Thursday 27 May 2021

AMOSI MAKALA KUTEMBEZA FAGIO LA CHUMA KWA OMBAOMBA

 Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala amesema zoezi la kuondoa Ombaomba litaanza mara moja kwani wanalichafua na kupoteza hadhi ya Dsm .

Uku akiwataka watu wenye Ulemavu kutokubali kutumika katika suhuri za kuombaomba .pia ametoa wito kwa asasi za kiraia kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Dsm katika kutokomeza na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Habari na Ally Thabiti  

DR AUGUSTINA ALEXANDER ABAINI MAZITO SEKTA YA MAJI

 Dr Augustina Alexander Lecturer & Head Department of Winter Resources Engineering. amesema kuwa wamefanya tafiti kuusu maswala ya Maji wameweza kubaini kwamba Wanawake na wasichana pamoja na Wazee wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kupata maji kwa kuyafuata maji ambayo yapo mbali.

Pia wamebaini kwenye tafiti zao vyanzo vyingi vya maji vinachafuliwa na kupelekea maji wanayotumia Wananchi yanakuwa si salama na kupelekea watu kupata madhara.

Ndio maana wamefanya tafiti zenye kuleta majawabu ya kunusulu na kuokoa maisha ya watumiaji maji tanzania ili wawe na Afya bora na kwawale wanaopata maji kwa umbali mrefu wapate maji kwa ukaribu.

Amesema haya kwenye wiki ya tafiti na bunifu Chuo Kikuu cha Mlimani.

Habari na Ally Thabiti 

BALOZI MSTAAFU MSEKELA AWA NA MATUMAINI YA TAFITI NA BUNIFU

 Balozi Mstaafu Dkt  Msekela  amesema tafiti na bunifu zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Mlimani zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo ambayo jamii ya Kitanzania wanayokabiliana nayo.

Ivyo tafiti hizi na bunifu hizi zitaleta mageuzi ya  kitechnolojia  katika kukuwa kwa sekta mbalimbali na kupelekea kukuwa kwa Uchumi wetu.

Serikali na wadau mbalimbali waendelee kutoa michango kwaajili ya kuziwezesha tafiti na bunifu hizi ziendelee kifanyika amesema haya wiki ya tafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Mlimani Dsm.

Habari na Ally Thabiti

CHANGOMA FRANCES KUKUZA UCHUMI WA BLUU KWA KISHINDO

 Muhadhiri Msaidizi na Mratibu Msaidizi wa kutoa Elimu kwa Umma na Mshauri Mkuu wa Shule ya Sayansi akuwa na technorojia Changoma  Frances amesema tafiti na bunifu wanazozifanya katika Chuo cha  Uvuvi  Kunduchi .

Lengo ni kuwasaidia wavuvi na wakulima wa bahari  kutumia  dhana bora za kisasa ili waweze kujikwamua kiuchumi amesema haya kwenye maonyesho ya wiki ya tafiti na bunifu Chuo Kikuu cha Mlimani Dsm.

Habari na Ally Thabiti

TIBA ZA KUKABILIANA NA MAGONJWA ZAPATIWA UFUMBUZI

 Josefu ni Mwanafunzi Chuo Kikuu cha Mlimani amesema wameamua kufanya utafiti na kubuni namna mtu avyopata fursa ya kuwasilisha maradhi yanayomsibu kwa daktali kwa kutumia technorojia akiwa nyumbani.

Amesema huduma hii itawafikia adi watu wa vijijini ambao ukosa huduma za Afya kwa kuwa mbali na vituo vya Afya,zahanati na hospitali .

Ametoa wito kwa serikali kuimarisha na kukuza mkongo wa taifa wa Mawasiliano amesema haya siku ya kirere ya wiki ya tafiti na ubunifu.

Habari na Ally Thabiti

MKUU WA CHUO KIKUU CHA MLIMANI CHAJA NA MAJAWABU YA VIWANDA

 Wiliam Anangise Makamu Mkuu wa Chuo cha Mlimani amesema Tafiti na Bunifu wanazozifanya kwaajili ya kuibuwa Viwanda vya tanzania viweze kukuwa kwa kasi kubwa.

Amesema Maagizo na Maelekezo aliyatoa Waziri Mkuu Majaliwa kasimu Majaliwa wakati wa Ufungizi wa wiki ya Utafiti na Ubunifu.

chuo Kikuu cha Mlimani kwa kutaka tafiti zao na bunifu zao ziweze kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili watanzania watatekeleza na kufanya kazi bila mkwamo wala vikwazo vyovyote .

Habari na Victoria Stanslaus

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TECHNOROJIA ATOA MAAGIZO MAZITO

 Ronald Akwirapo amewataka watu wanaofanya tafiti waje kutatua matatizo yanayowakabili watanzania pia majarida ya tafiti hizo yaandikwe kwa rugha rafiki ya Kiswahili na yapelekwe kwa watanzania amesema haya siku ya kirere cha wiki ya Tafiti na Ubunifu kwenye Chuo Kikuu cha Dsm.

Habari na Victoria Stanslaus

Wednesday 26 May 2021

CHUO CHA AFYA SHIRIKISHI MBEYA CHA FANYA TAFITI KABAMBE



 Dokta Binngwa wa Meno Fraviana Nyatu wa Chuo Kikuu cha Afya shirikishi Mbeya.amesema wamefanya upasuaji  kwa kina mama na tafiti hizi zimesaidia kuokoa na kusaidia kupunguza vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifunguwa .

Kuna tafiti za kutambua milipuko ya magonjwa nazo zinatumika katika kunusulu maisha ya watu.pia wamefanya tafiti za kutambua vina 7 vya binadamu .

Lengo kutambua sikoseli  hii itasaidia jamii kuondokana na dhana potofu kuwa sikoseli aitokani na Ushilikina .

Nawanafanya Tafiti za Meno Chuo Kikuu cha Afya shirikishi cha Mbeya  kinawataka wadau na serikali waunge mkono tafiti wanazo fanya amesema haya kwenye jijini Dsm

Habari picha na Victoria Stanslaus  

NMB BANK TAWI LA MLIMANI LATOA NENO KWENYE TAFITI


 Meneja wa Bank ya NMB Tawi la Chuo Kikuu Mlimani Joji Mlema amesema tafiti zinazofanywa zina tika kwa taifa na bunifu mbalimbali ivyo NMB Tawi la Chuo Kikuu Mlimani kinawataka watanzania na watafiti watumie uzi tafiti na bunifu ili watatuwe changamoto zinazowakabili kwenye jamii.

Joji Mlema amewataka wanafunzi wa Chuo Kikuu Mlimani na watu wengine watumie bank ya NMB kwa huduma mbalimbali mfano kuweka na kutoa fedha kwani ni Bank salama amesema haya kwenye kirere cha siku ya utafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Mlimani Dsm 

Habari picha na Ally Thabiti

JESHI LA POLISI USALAMA BARBARA I LAWATANGAZIA VITA MADEREVA


 Mkuu wa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Kamanda Wilbrodi Mutafungwa amewataka Madereva wanaoebdesha maroli kupelekea nchi jirani ikiwemo Kongo,burundi, rwanda ,Zambia,Kenya na nchi zinginezo waachane na vitendo vya ulevi,uvujaji wa banger,matumizi ya milungi pamoja na uzinzi kwani vitendo ivi vinapelekea na kuongezeka na kukithili ajali za Barabarani.

Ambako hivi sasa kwa mwaka 2021 ajali80 za maroli zimetokea vifo vipatavyo47  na majelui 66 ndio maana Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limeamua kutoa elimu na kuwajengea uwelewa Madereva wa Maroli kwaajili ya kudhibiti ajali.

Kamanda Mutafungwa amesema atuwa kali zitachukuliwa kwa Madereva wa Maroli watakaovunja na kukiuka sheria,kanuni na taratibu za Usalama Barabarani.

Amesema mbinu wanazo zitumia za kuwakwepa maaskali wa Barabarani wamezibaini amesema haya kwenye eneo la bandari kavu Dsm alipokutana na Madereva wa Maroli

Habari picha na Ally Thabiti you

Tuesday 25 May 2021

WAZEE WA MKOA WA DSM WAMKABIDHI MIKOBA AMOSI MAKALA

 

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dsm wamemtaka majukumu mema na kumfungulia milango ya Baraka Mkuu wa Mkoa wa Dsm.

