Thursday 21 December 2017

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI AWAFUTA MACHOZI WANA TABORA

Waziri wa ujenzi na uchukuzi Makame Mbarawa  amebariki ujenzi wa barabara kutoka Nyasa mpaka Tabora na mikoa mingine lengo kuwawezesha wanatabora waweze kusafiri kwa wakati na kusafirisha bidhaa zao

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MWENYE KITI WA TANRODI AMTOA OFU WAZIRI WA UCHUKUZI

Mwenyekiti wa tanrodi amemuaidi waziri Makame Mbarawa fedha zilizopangwa kwaajili ya barabara zitatumika kama zilivyopangiliwa

habari picha na ALLY THABITI

SUMATRA YAWAONYA VIKALI WENYE MABASI

Dkt Oscar Kikoyo katibu mtendaji ,baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini amewataka wamiliki wa mabasi kutopandisha nauli bei, kutoonyesha kanda za video za zilisizo na maadili ya kitanzania [Utupu]  wala kuubili maswala ya dini ,siasa na kutogeuza mabasi kuwa masoko na kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu .Endapo mtu atabainika kufanya hivi atatozwa faini ya shilingi laki mbili na elfu amsini[250000] ametoa wito kwa abiria kutoa taarifa kwa sumatra na kukemea vitendo ivi viovu.

habari picha na ALLY THABITI

PICHANI MAWAKIRI WAKIWA KWENYE VIWANJA VYA KARIM JEE

Habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MAWAKIRI WASALITI KUKIONA CHA MOTO

Msajili wa mahakama amesema wakiri yeyote atakayekiuka kanuni,taratibu na sheria atafutwa na hatua kali dhidi yake ziachukuliwa ikiwemo kupelekwa mahakamani


habari picha na ALLY THABITI

MAWAKIRI WABEBESHWA MZIGO MZITO

Jaji mkuu wa Tanzania amewataka mawakiri wote hapa nchini kuwa chachu ya maendeleo Lengo ili tufikie kuelekea Tanzania ya viwanda


habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTARII AKIWA NA WAITIMU

Naibu waziri wa maliasili na utarii akiwa kwenye picha ya pamoja na waitimu  pamoja na viongozi wao

WAITIMU WA CHUO CHA UTARII WATAKIWA KUWA WAZARENDO

Mkuu wa chuo cha utarii, amewataka waitimu wa chuo cha utarii wawe wazarendo,waadilifu na wenye umoja ili wawe wafanyakazi wema

habari picha na  ALLY THABITI

CHUO CHA UTARII CHATAKIWA KUWA NA MABADILIKO

Naibu waziri wa maliasili na utarii amekitaka chuo cha Taifa cha utarii kiweze kufunguwa matawi Tanzania nzima  na kifanye tafiti za kina ili kuendana na teknolojia ya kisasa

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MAWAKIRI WAFUNDWA

Wakiri nguli Pauro Benadi, amewataka mawakiri apa nchini kutojiusisha na vitendo vya rushwa wala uvunjifu wa amani na badara yake wajikite katika kutatuwa matatizo ya wananchi

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MKURUGENZI WA MRADI BINTI JITAMBUWE AAIDI MAZITO

Mkurugenzi wa mradi wa binti jitambuwe Kanky Mwaigomora, amesema atazidi kutoa elimu kwa mabinti na vijana lengo waweze kujitambuwa na kutambuwa haki zao za msingi ili waepukane na magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi kwa kukataa kutoa rushwa ya ngono na kuacha kufaya ngono zembe


habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI WANAFUNZI NA WATOTO WA MTAANI WAKIPEWA MAFUNZO

Peter Jaksoni ,pichani akiwapa mafunzo watoto wa mtaani na wanafunzi juu ya kujitambuwa  ili waweze kutimiza ndoto zao na malengo yao


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WATOTO WA MTAANI WATOA CHOZI ZITO

Victoria Samweli , ameitaka serikali na taasisi mbalimbali ziweze kutoa elimu kwa watoto wa mtaani kuusu magonjwa ya zinaa na jinsi ya kujikwamuwa kiuchumi .Lengo waweze kutatua changamoto zinazowakabili za maradhi, chakula na mavazi

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

RUSHWA YA NGONO NI KIKWAZO KWA WATOTO WA KIKE

Ana John ,  ni mwanafunzi kutoka chuo cha usafirishaji ameitaka serikali iwachukulie atuwa kali wale wote wanaoomba rushwa ya ngono kwa wanawake wanapoenda kuomba kazi kwenye ofisini

habari picha na  ALLY THABITI

ELIMU YAITAJIKA KUNUSURU WATOTO WA KIKE DHIDI YA GONJWA LA UKIMWI

Dokta  Esta Imanueli Makelema  , kutoka zahanati ya kunduchi amezitaka taasisi mbalimbali zijitaidi kutoa elimu kwa watoto wa kike juu ya kujitambuwa

habari picha na  ALLY THABITI

TANTREDE YAJIDHATITI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Mwenyekiti wa Tanrede amesema wanatoa mafunzo na elimu na kuandaa maonyesho mbalimbali ya kibiashara .Lengo kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MOJA YA MTEJA AKIPATA HUDUMA YA KIFEDHA

huyu ni kati ya wateja ambao wamenufaika na mfumo mpya wa Exim benki kwa kushirikiana na Selcom kwa kutoa fedha na kuweka fedha


habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI MFUMO WA KIFEDHA UKIZINDULIWA

Kama inavyoonekana pichani  hii ndio njia itumikayo kutoa fedha na kuweka kupitia benki ya Exim na Selcom

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI HUDUMA YA KIFEDHA IKIZINDULIWA

Pichani viongozi wa benki ya Exim na  Selcom wakizinduwa huduma raisi ya kifedha kwa masaa 24 na kukata utepe kwani ni kiashilio tosha kwa huduma hii kuanza kutumika

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

SELCOM YAJA KIVINGINE

Mkurugenzi wa mikakati ,Benjamini Mpamo kutoka selcom ameongezea kwa kusema,dhamira kuu ya selcom  ni kuwarahisishia maisha watanzania kwa njia ya teknolojia na kuakikisha huduma za kifedha zinapatikana kwa  njia rais na haraka kwa watanzania wote.katika kuhakikisha wanatimiza dhamira hii, selcom kwa kushilikiana na Exim benki wamewaletea huduma hii ya Cashpoint Atm ili kuwawezesha watanzania kutoa fedha kiuraisi kabisa  muda wote inapohitajika .huduma zingine zinapatikana kwenye Cashpoint Atm hivi karibuni ni pamoja na kununua Luku,kulipia bili ya maji[ Dawasco], kununua muda wa maongezi, kuangalia salio na kupata taarifa fupi ya miamara ya kadi kwa wateja wa Visa na Master Card. lengo kuu la Cashpoint Atm ni kuwaraisishia  wananchi huduma za kutoa fedha na kuwawezesha kutoa fedha muda wowote kwa haraka,salama na uhakika bila kuwa na wasiwasi wa kukosa huduma hii


habari picha na ALLY THABITI

BENKI YA EXIM YAJA KUTATUA HUDUMA ZA KIFEDHA

Mkurugenzi wa fedha wa benki ya Exim  Selemani  Mponda  amesema wameshirikiana na Selcom kwaajili ya kuwawezesha watanzania na wageni kupata huduma za kifedha  kwa urais na wkati na kwa muda wote kwa kuzinduwa Cashpoint Atm zilizowezesha wateja wa selcom,Exim banki , watumiaji wa mobile maney,visa na masterCard wa ndani ya nchi na wakimataifa kutoa fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi kwa masaa 24. uzinduzi huu umefanyika kwenye ofisi za Exim banki iliyopo posta jijini D ar es salaam


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

waSHIRIKI WA KONGAMANO WAKIPOKEA MAFUNZO

Washiriki wa kongamano la umeme  wakipokea mafunzo

PICHANI MUITIMU WA KONGAMANO LA UMEME AKIPEWA CHETI

Mwandisi Warda akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa kongamano la umeme

KIJANA ASIYEONA AONYESHA UWEZO WA AJABU

Ally Thabiti Mbungo  ni mwana habari asiyeona ambaye kafanya makubwa kwenye kongamano la umeme na kukabidhiwa cheti

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UMEME ATUPIA MADONGO SERIKALI

Mkurugenzi wa kampuni ya umeme ameitaka serikali  kuwatengenezea mazingira wezeshi  makampuni binafsi na umeme


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AWACHIMBA MKWARA WADAU WA UMEME

Naibu waziri wa viwanda na biashara Stera Manyanya amewataka wadau wa umeme kuwaongezea uwelewa mafundi wa umeme ili wapige atuwa

habari picha na  ALLY THABITI

MKURUGENZI WA TANTREDI AWATOA OFU MAFUNDI UMEME

Mkurugenzi wa Tantredi amewaakikishia mafundi umeme wapewa mafunzo na vitendea kazi  ili wakamilishe ndoto zao na kuisaidia serikali katika ujenzi wa viwanda

habari picha na ALLY THABITI

TANZANIA YA VIWANDA YATAKIWA KUWA NA UMEME WA UAKIKA

Mwandisi Warda ameitaka serikali kumuunga mkono kwa mafunzo anayotoa kwa mafundi umeme .lengo uwepo umeme wa uakika  ili kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda na uchumi  wa kati


habari picha  na  VICTORIA STANSLAUS

Thursday 7 December 2017

WANAFUNZI WANAOJITOLEA CHUO KIKUU DUCE WAPEWA TANO

Projestusi Kiaruzi mwendesha bodaboda kutoka temeke awapongeza wanafunzi wanaojitolea kutoka chuo kikuu duce kwa kuwafundisha kusoma na kuandika pamoja na kutambuwa haki zao za msingi. ameiomba serikali wawaunge mkono

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WANAFUNZI WA KUJITOLEA CHUOKIKUU DUCE WAJA KIVINGINE

Salumu  Rashidi amesema kujitolea ni uzarendo wao wanatimiza miaka56 ya uhurukwa kutoa elimu bule kwa secondary lengo kumuunga mkono hayati mwalimu Nyerere na kumuunga mkono rais Magufuli katika kuelekea Tanzania ya viwanda

habari picha na  ALLY THABITI

MEDIWANI RICHADI TAREMWA ATOA NENO ZITO KWA VIJANA

Mediwani Richadi Taremwa  amewataka vijana wa kitanzania  wasiache kujitolea  kwani ni uzarendo wao wanafunzi wa chuokikuu Duce wanawafundisha wanafunzi wa secondary wilaya ya Temeke bule.

habari picha na  ALLY THABITI

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU DUCE WANAOJITOLEA KUENZI UHURU WA 56 KWA VITENDO

Mratibu na mwanafunzi wa mwaka3 Duce Mididiusi Pauneli amesema wameamuwa kujitolea kufundisha masomo ya sayansi na hesabu bule katika shule za secondary wilaya ya Temeke. lengo kuazimisha miaka 56ya uhuru na kuonyesha  uzarendo. ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wote Tanzania waweze kujitolea

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

Wednesday 6 December 2017

PICHANI NI RIPOTI ILIOZINDULIWA

Hii ndio ripoti

PICHANI UZINDUZI WA RIPOTI YA IDADI YA WATU DUNIANI

Naibu waziri wa afya,jinsia watoto na wazee dokta  Faustini  Ndungulire akizinduwa ripoti ya idadi ya watu duniani

NAIBU WAZIRI WA AFYA, JINSIA WATOTO NA WAZEE AWAFUNGUA MACHO WATANZANIA JUU YA UZAZI WA MPANGO

Naibu waziri wa afya ,jinsia watoto na wazee dokta Faustini Ndungulire amewaambia watanzania kuwa  uzazi wa mpango ni bora na salama kwani unasaidia katika kupanga mipango ya nchi .pia amezitaka asasi za kiraia na kiserikali zikatoe elimu ya uzazi wa mpango kwa ngazi za kaya vijijini na mijini

habari picha na ALLY THABITI

PROFESA KUTOKA CHUO KIKUU AWATAKA WANAFUNZI VYUONI KUTUMIA UZAZI WA MPANGO

Profesa kutoka chuo kikuu mlimani amewataka wanafunzi wa vyuo kutumia njia za uzazi wa mpango kwani zitasaidia katika kuendelea na masomo

habari picha na  ALLY THABITI

WAZANZIBAR WATAKIWA KUACHANA NA MAWAZO MGANDO NA ZANA POTOFU JUU YA UZAZI WA MPANGO

Mwakilishi kutoka Zanzabar ameitaka jamii ya kizanzibar kuachana na zana potofu juu ya kutumia njia za uzazi wa mpango . kwani zina tija kiafya na kiuchumi na kwa malezi bora

