhimisha Siku ya huduma Kwa wateja makao makuu ya NSSF  jijini Dsm .

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

NSSF YAJA KIVINGINE


 Mkurugenzi wa NSSF Masha  Mshomba amewataka wanachama wa NSSF waendeleekuutumia Mfuko huu wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwani watanufaika na kufaidika Kwa kiasi kikubwa . 

Kwa sasa NSSF imejikita na kujidhatiti katika matumizi ya kiteknolojia Lengo kufanya KAZI zao Kwa urasi na Kasi zaidi, Masha Mshomba amesema katika matumizi ya teknolojia wamefika asilimia 50.

Amewataka watumishi wa NSSF na Wanachama wao kuzingatia matumizi ya teknolojia.amesema haya siku ya huduma Kwa wateja  makao makuu jijini Dsm eneo la posta ..

Habari picha na Victoria and

Friday 8 October 2021

MKURUGENZI WA ATOGS AWAPA UJASILI WATU WENYE ULEMAVU


 Eriki Mkurugenzi wa ATOGS anawataka Watu Wenye Ulemavu mbalimbali waitumie ATOGS ili waweze kujikwamuwa kiuchumi kwani kuna miradi ya Aina nyingi.

Habari picha na Ally Thabiti

MWENYEKITI WA ATOGS AFUNGUA MILANGO KWA VIJANA


 Mwenyekiti wa ATOGS amewataka Vijana wa Kitanzania kuchangamkia fursa ya Mafuta na Gesi .

 Habari na Ally Thabit

Thursday 7 October 2021

WAKATORIKI WAJA NA MSIMAMO MKALI WA CHANJO YA UVIKO 19


 Mratibu wa Huduma za Wakatoriki  za Kijamii Dr Antoni amewataka Wakatoriki wote nchini Tanzania wajitokeze Kwa wingi katika kuchanja Chanjo ya UVIKO 19 .

Pia ametoa wito kwa watu kuchanja Chanjo ya UVIKO 19 kwaajili ya Afya zao. Dr Antoni amesema nyenzo walizopewa Leo watazitumia kupitia makanisa Yao kwaajili ya kuamasisha watu wachanje Chanjo ya UVIKO 19 pamoja na kujilinda na kujikinga.

Habari picha na Victoria Stanslaus

BAKWATA YAIMIZA WATU KUCHANJA


 Katibu wa Vijana BAKWATA Taifa Othuman Zubari amewataka watu kukubali kuchanja ya UVIKO 19 kwani wataepuka kupata maambukizi ya Virusi vya UVIKO 19.

Pia BAKWATA wanaishukuru na kuipongeza serikali Kwa kuwapa nyezo za kutolea elimu ya UVIKO 19 kwenye misikiti yote Tanzania . Ametoa wito USAID,CSSC,PS ,WHO na mashirika mengine ya kiserikali na yasio ya kiserikali.

Habari picha na Victoria Stanslaus

Wednesday 6 October 2021

MTANGAZAJI NGULI WA MICHEZO MAURIDI KITENGE ABAINI MIHAROBAINI WA MICHEZO


 Mauridi Kitenge Mtangazaji wa Michezo amesema ili Michezo iweze kukuwa ni vyema watu wajitokeze katika kuwekeza kwani anaipongeza TFF na Bodi ya Rigi Kwa kuingia mkataba wa Fedha za Kitanzania bilioni 2.5 kupitia Bank ya NBC kwani Fedha hizi zitasaidia virabu vya rigi kuu soka tanzania bara katika kujikimu.

Habari picha na Ally Thabiti

LHRC YATOA MAPENDEKEZO MFUMO WA HAKIJINAI


 Furugensi Masawe Mkurugenzi wa Ujengezi na Mabolesho wa LHRC amesema Lengo la kufanya utafiti wa Mfumo wa HakiJinai nikuweza kuishawishi na kuishauri serikali ifanye mabadiliko ya sheria,Sera,kanuni na Taratibu za makosa ya Jinai katika upande wa Zamana . 

Kwani kuna ukiukwaji mkubwa wa Ibara ya 13 na 15 ya Katiba ya Tanzania Kwa watu kunyimwa Zamana kwenye upande wa jinai . Kwani zaidi ya asilimia 60 watu wapo maabusu ambako uhasirika kisaikolojia,kiafya,kielimu na kiuchumi .

Habari picha na Ally Thabiti

RAISI WA TFF AWASHUURIKIA WAAMUZI


 Raisi wa TFF amesema Wameweka Mikakati ya Kubolesha Maslai ya Waamuzi nchini Tanzania pia ameitaka Bodi ya Rigi izingatie maswala ya Utaawara Bora.

Habari picha na Ally Thabiti

Tuesday 5 October 2021

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA AWEKA MSIMAMO MKALI


 Amoni Mpanju Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria amesema Tanzania aitokubali kupitisha Sheri ya Ushoga na itakubali sheria zinazofuata Utu,Utamaduni na Mira za Kitanzania.

Amesema THRDC imeweka mikakati mizuri ya kukusabya maoni ivyo serikali inawaunga mkono .