Mwenyekiti wa Wazee Mzee Mkali amesema wapo tayari kufanya kazi na Amosi Makala na wamempokea  kama inavyoonekana pichani kishito kwake na Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala.

Habari picha Ally Thabiti

MKUU WA MKOA WA DSM AWAVALIA NJUGA WAZEE WA DSM


 Amosi Makala Mkuu wa Mkoa wa Dsm amewataka wasaidizi wake kutoa wawekea vikwazo na vipibgamizi Wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Dsm .amesema Wazee ni kundi muhimu ivyo ni vyema kudhirikiana nao kwaajili ya Maendeleo ya Dsm.

Amosi Makala Mkuu wa Mkoa wa Dsm amesema atapita kata kwa kata kwaajili ya kutatua kelo za Wananchi .pia ameaidi kukutana na Wazee wa wa Chama cha Mapinduzi CCM kila baada ya miezi 3.

Ivyo amewataka Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM wampokee na wampe uahirikiano wa kutosha.

Habari picha na Ally Thabiti

BAROZI LIUNDI AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO


 BAROZI Mstaafu wa Tanzania Mzee Liundi amewataka Vijana wa Kitanzania kuwa wazalendo,waadilifu,na wasikate tamaa. Amesema Baraza la Wazee la CCM Mkoa wa Dsm wanafuraha na matumaini na Amosi Makala ambae ni Mkoa wa Dsm kwani amelelewa na kukuwa kwenye mikono na misingi bora na Imara ya Chama cha Mapinduzi.

Pia amesema demokrasia Imara ya kupeana nafasi za uongozi ndio maana nchi yetu Amani na Umoja pamoja na mshikamano vinatawara.

Amesisitiza kwa kusema Baraza la Wazee wa CCM linamuunga mkono Rais Mama Samia Suluhu Hasani.

Habari picha na Ally Thabiti



WAZEE WA CCM WAMPA BARAKA MKUU WA MKOA WA DSM


 Mjumbe wa Baraza la Wazee la CCM Mkoa wa Dsm Mzee Ramadhani Madabida amesema watampa uahirikiano wa kutosha Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala. Pia Baraza la Wazee lina matumaini makubwa na Amosi Makala kwani ni miongozo bora,makini,madhubuti,mzalendo na mkweli.

Ivyo watu wa Dsm wategemee changamoto zinazowakabili zitatatuliwa kwa wakati . Mzee Ramadhani Madabida ametoa wito kwa Wana Dsm kumuunga mkono na kudhirikiana nae bega kwa bega Mkuu wa Mkoa wa Dsm Amosi Makala.

Habari picha na Ally Thabiti

Friday 21 May 2021

MKURUGENZI WA BABA WATOTO AIPA TANO WIZARA YA HABARI,SANAA,MICHEZO NA UTAMADUNI

Mgunga Mwa Mnyenyelwa Mkurugenzi wa taasisi ya Babawatoto amesema Wizara ya habari, sanaa, michezo na Utamaduni kongamano walilolifanya la kuifundisha jamii namna ya kuwa wazarendo,Uadilifu ,umoja na mshikamano ni jambo ziti na jema.

Ivyo Wizara owe inafanya mala kwa mala bila kukosa kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali .wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na secondary , Wana vyuo,watunga sera,walimu na watoa maamuzi mbalimbali bila kuziacha asasi mbalimbali za kiraia kama walivyofanya leo .

Mkurugenzi wa Babawatoto amesema makongamano ya namna hii yatarejesha maadili mema kwa viongozi,walimu,wanafunzi na makundi mengine pia Utu Utarejea.

Ametoa wito kwa viongozi wa Wizara kuwa makongamano kama haya yafanyike nchi nzima ususani kuanzia ngazi za mitaa ,vijiji,kata na ngazi zingine ambako uko ndiko Uzarendo ,Utu ,mmomonyoko wa maadili vitendo hivi vimekithiri kwa kiwango kikubwa.

