Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD wa Mizani amesema Kwa sasa wanafanya makongamano na semina mbalimbali Kwa wadau mbalimbali wa Usafirishaji namna ya kutumia Mizani ambako wameanza elimu Kwa Mkoa wa Dsm na Pwani na wamefurahishwa na mwitikio mkubwa wa wadau wa Usafirishaji na jinsi walivyopokea Mafunzo haya.
Mikoa mingine watakayoenda Lindi ,Mtwara,Dodoma,Singida ,Morogoro,Tanga Iringa,Mbeya Ruvuma,Katavi,Geita,Mwanza,Arusha na Mikoa mingine. Lengo la semina hizi ni kuwaongezea uwelewa na ufahamu na umuhimu wa kuzingatia Sheria,kanuni na Taratibu za Mizani.
Ametoa wito Kwa wadau wa Usafirishaji wazingatie Uzito unaotakiwa kwenye magari Yao kwaajili ya kutunza na kulinda barabara na madaraja hili yaweze kudumu Kwa muda mrefu.
Kwani wakizingatia haya tutapunguza gharama za ujenzi wa barabara na madaraja ambako Fedha hizi zitasaidia katika kutatuwa Changamoto ya Afya, Elimu,maji na maeneo mengineyo.
Japhet Kivuyo Meneja wa TANROAD amesema haya wakati wa semina na wadau wa Usafirishaji jijini Dsm.
Habari picha Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment