Wednesday 29 March 2023

WAZIRI WA UJENZI AIPONGEZA TBA

Prof. Makame Mbawala amezindua nyumba yaghorofa saba eneo la magomeni kota ambayo inauwezo wakuchukua familia 16 hivyo awapongeza wakala wa majengo kwakujenga nyumba zenye ubora na zenye gharama nafuu na kuweza kuweka mfumo wa kadi kwenye milango kwani itasaidia ukusanyaji kodi kwa wadaiwa sugu nae mtendaji mkuu wa wakala wa majengo amemshukuru na kumpongeza rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miladi kwa wakati nae mwenyekiti wa kamati wa miundo mbinu kwenye bunge la Tanzania ameahidi kutoa ushirikiano kwa wakala majengo Tanzania.

Habari picha na Ally Thabith 

AIRTEL NA BENKI YA LETSHEGO KUWAJAZA MAPESA WATANZANIA


 

Tuesday 21 March 2023

Treni ya SGR kuanza safari bila abiria, LATRA kuchunguza

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema Treni ya Mwendokasi inatarajia kuanza safari kwa kipande kilichokamilika mwishoni mwa mwezi April au mwazoni mwa mwezi May mwaka huu.

Kadogosa amesema hilo Jijini Dodoma mara baada ya kuwasili kwa msafara wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake wa CCM waliotumia usafiri wa Treni ya Mkandarasi kutokea Dar es salaam hadi Dodoma ili kushuhudia mwenendo wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).

Kadogosa amesema “Hatutapandisha kwanza Abiria kuna matakwa ya kisheria ambayo tunafuata LATRA ambao wanatakiwa wafanye ukaguzi wao wakishajiridhisha kwenye mifumo tutweza kuanza, pia tuna suala la bei ambalo wanashirikisha Wananchi sehemu mbalimbali tunapofika”


TIGO , SELCOM NA MASTERCARD WAJA NA SULUHISHO LA MALIPO YA KIDIGITALI MTANDAONI NCHINI TANZANIA


Wateja wote wa Tigo Pesa nchini Tanzania, sasa wanaweza kufanya malipo mtandaoni duniani kote kwa kutumia Mastercard Virtual Card.



Dar es Salaam. Tarehe 21 Machi 2023. Tigo Tanzania, Selcom na Mastercard Inc. wametangaza ushirikiano wa kimkakati ambao utawafanya wadau hawa watatu wa sekta hiyo kuleta mapinduzi ya mfumo wa malipo ya kidijitali kwa kuwezesha malipo rahisi ya mtandaoni duniani kote kupitia huduma ya mtandaoni ya Tigo Mastercard kupitia teknoloji ya kadi kutoka Selcom. (CaaS)

Ushirikiano huu utawawezesha wateja wa Tigo Pesa kufanya miamala kwenye majukwaa ya malipo ya kimataifa na kufaidika na teknolojia ya Mastercard ambayo itawezesha fursa mpya za biashara ya kidijitali kwa wateja na wafanyabiashara, kupitia utumiaji rahisi na salama wa malipo.

Uzinduzi wa kadi ya mtandaoni utahakikisha uwezo wa Tigo kuwapa wateja wake upatikanaji wa bidhaa na huduma , wamiliki wa kadi za mkopo huku ikibadilisha mfumo wake wa pesa kwenye simu ya mkononi. Zaidi ya hayo, ushirikiano huo utaleta masuluhisho mengi ya kisasa ya malipo ya kidijitali  nchini Tanzania na kuwaunganisha wateja wa Tigo nchini Tanzania kwenye soko la kimataifa la mtandaoni katika visa vingi vya utumiaji wa malipo ya kidijitali na kutoa ufikiaji wa mtandao wa kimataifa wa wafanyabiashara wa Mastercard.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi . Angelica Pesha alisema kuwa:

“Kama kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali nchini Tanzania tuko macho kila wakati, kwa ushirikiano huo, wateja wetu sasa wataweza kukamilisha miamala ya mtandaoni inayohitaji sifa za MasterCard. , huku wakitumia fedha zao za Tigo Pesa. Pia inamaanisha kuwa huduma hii itawaruhusu wateja kulipia bidhaa na huduma kwa haraka na kwa urahisi katika soko la kimataifa, tunatumai ushirikiano huu utaboresha uzoefu wa mtumiaji na upatikanaji wa huduma nyingi za kifedha kupitia simu za mkononi”.
"Ushirikiano huu unaimarisha zaidi nafasi yetu kama mtoaji chaguo la huduma za kifedha kwa Simu ya Mkononi na tunaamini kuwa ubia huu utaongeza idadi ya miamala ya biashara ya kuvuka mipaka, hii inaonyesha kuwa Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha nchini Tanzania. kadi inaruhusu watumiaji wa Tigo kufanya malipo kwa urahisi katika kituo chochote cha ununuzi mtandaoni ambapo Mastercard inakubaliwa bila kuhitaji akaunti ya benki au kadi ya mkopo. Ili kuunda kadi pepe, wateja wanapaswa kupiga menyu ya Tigo Pesa (*150*01#) au kutumia App ya Tigo Pesa na kufuata hatua rahisi. Baada ya kadi kutengenezwa, kadi pepe iko tayari kutumika kwa malipo ya mtandaoni.” Alisema Pesha.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji alifurahishwa na ushirikiano huo muhimu, "Selcom, tunajivunia dhamira yetu isiyoyumba ya uvumbuzi na ubora katika sekta ya malipo. Tunayofuraha kuungana na washirika  kama Tigo Pesa na Mastercard kuzindua huduma hii iliyounganishwa na Akaunti ya TigoPesa. Kwa kuwekeza mara kwa mara katika miundombinu yetu na kuboresha uwepo wetu wa soko, tunalenga kutoa masuluhisho ya kisasa, yanayotegemewa ambayo yanakuza ukuaji na mafanikio kwa washirika wetu na wateja vile vile."


Naye Ngozi Megwa, Makamu wa Rais Mwandamizi, Ushirikiano wa Kidijitali EEMEA, Mastercard alisema, “Mastercard inatambua kuwa watumiaji leo wanatafuta bidhaa rahisi na salama za kifedha ambazo zinaongeza thamani zaidi katika maisha yao ya kila siku. Mbinu yetu ya ubunifu inalenga kuwezesha mageuzi ya kidijitali ya washirika wetu ili mamilioni ya wateja waweze kufurahia ufikiaji wa mfumo wa malipo wa kimataifa wa malipo na uzoefu bora wa mtumiaji. Teknolojia yetu imetayarishwa kikamilifu ili kuwawezesha washirika wetu kuzindua masuluhisho ya kibunifu na yanayofaa ambayo yataunda pendekezo dhabiti la thamani kwa wateja wetu wote. Pamoja na uhusiano wetu ulioimarika na wahusika wa sekta ya mawasiliano ya simu, ushirikiano huu na Tigo unajumuisha dhamira yetu ya kupanua zaidi chaguo la wateja na ufikiaji wa biashara ya kidijitali.”
Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kuomba kadi pepe kutoka kwenye menyu ya Tigo Pesa kwa kupiga *150*01#, kisha uchague Huduma za Kifedha (7), Chagua Kadi za Tigo Pesa (7), Chagua Tigo Pesa MasterCard (1) ili kuendelea. APP ya Tigo Pesa Chagua Huduma za Kifedha, Chagua  Kadi za Tigo Pesa, kisha Chagua Tigo Pesa MasterCard ili kuendelea. Zaidi ya hayo; Tigo Pesa itawapa wateja wake chaguo nyingi za kutengeneza kadi, ambazo ni; Kadi ya Matumizi ya Mara Moja na Uhalali ambayo ina chaguo la Siku 90. Baada ya kadi kuundwa, kadi pepe iko tayari kutumika kwa malipo ya mtandaoni

Habari picha na Ally Thabit

WAKAZI WAISHIO MBONDE LA MSIMBAZI WATOA CHOZI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 Mwenyekiti wawa kazi waishio ponde la mto msimbazi wamepeleka barua ya malalamiko kwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwani hawakubaliani na malipo waliofanyiwa kwenye nyumba zao kupitia mradi wa DMDP.