Habari picha na Ally Thabiti

 

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,SANAA,MICHEZO NA UTAMADUNI ABAINISHA MIKAKATI KABAMBE


 Ally Posi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari,sanaa,michezo na utamaduni.amesema Lengo la kuandaa kongamano ni kutoa elimu na mafunzo kwa watanzania ili waweze kujua na kutambua istoria ,utamaduni pamoja na maswala ya Uzarendo,Uadilifu na uwajibikaji.

Ambayo yalifaywa na viongozi walio pita akiwemo Rais wa awamu ya kwanza hayati Julius Kambalage Nyerere .amesema haya jijini Dsm

Habari picha na Ally Thabiti

Thursday 20 May 2021

TASAC YAWATAKA WANAHABARI KUTUMIA UWEREDI KATIKA KAZI ZAO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) amewasii Wanahabari na Wahariri wa habari kuzingatia uweredi katika kutoa habari ili kuepuka mkanganyiko .

Pia amesema TASAC ,Wanahabari na Wahariri washirikiane katika kazi .amesema mawakala wa Forodha wanazidi kusajiliwa na Wanahabari wawewanafanya tafiti kabla ya kukosoa TASAC .

Amesema haya wakati wa kuitimisha  semina ya siku mbili ya Wanahabari na Wahariri wa habari Mkoa wa Dsm.

Habari picha na Victoria Stanslaus


 

TASAC YAISHUKIA VIKALI WANAOWACHAFUA


 Meneja wa Meli wa TASAC  amewataka watu wawe wazarendo na kazi wanazozifanya  TASAC.

Kwani TASAC imeondoa tozo 7 pia wanashirikisha wadau kwa mabadiliko yoyote ya kisheria na kikanuni ,pia wanatoa Elimu yakuongeza uwelewa wa kazi za TASAC kwa kutumia vyombo vya habari .

TASAC imefungua milango ya kukosolewa ili huduma ziwe bora na mapato yaongezeke,amesema haya kwenye semina ya Wanahabari na Wahariri Mkoa wa Dsm 

Habari picha na Victoria Stanslaus

Wednesday 19 May 2021

JULIAS MITINJE WA TASAC ATOA NENO

 Asilimia 90 ya Biashara zinasafirishwa kupitia  bahari ndio maana TASAC imeundwa kwaajili ya kuleta  ushindani sawa ,kuwalinda watumiaji wa bahari na kuimarisha ulinzi .

Pia Julias Mitinje amesema kuna bandari 3 dar es salaam,Lindi na  Tanga .

Pia kuna bandari kavu 14 pia kuna mawakala wa Meli 24 kupitia kifungu cha 12TASAC inatoa reseni amesema haya wakati akiwasilisha mada kwa Wanahabari na Wahariri Dsm 

Habari na Victoria Stanslaus

TASAC YABAINISHA BIDHAA WANAZOSIMAMIA

 Meneja wa Forodha TASAC  amesema TASAC ilianzishwa kwa sheria namba 14 ya mwaka 2017 ,amesema bidhaa wanazosimamia Madini,makinikia ,mashine za Madini ,siraha au vilipuzi,mbolea ,kemikali,sukari,gesi,mafuta ya kula na mafuta ya petroli na dizeri.

Pia wanakagua mizigo  Kutokana na kifungu cha 7A amesema haya wakati akiwasilisha mada kwa Wanahabari na Wahariri jijini Dsm.

Habari na Victoria Stanslaus


TASAC YAKUTANA NA WANAHABARI

 Mkurugenzi wa huduma za Meli Bandarini amesema TASAC imeamuwa kutoa semina kwa Wanahabari na  Wahariri. Lengo kuwajengea Uwezo wa kujua kazi zinazofanywa na TASAC .semina hii inafanyika  Dsm

Habari na  Victoria Stanslaus

Tuesday 18 May 2021

MKURUGENZI MTENDAJI WA E GOVERNMENT I AUTHORITY AWATOA OFU WADAU WA MIFUMO


 Eng Benedict Ndomba amesema watu waondoe mashaka na ofu katika Mifumo ya serikali kwani ni Mifumo mizuri ambako inawezesha watu kupata huduma zao kwa alaka na upesi.