Habari picha na Victoria Stanslaus

THRDC YAKUTANA NA ASASI ZA KIRAIA

Mkurugenzi wa THRDC Onesmo Olengulumo amesema Lengo la kukutana na Asasi za Kiraia kukusabya maoni na michango kuusu haki za binadam ambako tarehe 5 mwezi 11 /2021 yataenda kujadiliwa kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa.

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

PINGO'S FORUM YALAANI VIKALI UNYANG'AJI WA ARDHI


 Elie Chansa Afisa Habari wa PINGO'S FORUM amesema Waanzabe na jamii nyingine aipendezwi na kitendo cha serikali kuwafukuzaaeneo wanayoishi . Mfano eneo la Colima vitatu Wilaya ya Habari Mkoa wa Manyara serikali imewapoko ya Ardhi Waanzabe .

Wanaipongeza THRDC Kwa kuwasimamia na kuwatetea mpaka wameshinda keai hiyo richa ya serikali Kigoma kutekeleza amli ya mahakama.

HAbari picha na Victoria Stanslaus

MTANDAO WA WAFUGAJI WATAKA WATAMBULIKE

Mkurugenzi wa Mtandao wa Wafugaji Tanzania (TPCF) Joseph Oleparsambei ameitaka serikali iweke sheria na Sera za kuwatambua Wafugaji ili waepukane na adha ya kufukuzwa na mifugo Yao.

Pia no vyema serikali iwajengee shule,hosptali na Masoko kwani  Wafugaji Wana Haki Kama watu wengine . Mkurugenzi wa TPCF ameipongeza na kuishukuru THRDC Kwa namna wanavyotetea na kupigania Haki za binadam nchini Tanzania.

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

WATU WENYE ULEMAVU WAPONGEZA THRDC


 Musa Kabimba Katibu Mkuu wa Watu Wenye Ualbino ameipongeza jitihada na juhudi zinazofanywa na THRDC katika kutetea na kupigania Haki za binadam.  pia maswala ya watu wenye Ulemavu yanapewa kipaumbele .

Mfano kwenye taasisi za kiserikali wapo wawakilishi wa Watu wenye Ulemavu.

Habari picha na Victoria Stanslaus

Monday 4 October 2021

LHRC YABAINI MAZITO


 Jeradi wa LHRC amesema Utafiti waliofanya kwenye nchi ya Uganda,Kenya,Marawi,Zambia na Zanzibar wamebaini kuwa makosa ya Haki jinai kwenye nchi izi Yana Zamana .

Ivyo wanaitaka serikali ya Tanzania kufanya mabadiliko ya mfumo WA kisheria upande wa kijinai.

Habari picha na Victoria Stanslaus

LHRC YALIA NA HAKI YA ZAMANA


 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC Sofia Komba amesema wameamuwa kufanya utafiti kuusu Haki ya Zamana kwani Ibara ya 13 na 15 inavunjwa Kwa kiasi kikubwa Tanzania.

Ivyo ripoti iliyozinduliwa Leo utaleta mabadiliko ya Haki jinai upande Zamana.

Habari picha na Victoria Stanslaus

GAMBIA YAIPIGA TAFU BAKWATA


 Raisi Chuo cha Kiislam cha Kimataifa amesema wameingia MOU na BAKWATA Lengo kuimarisha na kuboresha mfumo WA utoaji elimu Kwa njia ya masafa Kwa nchi ya Tanzania na Gambia .

Habari picha na Ally Thabiti

SHEE WA MKOA WA DSM ATOA NENO KWA VIONGOZI WA BAKWATAI


 Shee wa Mkoa wa Dsm Ali Aji Mussa Salum amewataka Viongozi wote wa BAKWATA  wajiunge na kusoma elimu ya masafa na waweze kuelimika na kujifunza . Pia amekishukuru nchi ya Gambia Kwa kuingia MOU na BAKWATA  kwani kutaimalisha utoaji elimu Bora.

Habari picha na Ally Thabiti

MUFTI MKUU WA BAKWATA AFUNGUA MILANGO

 

Abubakari Bin Zuberi Mufti Mkuu wa Tanzania amewataka watu ,taasisi na nchi mbalimbali kujitokeza Kwa wingi kuwekeza Fedha zao ndani ya BAKWATA  Kwa upande WA utoaji elimu Mtandaoni kwani BAKWATA inaitaji kuungwa mkono Kwa Malina pesa ili Mafunzo na elimu inayotolewa iwe endelevu .

Pia BAKWATA wameipongeza nchi ya Gambia Kwa kuingia M .O.U. 

Habari picha na Ally Thabiti


BAKWATA YAPATA MAFANIKIO


 Katibu wa BAKWATA  Jamali amesema wanajivunia kuingia makubaliano na nchi ya Gambia kwaajili ya Mafunzo kwanjia ya mtandao kwani Viongozi wengi wa BAKWATA  watazidi kupata Mafunzo Bora na mazuri.