Habari kamili na Ally Thabith

DUWASA YABAINISHA MAFANIKIO YA MAJI

 Joseph Simon Mkurugenzi mkuu wa Maji Dodoma amesema kipindi cha Rais Dr. Samia Suluhu Hassani mtandao wa upatikanaji wa maji mkoani Dodoma umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Habari Kamili na Ally Thabith

LATRA MKOA WA DODOMA WAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 Ezekiel Emmanuel afisa mfawidhi Latra mkoa wa Dodoma amesema kipindi cha miaka miwili cha Dr. Samia Suluhu Hassan Dodoma imeongeza usajili wa Mabasi na Daradara

Habari kamili na Ally Thabit

Wednesday 8 March 2023

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, RC Dodoma afanya hili

 


Dkt. Kisenge awataka wafanyakazi wa JKCI kuwafundisha wataalamu wa afya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa moyo

 Dkt. Kisenge awataka wafanyakazi wa JKCI kuwafundisha wataalamu wa afya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa moyo

Na Mwandishi Maalum – Dar es Salaam

6/3/2023 Wataalamu  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kuwafundisha jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa moyo wahudumu wa afya wa hospitali mbalimbali hapa nchini ili huduma hiyo iweze kupatikana katika maeneo mengi zaidi.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema ni jukumu la Taasisi hiyo kuhakikisha ujuzi waliokuwa nao wataalamu wake wa kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo unawafikia wataalamu wengi zaidi nchini  jambo ambalo litasababisha wananchi wengi kufikiwa na huduma hiyo.

“Leo hii mtaalamu wa magonjwa ya moyo unaweza kupata tatizo la moyo ukiwa nje ya Dar es Salaam au kijini kwenu ulikozaliwa na unaweza kufa kwa kukosa huduma ya kibingwa kwa kuwa mahali ulipo haipatikani, lakini kama tutawafundisha wataalamu wenzetu jinsi ya kutoa huduma ya matibabu ya moyo na huduma hii ikapatikana katika Hospitali zote itasaidia kila mgonjwa kupata huduma kwa wakati”.

“Katika Taasisi yetu tumejipanga kila mfanyakazi kuanzia mlinzi hadi wakurugenzi ambao siyo wa kada ya afya kupewa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharura la kiafya ninaamini kwa kuwapatia mafunzo haya kutawasaidia kuokoa maisha ya watu watakaopata matatizo ya dharura ya kiafya mahali popote pale watakapokuwa”,alisema Dkt. Kisenge.

 Aidha Dkt. Kisenge aliwashukuru na kuwapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa utendaji wa kazi wanaoufanya na kuwataka kuendelea kuwahudumia watanzania wenye matatatizo ya moyo huku wakifuata mpango mkakati wa Taasisi hiyo kwa mwaka 2022/23 – 2025/26  kwa kutimiza malengo waliyojiwekea.

Dkt. Kisenge alishukuru, “Ninawashukuru wafanyakazi wa Taasisi hii kwa kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano ninawaomba tuendelee kushikamana kwa kufuata dira ya JKCI ili iwe taasisi ya Kimataifa”, .

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Taifa Dkt. Janeth Madete aliwapongeza viongozi wa baraza hilo kwa kuongoza kikao vizuri na kujadili mambo mbalimbali ya kazi za Taasisi hiyo kwa faida ya watanzania.

Dkt. Janeth alisema kuwepo kwake katika kikao hicho alijifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna wajumbe wa baraza hilo walivyojadili kwa pamoja jinsi ya kutoa huduma bora kwa wananchi wakiwemo wagonjwa.

“Nimeona hapa mmejadili maslahi ya wafanyakazi wakiwemo wa chini ambao mishahara yao ni midogo, ninaupongeza uongozi wa JKCI kwa kuangalia maslahi ya wafanyakazi wa chini kwa kufanya hivi utendaji kazi wa Taasisi hii utaenda vizuri”, alipongeza Dkt. Janeth.

Mwisho.