Ingawa kuna changamoto chache EGA wanazifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi mala moka kwa kudhirikiana na wadau mbalimbali .

Ametoa rai kwa watu waendelee kutumia Mifumo hii kwa maslai mapana kwa Taifa na Wananchi amesema haya Makao Makuu ya EGA jijini Dsm alipotembelea na Waziri.

Habari picha na Ally Thabiti

  

WAZIRI WA NCHI,OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ATOA ONYO ZITO


 Mohamed O .Mchengerwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora  amewataka wale wote wanaochezea Mifumo ya serikali waache mala moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao .

Pia  taasisi za serikali ambazo zina mpango wa kujiondoa kwenye mfumo wa serikali zitakuwa zinakiuka sheria namba10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020.

Kufanya hivi kwa kujitoa kwao ni kitendo cha  kuujumu uchumi .Mohamed O Mchengerwa Ameupongeza uongozi na watumishi wa EGA kwa kutengeneza Mifumo Imara,madhubuti na yenye kuaminika .

Kwani Mifumo yao inasaidia serikali katika kudhibiti upotevu wa mapato na uvujaji wa taarifa .ametoa wito kwa taasisi za serikali na wadau wengine waendelee kutumia Mifumo ya serikali ilioandaliwa na EGA .

Nawanao taka kuanzisha Mifumo yao watoe taarifa EGA  .amesema haya Makao Makuu ya Ofisi za EGA jijini Dsm

Habari picha na Ally Thabiti

Monday 17 May 2021

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI ATOA SIRI YA RAIS SAMIA SULUHU HASANI

Wiliam Olenasha Naibu Waziri wa Uwekezaji amesema rais Samia Suluhu Hasani anataka uwazi   na kutocheleweshwa kwa vibari vya wawawekezaji nchini tanzania .ndio maana .

Wizara ya Uwekezaji inaweka mazingira rafiki na wezeshi kwa yeyote atakae taka kuwekeza tanzania .amewataka wafanyabiashara waqe na umoja na wasitoe taarifa za  uongo ,na watumishi wa TIC wasiwe qarasimu kwa wataotaka kuwekeza nchini tanzania.

William Olenasha amesema Lengo la rais Samia Suluhu Hasani kuongeza kasi ya Uwekezaji ili akira zipatikane kwa wingi,kipato cha mtu mmoja mmoja kiongezeke na uchumi wa tanzania ikue kwa kasi kubwa zaidi

 Ndio maana Wizara imefanya ziara kwenye Kituo cha Uwekezaji tanzania ili watambue wajibu wao na majukumu yao kwa taifa la tanzania kakika kuwavutia wawekezaji Amesema haya Makao Makuu ya Kituo cha Uwekezaji tanzania

Habari picha na Victoria Stanslaus

WAZIRI WA UWEKEZAJI ATOA SIKU 14



 Jofrey Mwambe Waziri wa Uwekezaji ametoa siku 14 kwa wawekezaji wote  ndani ya nchi  na nje ya nchi ambao walipata vikwazo walivyotaka kuwekeza nchini tanzania.

Ivyo Wizara yake ya Uwekezaji imewapa fursa ya kuandikia barua ilu waweze kitatuliwa changamoto zao ili waweze kuwekeza tanzania .

Jofrey Mwambe amewataka watumishi wa TIC kutoa omba wala kupokea rushwa,pia uchache wa watumishi wa TIC unafanyika kazi.  huku akitaka Ofisi zote za kanda za TIC zifunguliwe.

Swala la Mabadiliko ya Sera na Sheria za Uwekezaji zinafanyiwa kazi Waziri wa Uwekezaji Jofrey Mwambe amesema haya alipotembea Makao Makuu ya Kituo cha Uwekezaji TIC jijini Dsm.

Habari picha na Victoria Stanslaus

Wednesday 12 May 2021

TWCC YATEMA CHECHE KWA RAIS SAMIA SULUHU HASANI

 Chama cha wafanya Biashara Wanawake tanzania (TWCC)imedhamilia kufanya kazi na serikali ya Mhe Samia kwa kuhakikisha Wanawake wanashiriki kikamilifu katika fursa za kibiashara na uwekezaji.