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WATANZANIA WATOLEWA OFU JUU YA UZAZI WA MPANGO

Mdau wa afya ya uzazi salama amewatoa ofu watumiajiwa njia ya uzazi wa mpango kuwa azina madhara

SWALA LA IDADI YA WATU SI TATIZO

Iblahim Kalenga kutoka ofisi ya takwim na mipango amesema swala la idadi ya watu si tatizo ila watu wanatakiwa wazae kwa mpango na wakati ili waweze kuwahudumia

habari picha na  ALLY THABITI

MDAU WA AFYA YA UZAZI AISII JAMII

Mdau wa afya ya uzazi ameitaka jamii ya kitanzania kutumia njia bora za uzazi wa mpango ili kupata watoto wenye afya njema


habari picha na  ALLY THABITI

MWAKILISHI MKAZI WA UNFPIA TANZANZANIA AAIDI MEMA

Mwakilishi mkazi wa Unfpa Tanzania bi Jacqueline Mahon amesema watazidi kuimarisha maswala ya afya ya uzazi ili watu wawezekutumia njia bora za uzazi wa mpango na kupata idadi ya watu inayolizisha

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI WAADHIRI,WAITIMU NA MGENI RASMI WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA

Pichani waitimu ,waadhiri na mgeni rasmi wakiwa kwenye picha ya pamoja  kwenye maafari ya 11ya chuo kikuu ardhi


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MGENI RASMI AKIWASIRI

Aliye kuwa waziri mkuu mstaafu kwasasa mkuu wa chuo kikuu ardhi prof Devidi Prospa Msuya akiwasiri kwenye viwanja vya chuo kikuu ardhi kwaajili ya kuwatunukia vyeti waitimu




habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI WAADHIRI NA WAITIMU WA CHUO KIKUU ARDHI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO

Waadhiri na waitimu wa chuo kikuu ardhi wakiwa kwenye maandamano ya maafari ya 11 uku wakiambatana na maprofesa mbalimbali


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MUITIMU CHUO KIKUU ARDHI AITAKA JAMII YA KITANZANIA KUACHANA NA MIRA NA DESTURI POTOFU

Muitimu wa chuo kikuu ardhi  Asha Mustafa ameitaka jamii ya kitaanzania iachane na mira na desturi zilizopitwa na wakati na zisizofaa juu a mtoto wa kike kuwa ni mtu wa tu .kwani mtoto wakike anatakiwa apewe elimu


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WAITIMU WA CHUO KIKUU ARDHI WAAIDI MAZITO

Muitimu wa chuo kikuu ardhi  Mturi Hammadi  amesema elimu alioipata chuo kikuu ardhi ataitumia kwaajili ya kutatua migogoro ya ardhi iliyopo nchini Tanzania

habari picha na ALLY THABITI

PICHANI MUITIMU AKITUNUKIWA CHETI

Pichani muitimu wa chuo kikuu ardhi akitunukiwa cheti na mkuu wa chuo kikuu ardhi

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI PICHANI AKIWATUNUKIA VYETI WAITIMU

Mkuu wa chuo kikuu ardhi na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania prof Devidi Prospa Msuya akiwatunukia vyeti waitimu walioitimu chuo kikuu ardhi . kwenye maafari ya 11 kwa mwaka 2017

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

CHUO KIKUU ARDHI CHAJIVUNIA KUWA NA TAFITI ZENYE TIJA

Makamu mkuu wa chuo kikuu ardhi Evaristi Riwa  amesema kuwa wameshiriki kufanya tafiti mbalimbali hapa nchini Tanzania ambazo zimeweza kutatuwa migogoro ya ardhi . pia wameweza kushiriki kwenye upangaji  wa mipango miji na ujenzi wa reli. ameiomba serikali iweze kuwasaidia katika utengenezaji wa miundombinu ya chuo kikuu ardhi amesema aya kwenye maafari ya 11 ambayo yamefanyika chuo kikuu ardhi jijini Dar es salaam



habari picha na VICTORIA STANSLAUS

WAITIMU WA CHUO KIKUU ARDHI WATAKIWA KULETA MATOKEO CHANYA

Mwenyekiti wa bodi chuo kikuu ardhi amewataka waitimu kuleta mabadiliko katika nchi  ya Tanzania wakati wa ujenzi wa viwanda  . amesema aya kwenye maafari ya 11 yaliofanyika kwenye viwanja vya chuo kikuu ardhi jijini Dar es salaam


habari picha na  ALLY THABITI