MENEJA TARURA MKOA WA DODOMA AELEZA MAFANIKIO YA RAISI Dr. SAMIA SULUHU HASSAN

 meneja wa TARURA mkoa wa Dodoma Mwandisi Kirembe amesema ndnai ya miaka miwiliy ya Dr. Samia Suluhu Hasan Barabara za mkoa wa Dodoma ambazo ziko chini ya TARURA ziweza kujengwa kwa kiwango cha RAMI na changarawe pia ongezeko la fedha limekuwa kubwa, mfano TOZO za barabara, mfuko wa tozo za barabra na fedha za  bajeti

MENEJA wa TARURA ametoa wito kwa watanzania kuendelea kumuunga mkono mweshimiwa Raisi nakummpa ushirikiano

habari kamili na Ally Thabith

TRA DODOMA YAPONGEZA MAFANIKIO YA RAIS SAMIA

 Meneja Msaidizi TRA mkoa wa Dodoma kipindi cha miaka miwili cha uongozi wa Raisi Dr. Samia Suluhu Hassani mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na watu wa Dodoma kulipa kodi kwa hiari yao, ongezeko la makusanyo mkoa wa dodoma, watu kujisajili TRA kwa wingi. Pia ametoa wito kwa watanzania waendelee kumuunga mkono Dr Samira Suluhu Hassan.

Habari kamili na Ally thabith

WAZIRI WA MAJI APONGEZA CHUO CHA MAJI

 Juma Aweso waziri wa maji amekipongeza chuo cha maji kwa kufanya kongamano kubwa la pili ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujadili changamoto zilizopo kwenye sector ya maji pia amempongeza Dr. Samia Suluhu Hasssani kwa kuweza kukamilisha kwa kiasi kikubwa miradi mbalimbali ya maji

habari Kamili na Ally Thabith


Saturday 4 March 2023

AFYA YA AKILI KUPEWA KIPAUMBELE

Rais wa ELECT Dr. Mery Sando amesema huu mwaka wa chama cha madaktari wanawake amesema kikubwa kuendeleza utambuzi na uchunguzi wa saratani wanamalengo ya kujenga Hospitali yao kuelimisha jamii pia wamefika mikoa saba (7) na wanamama waliopewa matibabu ni elfu 77. amesema haya kwa niaba ya mewata.

Nae ZAITUNI  Daktari wa  watoto amesema saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi. Kwanza kuelimishana na kila mtu awe macho kujikinga kwa kuchoma chanjo. Afya ya akili imeongezeka kwenye nchi asa watoto kwa ugumu wa maisha pia akinamam wakati wa kujifungua, unyanyasaji wa kijinsia unapelekea watoto kuwa na afya ya akili.

Hospitali watakayo jenga aitobagua jinsia lengo kubwa wanawake kwenye afya ya uzazi, idara ya watoto. idara mbalimbali kama sukari na mengineyo, wito kwa jamii watoto kufanyiwa unyanyasaji nyumbani mpaka nje ili kukomesha ukatili tuwalinde watoto tusimame kidete kuakikisha manyanyaso akuna. Mwanamke awaitaji mawazo mengi wakati wa ujauzito tuwapende na kuwapa moyo ili wajifungue salama 

Habari na Victoria Stanslaus 


MEWATA KUFURAHIA MAFANIKIO YA MIAKA 35

Katibu aliyemaliza muda wake BI. FURAHA amesema wana mikakati ya namna ya kupunguz magonjwa yasiyo ambukiza ususani saratani ya matiti. Pia mewata wamejikita kwenye magonjwa ya afya ya hakili, Salatani ya Mlango wa Kizazi ambao unatokana na kuwa na wapenzi wengimsongo wa mawazo kazi kuwa nyingi na mambo mengine amesema haya Daktari wa watoto kutoka mewata.

Nae pia Daktari ASHA mwenyekiti na mratibu wa afya ya hakili kwa jamii amesema lengo la kongamano jinsi ya kuunga mkono serikali kwa upande wa afya ya hakili uanzia kwenye mimba kama mewata wamefikilia kuwamasisha jamii kufunguka na wazungumze. Amesema haya bado yatapewa kipaumbele wadau wajitokeze kuisaidia serikali. Chanjo imeletwa kwa ajili yakujikinga na salatani na pia wataendelea kuelimisha jamii kuhusiana na ugonjwa huo