Bi Mercy Sila amesema mchango wa wawekezaji ni mkubwa ,kwani Viwanda vyao hununua mali ghafi kutoka kwa wazalishaji wa ndani  wakiwemo Wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 60 kwenye sekta ya kilimo. 

Mhe raisameahinisha vipaumbele vya maboresho katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,nishati,maji,Madini na ujenzi . Zaidi ya asilimia 54 ya wafanya Biashara tanzania ni Wanawake.

Pia mwenyekiti wa TWCC bi Mercy Sila pamoja na bodiyake wamempongeza mhe rais kwa ziara alioifanya nchi jirani ya Kenya ni ziara ambayo imeleta matumaini mapya katika kuboresha uhuaiano wa nchi mbili hasa katika kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuri zao bila vikwazo vyovyote katika jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Tanzania ina mipango Mungu na nchi ya Kenya na zaidi ya asilimia 75 ya Biashara  za mipaka zinafanywa na Wanawake.

Wanawake hawa wafanya Biashara ndogondogo na hasa kukuza mazao yao nchi jirani ambayo ni Kenya ni nchi mojawapo . hivyo TWCc wamefarijika kuona hatua alipichukua rais Samia kuhakikisha  nchi yetu unajuwa na Mausiano  mazuri na nchi jirani  kwa ustawi wa uahirikiano pamoja na Maendeleo ya jumuiya yetu.

Bi Mercy ameahidi uahirikiano kipindi chote cha serikali ya rais SAMIA. 

Habari na Ally Thabiti 



 

AREX KAPIGA AISHUKURU HAKI ELIMU

Mfanya kazi wa Clouds Arex Kapiga Ameipongeza HAKI ELIMU kwa kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sera na sheria kwenye sekta ya Elimu .

Ameitaka serikali kuyapokea na kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa .

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

HAKI ELIMU YAJA NA MAONI


 Mmoja ya wajumbe wa HAKI ELIMU wanaitaka serikali ifanye mabadiliko ya sera na sheria kwenye sekta ya Elimu kwani aziendani na Kasi ya mabadiliko ya sasa.

Habari picha na Victoria Stanslaus

TBS WAIPONGEZA TRADE MARK


 Mkurugenzi wa Tbs Dr Yusufu Othumani Ngenya amesema mfumo  waliouzinduwa una faida kubwa na nyingi ambako utaondoa gharama za kuangalia namna Tbs inavyoendeshwa na upatikanaji wa vibali .

Pia watapata mafunzo mbalimbali kutoka Tbs kupitia mfumo huu ivyo amewataka watu kutumia mfumo huu kwaajili ya maslai yao mapana ya kiuchumi na kimaendeleo  . 

Pia ameipongeza Trade Mark kwa ubunifu wao .

Habari picha na Victoria Stanslaus

TRADE MARK YAONYESHA MILANGO VIJANA


 Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark Imanueli Ulanga amesema wameshirikiana na Tbs katika kutengeneza proglam ambako mtu anaweza kujifunza na kupata miongozo mbalimbali ya Tbs.

Pia watakuja na mpango mkakati Kabambe kw aajili ya kuwafikia watu wenye Ulemavu

Habari picha Ally Thabiti

NANDY KUTIKISA DUNIA


 Msanii wa Kike wa Kizazi Jipya cha Bongo Freva NANDY amesema ameamuwa kuanzisha tuwa yake kuanzia  Mkoa wa Kigoma na mikoa mingine nchini tanzania .

Pia ataenda nchi ya Kenya kwenye mji wa Nairobi pamoja na Mombasa, Lengo lake kuweza kuwafikia Mashariki na kuitafuta fursa mbalimbali za kibiashara.  

 pamoja na kutoa elimu ,burudani na mafunzo kwa jamii  amesema haya jiji Dsm  kauli mbinu inasema  WATAKAA TUUU ametoa rai aungwe mkono na watu wote  .

Habari picha na Victoria Stanslaus

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATOA NENO


 Prof Kitila Mkumbo Waziri wa Viwanda na Biashara amewataka makampuni ya Kitanzania,wafanya Biashara,wenye Viwanda na wajasilia mali wadogo wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho ya sabasaba ya 45 yatakayo fanyika Dsm .