Habari picha na Ally

Friday 1 October 2021

TAURA YAPAZA SAUTI AJALI ZA BARABARANI


 Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria  Wanawake Kwa niaba ya Asasi za Kiraia wamependekeza kuwepo na mabadiliko ya Sheria ya barabarani Lengo kupunguza Kama sio kuondoa Ajali za barabarani nchini Tanzania .

Pia mambo sita yazingatiwe ikiwemo matumizi ya kuvaa mkanda, matumizi ya kofia ngumu ,watu waache kutumia simu wa wanapokuwa wanaendesha vyombo vya Moto na mengineyo. 

Habari picha Victoria Stanslaus

KISUVITA CHATOA ZAWADI KWA SUMA JKT

Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Maj Jenelali Rajabu Nduku  Mabele pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenelali  ASolomon  Lyanga Shausi, ameipongeza Wizara ya habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Kwa juhudi wanazofanya katika kuhakikisha  Sanaa inazidi kutanuka nchini.

Pia Amewapongeza kikundi  cha Sanaa na Utamaduni Kwa Viziwi Tanzania KISUVITA   Kwa kuanzisha Mashindano ya Mr na Miss Viziwi.

Amekishukuru Kikundi cha KISUVITA  Kwa kuona umuhimu wa kutoa zawadi Kwa SUMAJKT ikiwa ni shukurani Kwa kuwadhamini katika Shughuli  Yao muhimu ya Mashindano ya Mr na Miss Deaf Africa 2021 ,Kwa niaba ya ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  na Afisa Mtendaji Mkuu wa  SUMAJKT Maj Jenelali  Rajabu Nduku Mabele pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenelali ASolomon Lyanga Shausi ameshukuru zawadi wameipokea wanaishukuru Sana.


KISUVITA ilipoomba SUMAJKT iwadhamini katika Mashindano haya ya Mr na Miss Deaf Africa Uongozi wa SUMAJKT uliona ni Jambo Jena kwani katika Mashindano haya ya kimataifa akishinda mtanzania itasaidia kuutangaza vivutio mbalimbaliVilivyopo nchini  

Mfano Mbuga za Wanyama Kama Serengeti na Ngorongoro na Mlima Kirimanjaro Kwa kufanya ivyo itasaidia kuongeza watalii kuja Tanzania ivyo kuwezesha kukuwa Kwa Uchumi wa nchi,ukizingatia SUMAJKT ilianzisha Kwa Lengo la kuzalisha Mali ili kusaidia serikali katika kuendesha Mafunzo ya JKT, pia kusaidia kukuza Uchumi wa nchi.

Hivyo amewashukuru Kwa ujio wao na amewataka maandalizi mema ya Mashindano haya ya Miss na Mr Deaf Africa 2021 ambako yatafanyikia kilele chake tarehe 01/10/2021..

Hbari na Ally Thabiti


 

BABU TALE AWATAKA VIKANA KUCHANGAMKIA FURSA


 Mbunge wa Morogoro Bay Tale amewataka Wanahabari vijana wanaomiliki mitandao ya kijamii wachangamkie fursa kupitia DIZZIM TV Kwa kuuza Vipindi vyao kwani watapata Fedha za kujikimu na kuondokana na umasikini .

Habari picha na Ally Thabiti

SALAM SKA ATANGAZA DONGE NONO KWA WATAZAMAJI WA DIZZIM TV


 Salam Ska amewataka watu watazame DIZZIM TV kupitia kisimbuzi cha Startimes namba 110 na dishi 201 kwani watapata zawadi za pesa na kisimbuzi cha Startimes shindano ili litafanyika ndani ya wiki 4 na zawadi hizi zitawafikia washindi popote walipo .

Habari picha na Ally Thabiti

KANALI RESPICIUS KAIZA ATOA RAI KWA WAZAZI NA WALEZI

Kanali Respicius Kaiza amewataka Wazazi na Walezi kuwapeleka watoto wenye Ulemavu wa Aina zote wapelekwe shuleni  ili wapate Elimu Ili waweze kujikwamuwa kiuchumi na waweze Kujitegemea .

Kwani watu wenye Ulemavu wanaweza na Wana uwezo mkubwa katika utendaji kazi amesema haya wakati watu wenye Uziwi walipokuwa wakiwashukuru Jkt Kwa kuwadhamini kwenye Mashindano ya Mr na Miss Viziwi.

Habari picha na Ally Thabiti

MENEJA VIPINDI WA DIZZIM TV AJAWA NA MATUMAINI


 Meneja wa Vipindi wa DIZZIM TV amesema Swala la kujiunga na Startimes kutaongeza idada ya watazamaji DIZZIM TV ivyo amewataka watu  kununuwa Kwa wingi ving'amuzi vya Startimes  na waangalie DIZZIM TV kupitia kisimbuzi cha Antena namba 110 na kisimbushi cha dishi 201.

Habari picha na Ally Thabiti

SIKIKA KUFIKIA WATU WENYE ULEMAVU


 Godfrei Kutoka Sikika amesema wanafanya tafiti kwaajili ya watu kupata taarifa za bajeti za kiserikali  .pia watu wenye Ulemavu nao wanahaki ya kupata taarifa.

Habari picha na Ally Thabiti