Habari na Victoria Stanslaus

Friday 3 March 2023

3 TECH STARTUPS EMERGE, WINNERS OF THE VODACOM DIGITAL ACCELERATOR, SEASON 2


NGUVU KAMANDO Mkurugenzi wa Digital na huduma za ziada amesema VADACOM  wakishirikiana na COSTECH wametoa mafunzi week kumi na mbili (12) sawa na miezi mitatu (3) lengo kufika kimataifa wabunifu wa kitanzania ambapo vipaumbele vyao ni elimu, afya, usafiri kilimo na kadharika. Kampuni tatu zitaendalea kupewa mafunzo zaidi lengo kuibua vipaji ili kuboresha uchumi na kuongeza chachu wamejikita kiasi milioni 200. Kilimo, elimu ususani mambo ya sayansi wenzao wamejikita kwenye mazingira. vijana wameiva na wamepikwa vizuri hivyo basi vijana waendelee kuchangamkia frusa nyengine pins zinapokuja. ametoa wito makampuni mengine waige ili fursa zipatikane kwa wingi.

Nae LUCAS kutoka smart Darasa amesema mafunzo mbalimbali yamewasaidia kukuwa kwa Taasisi zao na pia imewasaidia kuongeza timu kutoka watu sita (6) hadi kumi na mbili (12), pia amesema  kushiriki kwenye program hizi inasaidia kukua kwa taasisi zao na kuimalika zaidi.

Nae LARRY AYO kutoka Stamartlab Program meneja amesema program ilikuwa ya meezi mitatu kampuni tatu wamejitaidi Twenzao, Kilimo Bando watawezeshwa zaidi kuboresha makampuni yao.

Habari picha na

VICTORIA STANSLAUS


Thursday 2 March 2023

MAELEZO YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI YA MHE. MKUU WA MKOA WA DSM KWA NIABA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZIJUU YA TUKIO LA SHUGHULI YA KUFUNGA MRADI WA MAJARIBIO WA MPANGO WA HATUA KUMI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA SALAMA NCHINI TANZANIA

 

MAELEZO YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

YA MHE. MKUU WA MKOA WA DSM KWA NIABA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZIJUU
 YA TUKIO LA SHUGHULI YA KUFUNGA MRADI WA MAJARIBIO WA MPANGO WA 
HATUA KUMI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA SALAMA NCHINI TANZANIA

Tarehe 2 Machi, 2023

 

Habari za asubuhi kwenu nyote.

 

v Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa taasisi zilizofanikisha Mradi huu kwa Tanzania, ambazo ni:

                   i.            Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani, UK Aid, na Global Road Safety Facility ya Benki ya Dunia kwa ufadhili wa Mpango huu.

                 ii.            Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA) kwa kuwa taasisi ya Umoja wa Mataifa inayotekeleza mradi huo.

              iii.            Shirikisho la Barabara la Kimataifa (IRF) ambalo makao makuu yake yako Geneva, Uswizi kwa kuwa kiongozi wa mradi, na Mpango wa Kimataifa wa Tathmini ya Barabara (iRAP), Chama cha Barabara Duniani (PIARC) na Chama cha Barabara Tanzania (TARA) kwa kufanya kazi kama taasisi washirikakatika utekelezaji wa mradi huu hapa nchini Tanzania.

 

Pongezi zangu pia ziwaendee wadau wote kwa kuhusika kikamilifu katika mradi huu ambao umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kabisa duniani kutekeleza Mradi wa Majaribio wa Mpango wa Hatua Kumi wa Miundombinu ya Barabara Salama nchini Tanzania. Tunajisikia fahari kupata fursa hii na kwa matokeo ambayo miezi hii 30 ya kazi ya pamoja imeleta. Leo tupo kusherehekea kwa pamoja mafanikio haya ambayo utekelezaji wake utasaidia kuifanya nchi yetu kuondokana na barabara hatarishi.

 

v Ripoti ya Hali ya Kimataifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Usalama Barabarani ya mwaka 2018 inakadiria kuwa zaidi ya watu 16,000 huuawa kwenye barabara za Tanzania kila mwaka. Vifo vingi huwa ni vijana. Usalama barabarani ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri wa miaka 5-29.

Tumepewa dhamana na watanzania na hivyo tunalazimika kuchukua hatua na kubadili mwelekeo huu na Mradi wa Hatua Kumi umetupatia maarifa, ujuzi na zana za kufanya hivyo.