Ambako watapata fursa mbalimbali kukuza bidhaa zao ,kutangaza bidhaa zao na kutambulika kitaifa na kimataifa .

Pia wataweza kubadilishana ujuzi na uzoefu kwenye Biashara, nchi zipatazo 7 zitaahiriki kwenye maonyesho ya sabasaba ,kampuni 54 kutoka nje ya nchi nazo zitakuwepo .

Huku kampuni  Kitanzania 2801 zitaahiriki .pia kutakuwa na mikutano ya B to B amesema haya jijini Dsm  makao makuu ya NDC wakati akiongea na Wana habari.

Habari picha na Victoria Stanslaus

TANTRADE KUWAINUA WENYE ULEMAVU NA WASANII

Mkurugenzi wa Tantrade amewataka watu wenye Ulemavu wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho ya 45 ya saba saba yatakayofanyika Dsm kuanzia tarehe 28 mwezi 6  mwaka 2021 .

Lengo wake kukuza na kutangaza bidhaa zao kupitia kwenye taasisi zao ivyo watu wenye Ulemavu wa sina mbalimbali watakuwa na banda lao maalum kwaajili ya bidhaa zao .

Pia atakuwepo fundi asieona mshona nguo Abdullah Ali Nyangalio uku Wasanii mbalimbali watakuwepo kwaajili ya kuonyesha bidhaa zao pamoja na  vipaji vyao .

Kiingilio kwa mtoto sh.1000 na mkubwa 3000 fedha ya Kitanzania .

Habari picha na Victoria Stanslaus
 

JOTI APATA SHAVU

 

Msanii Joti Ameipongeza kampuni ya tangu ya  Plascon kwa kuweza kumpa fursa ya kutangaza bidhaa yao ivyo amesema ataitangaza vizuri .

Huku akiwata watanzania na wasio watanzania kuitumia rangi ya  Plascon kwani ina ubora na mvuto mkubwa

Habari picha na Victoria Stanslaus  

MWENYEKITI WA CHAMBER YA WACHIMBA MADINI TANZANIA ATOA MBINU NZITO


 Firbeti Lweimamu Mwenyekiti wa Chamber ya wachimba Madini amesema ili tuweze kufanikiwa na kupinga hatua kwenye sekta ya Madini  ni vyema serikali ifanye mabadiliko kwenye sera ya Madini pamoja na sheria zake.

Pia kuwepo na tafiti mbalimbali na za mala kwa mala kwenye upande wa Madini swala la utitili wa kodi limekiwa kikwazo kwa wawekezaji wa Madini.

Reseni za kufanya tafiti imekuwa changamoti.

Habari picha na Ally Thabiti

WAZIRI WA MADINI AIPONGEZA CHAMBER YA MADINI

Doto Biteku Waziri wa Madini amesema anaipongeza taasisi ya Chamber ya wachimba Madini tanzania kwa kuwatafutia fursa mbalimbali za Masoko wachimba madini .

Pia Waziri ameahidi changamoto zilizo wasilishwa kwake za kisera na kisheria zinazousu maswala ya Madini Wizara itafanyia kazi.

 Changamoto ya mitaji,tafiti na maswala ya mikopo kwa wachimba madini serikali inaamini ni kikwazo kikubwa ivyo watafanyia kazi ili kuweza kutatua matatizo haya .

Ametoa wito kwa watanzania kulinda migodi yetu na amewataka wawekezaji wa  migodi kutowanyanyasa watanzania  .

Habari picha na Ally Thabiti

Saturday 8 May 2021

KAMISHNA JENERALI ATANGAZA VITA


Jeradi Kusaya  Kamishna Jenerali wa Tume ya kudhibiti na kupambana  na dawa za kulevya  amewataka watu nchini tanzania kutoa taarifa pindi wanapo baini kuinngizwa kwa dawa za kulevya nchini  tanzania .

Amesema usiku unazingatiwa  kwa watoa taarifa  Tume imejipanga kikamilifu katika kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya  amesema haya alipotoabtaarifa za kukamatwa raia wa Irani mkoani  Lindi kwenye bahari ya Indi wakiwa na kilo 859 za dawa za kulevya .

Habari picha na Victoria Stanslaus

WAKUNGA WAIASA SERIKALI

Ndugu Franci Afsa Mkunga amesema ni vyema serikali ya tanzania kurusha mfumo wa zamani  .mtu akimaliza kidato cha 4 anaenda kusomea maswala ya ukiunga kwani hii italeta amasa kubwa  ya watu kwenda kusomea tasnia hii.

Baada ya kusitisha mfumo huu idadi ya wakunga nchini imekuwa ndogo  ivyo ni vyema serikali kurejesha mfumo huu kwaajili ya kunusulu sekta hii ya ukiunga isididimie  kama sio kupoteza kabisa .

Amesema  haya kwenye kilele cha siku ya wakunga duniani ambako uazimishwa kila ifikapo target 5 kila mwezi wa 5 kila mwaka  .
Habari picha na Victoria Stanslaus

WAKUNGA WAJA NA MBINU ZA KUOKOA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

 Raisi wa Wakunga  Tanzania Teddy Mwanga ameitaka serikali kuweka mazingira wezeshi na rafiki  kwa wakunga . KWA kuwapa vifaa vya kutosha, mafunzo ya mala kwa mala ,maslai bora pamoja na kuwapa makazina marazi bora na salama .

Hiiitaleta chachi na hadhi kwa wakunga kuipenda kazi hii na kutoa  huduma kwa  moyo mmoja kwani  mama mjamzito anapoudumiwa na mkunga aliyekuwa na Elimu maisha yake na mtoto yatakuwa salama  wakati wa kujifunguwa . 

 Amesema haya siku ya wakunga ambako uazimishwa kila ifikapo target mwezi 5 kila mwaka  duniani kote.


Habari picha na Victoria Stanslaus


WSIO ONA WAAIDI MAZITO KWA LATRA CC C


 Ally Thabiti ni Kijana Asiye Ona ambae ameshiriki kwenye mafunzo ya tiketi mtandaoni  . amepongeza kwa kupata mafunzo haya kwani yamemjengea Uwezo na uelewa na mfumo wa tiketi mtandaoni .

Amesema mafunzo haya atayatumia vizuri  na kwenda kuwaelimisha na kundi la wenye Ulemavu na wasio na Ulemavu.

Habari picha na Victoria Stanslaus


MWENYEKITI WA WASIIONA AIPONGEZA LATRA CCC


 Mwenyekiti wa Chama cha wasio Ona amesema Elimu ya kiketi mtandaoni imekuja wakati muafaka  kwani mafunzo haya yatawawezesha wasioona kwa kiasi kikubwa .   Kuepuka usumbufu ,kuingia gharama wakati wa kukata tiketi,wizi wa mizito yao na kujiakikishia usalama wa safari zao .

Kipngoamewataka watu wenye Ulemavu na wasio na Ulemavu kupokea na kuitumia mfumo huu wa tiketi mtandao kwa maslai yao,serikali na wamiliki wa mabasi. 

Ameishukuru LATRA CCC kwa kuwashirikisha watu wenye Ulemavu  juu ya mfumo huu wa tiketi mtandaoni matharani kwa  kutoa elimu na vipeperushi kwa wasio Ona  .amesema haya wilaya ya Ubungo kwenye standi ya Magufuli jijini Dsm 

Habari na Victoria Stanslaus

LATRA CCC YATOA ELIMU KWA WASIO ONA

 


Katibu Mtendaji wa Baraza la LATRA  Deo Ngowi amesema wameamua kuwapa Elimu ya namna ya kukata tiketi mtandaoni  watu wenye Ulemavu wakutokuona . 

Lengo kundi hili lisiachwe nyuma Kutokana na mabadiliko ya mfumo wa kukata tiketi mtandaoni .

Pia wamewapa vipeperushi vya nukta nundu ili waendelee kujifunza zaidi na wakatoe Elimu kwa wengine. am edema haya kwenye standi ya Magufuli mbezi jijini Dsm 

Habari picha na Victoria Stanslaus