 

Septemba mwaka 2022tulikuwa na uzinduzi wa Programu ya Kitaifa ya Kutathmini Viwango na Usalama wa Barabara Tanzania (TanRAP) ambayo inaipatia nchi yetu jukwaa la kubadilishana na kujifunza kutoka kwa mataifa mengine, kupitisha viwango vya kimataifa vya ubora wa usalama wa barabara zetu kwa kuzipatia madaraja ya nyota 3 au zaidi kwa watumiaji wote wa barabara na kujenga uwezo na maarifa ya ndani kwa nchi yetu kwa siku zijazo.

 

Leo, shukrani pia kwa mradi huu wa Hatua Kumi, karibu Km 10,000 za barabara na miundo zimefanyiwa tathmini kupitia mbinu za iRAP ili kubaini usalama uliojengwa ndani ya barabara zote zilizopo na barabara zinazopendekezwa kuboreshwa. Tathmini hizo zimethibitisha kuwa hatua za usalama barabarani zitapunguza hatari za vifo barabarani na kuwa na faida kubwa kwenye uwekezaji.

 

v Makadirio ya gharama ya kila mwaka ya vifo na majeraha makubwa nchini Tanzania hugharimu dola za Marekani bilioni 4.1 sawa na asilimia 8.2 ya Pato la Taifa. Kwa hiyo, Ajali za barabarani zinawakilisha changamoto kubwa kwa Tanzania ambayo inahitaji mikakati na mipango ya kutosha.

Kupitia Mradi wa Hatua Kumi, wadau wengi  wamekuwa wakifanya kazi kwa muda katika kuandaa rasimu ya mapendekezo ya mkakati mahususi wa usalama wa miundombinu ya barabara na mpango kazi na ninayofuraha kushuhudia leo matunda ya kazi hiyo ambayo yataarifu hatua ya serikali tunapoandaa mkakati wa jumla wa usalama barabarani kwa nchi na tunapoandaa mipango ya uwekezaji wa barabarani. Mpango ulioandaliwa katika mfumo wa Mradi wa Hatua kumi unawasilisha mkakati wa kitaifa wa usalama wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania kwa kipindi cha 2021-2030. Mpango wa utekelezaji unalenga kutoa maendeleo, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya hatua za usalama. Kama ilivyoripotiwa katika ripoti, uwekezaji wa takriban 0.15% wa pato la Taifa (GDP) kwa mwaka hadi kufikia 2030 utakuwa umewezesha kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya watu 7,100 kwa mwaka na pia USD 26 ya faida itapatikana kwa kila USD 1 itakayowekezwa.

v Ingawa hatua nyingi zinazohitajika ili kuokoa maisha ni rahisi kitaalamu na ni rahisi kujenga, kuna vikwazo vingi vya kufikia na kudumisha matokeo ya usalama barabarani nchini Tanzania. Viwango vilivyopitwa na wakati, na miongozo ni sehemu ya vikwazo hivyo. Tunashukuru kwa juhudi ambazo zimefanywa na wengi wenu katika kuandaa rasimu ya mapendekezo ya marekebisho ya Mwongozo wa Usanifu wa Kijiometri wa Barabara Tanzania (RGDM) ili kutathmini ufaafu wake katika kushughulikia mahitaji ya usalama wa watumiaji wote wa barabara na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UNSDG) namba 3 na 4 kwa usalama wa barabara mpya na zilizopo.

 

 

v Maarifa, ujuzi na ufahamu wa uhandisi usalama barabarani bado ni mdogo kati ya wataalamu wa usafiri katika nchi yetu. Nimefurahishwa kujua kwamba shughuli za kujenga uwezo wa Mradi wa Hatua Kumi kwa ujumla zimefikia zaidi ya wataalamu 500 wa Kitanzania na kwamba sasa tunaweza kutegemea wataalamu 150 ambao kupitia kozi za Mradi wa Hatua Kumi wamethibitishwa katika Uhandisi wa Usalama Barabarani. Tathmini za iRAP, Ukadiriaji wa Nyota wa Miundo na Ukaguzi wa Usalama Barabarani.

 

Tumepanga kuweka ari na kasi sawa, kutoa mafunzo kwa watu wengi zaidi na kufanya maendeleo kwa nchi yetu na watu wetu kupitia mpango wa kitaifa wa mafunzo na ithibati kama ilivyoandaliwa na Mradi wa Hatua Kumi kufuatia mapitio ya kina ya mafunzo yaliyopo na tathmini ya mapungufu ya mafunzo.

 

 

Sasa tuendelee na kazi nzuri na tuifanye kwa pamoja Tanzania bila barabara hatarishi!

 

Ahsanteni Sana.

 

UPATIKANAJI WA GESI ASILIA KWA MATUMIZI YA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM

  


                 TAARIFA KWA UMMA

 

UPATIKANAJI WA GESI ASILIA KWA MATUMIZI YA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM

Kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuweka mfumo ya gesi asilia (CNG) kwenye magari yao ili kuweza kupunguza gharama ya uendeshaji wa magari. Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wanaweza kuokoa hadi zaidi ya asilimia 45 ya gharama ya matumizi ya mafuta.

Mpaka sasa, tunavyo vituo viwili katika mkoa wa Dar es Salaam kikiwemo cha Ubungo kinachomilikiwa kwa Ubia kati ya TPDC na PANAFRICA na kile kinachomilikiwa na Anric kilichopo Tazara. Lakini pia, Kampuni ya Dangote inamiliki kituo binafsi kilichopo Mtwara. Vituo vingi zaidi vinahitajika ili kukidhi mahitaji yaliyoongezaka kwa wingi katika muda mfupi.

Jumla ya vituo 9 vya kujaza gesi kwenye magari vinatarajiwa kujengwa na kukamilka ndani ya miezi 24 ijayo, ambapo;

  1. Vituo viwili vya kujaza gesi kwenye magari vitapatikana kabla ya mwisho wa mwaka huu. Vituo hivyo vinajengwa na kampuni ya TAQA DALBIT katika maeneo ya Uwanja wa Ndege na kituo kingine kitajengwa Sinza mkabala na barabara ya Sam Nujoma. Vituo hivi vitakuwa na karakana za kuweka mifumo ya CNG kwenye magari. Aidha, vifaa vya kujenga vituo hivi tayari vimeanza kusafirishwa kuja nchini.
  2. Kituo Kikuu (Mother Station) cha TPDC kitajengwa Mlimani City barabara ya Sam Nujoma. Kituo hiki kitakuwa na uwezo wa kujaza magari sita kwa wakati mmoja pamoja na malori sita ya kubeba CNG kupeleka kwenye vituo vidogo. Kituo mama hicho kitaweza kuongeza kasi ya uwepo wa vituo vidogo vya kujaza gesi kwenye magari. Kituo hiki pia kitakuwa na Karakana ya uwekaji wa mifumo ya gesi kwenye magari itakayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mkandarasi wa ujenzi wa kituo hiki ameshapatikana.
  3. Vituo vingine vitakavyojengwa katika kipindi cha miezi 24 ni pamoja na; kituo kitakachojengwa Bagamoyo na kampuni ya TURKY Petroleum, kituo kitakachojengwa na Kampuni ya Anric huko Mkuranga, kituo kitakachojengwa na Kampuni ya BQ katika maeneo ya Goba, na kituo kitakachojengwa na Kampuni ya DANGOTE Mkuranga. Aidha, TPDC ilikwishatoa idhini kwa makampuni jumla 20 kujenga vituo vya CNG nchini.

Foleni zinazoonekana kwa sasa katika kituo cha kujaza gesi asilia kwenye magari cha Ubungo, zimetokana na hitilafu iliyotokea katika gari linalobeba gesi (CNG tanker) kupeleka kituo cha Anric TAZARA, ambapo bomba lake la kupokelea CNG limepasuka, na linafanyiwa matengenezo na kutarajiwa kuanza huduma mwishoni mwa wiki ijayo.

Ni matumaini yetu kwamba huduma katika kituo cha Anric TAZARA itarejea na kupunguza adha inayoendelea kwa sasa, hata hivyo inatarajiwa kuwa ndani ya miezi 24 vituo vya CNG vitaenea kwa wingi hapa nchini na kuondoa changamoto zinazoonekana kwa sasa na kuwezesha wananchi wengi kunufaika na huduma hii.

 

 

Imetolewa na;

Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania

Jengo la PSSF Kambarage/ Ghorofa ya 8, Mtaa wa Jakaya Kikwete

S.L.P 1191

DODOMA.