Thursday 19 July 2018

WAZIRI JAFO AIBUA MAZITO KWA WASHIKAMKIA

Waziri wa tamisemi mh Jafo Selemani Jafo  amesema chanzo cha shule ya sekondari ya Jangwani kushika nafasi ya mwisho kwenye matokeo kidato cha sita ni walimu kutotimiza majukumu yao ikiwemo kuto andika notsi kwa  wanafunzi kutofundisha kwa uweledi na wengine kwenda kufundisha shule binafsi hivyo amemuagiza mkuu wa wilaya ya ilala mama Sofia Mjema kutoa walimu hao na kuwaleta walimu wapya amesema haya alivyotembelea shule ya sekondari ya Jangwani jijini Dar es salaam
wanafunzi wa shule ya Jagwani wakimsikiliza mh Jafo

SERA YA MAADILI NDO MWAROBAINI KABAMBE KWA WATUMISHI

Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ali Hapi amesema sasa ni wakati muafaka kuanzishwa na kuwepo kwa sera ya taifa inayohusu maadili ili tupate sheria ambayo itawabana na kuhukumu viongozi na watumishi wa serikali  ambao wanakiuka misingi ya maadili kwenye kazi zao amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na tume ya maadili kwa viongozi wa umma katika ukumbi wa Anatogo jijini Dar es salaam

MAGIZO YA WAZIRI WA ELIMU ,SAYANSI NA TEKNOROJIA YA VUTA HISIA NZITO

Naibu makamu mkuu wa chuo cha SUA(utawala wa fedha) prof,  Yonika Ngaja amesema maagizo yaliotolewa na waziri wa elimu wa sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako ya vyuo vyote vifanye tafiti zenye kutatua matatizo ya jamii wamepokea na watatekeleza kwa vitendo pia vyuo ambavyo havijakidhi viwango na vigezo suala la kufutwa hatua vitachukuliwa kwa vyuo hivyo ilikupata wanafunzi bora  na elimu bora kwa lengo la kuelekea Tanzania ya viwanda lifanikiwe kwa kiasi kikubwa kuweza kupata wataalam wengi na wenye ujuzi amesema hayo wakati wakutoa neno la shukrani kwa waziri wa elimu,sayansi na teknolojia prof Joyce Ndalichako  wakatiwa kufungua maonyesho ya 13 ya vyuo vikuu ya siku nne kuanzia 18/07/2018 mpaka 20/07/2018 mnazi mmoja jijini Dar es salaam, habari picha na Ali Thabit
 

WADAU WA ASASI ZA KIRAIA, KISHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WAKISHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE SERA MPYA

Wadau mbalimbali wakutana kwenye hoteli ya Wanyama iliyoko Sinza jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kujadili sera mpya kwa asasi za kiraia kupitia kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania


ASASI ZA KIRAIA WATAKIWA KUUNGA MKONO SERA MPYA

Ismail Abdunuru Sulemani katibu mkuu wa asasi za kiraia nchini Tanzania zisizo za kiserikali amezitaka asasi zote nchini kuunga mkono jitihada na juhudi za serikali katika kubadilisha sera za asasi za kiraia kwa kushiriki katika utoaji wa maoni kwa lengo la kuondoa sera ya mwaka 2001 kwa kuleta sera mpya kwaajili ya kuendana na wakati wa sasa amesema haya kwenye mkutano ulioandaliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LHRC uliofanyika sinza mori katika Wanyama hoteli jijini Dar es salaam.habari picha na Ali Thabit

WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO WAIPATANO SIDO

viongozi wa sido sabasaba
mjasiriamali Danius akiongea
Mjasiriamali Dainus Zabron Kaindi amesema amenufaika na elimu ya usindikaji wa mbogamboga za majani kupitia sido hivyo amewataka watanzania waweze kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na sido kwakuwa fursa hizo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa watanzania katika wimbi la umasikini
mjasiriamali Lucia akiongea
Pia Lucia Cosmas amesema sido imemsaidia kwa kiasi kikubwa katika kutangaza bidhaa zake za furnituch kitaifa na kimataifa na amekiri waziwazi kuwa sido inaunga mkono adhima ya rais Magufuli kwa vitendo kuelekea Tanzania ya viwanda kwa kuwaibua na kuwainua watu wa viwanda vidogovidogo kwa kuwapa elimu,kuwatia moyo pamoja na masoko 




  wamesema hayo katika maonyesho ya 42 sabasaba Dar es salaam.                                  habari picha na Ali Thabit

SIDO YAWAFUTA MACHOZI WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO


mjasiriamali Merry akiongea na mwandishi
Mjasiriamali Merry kutoka sinza ameto shukrani zake kwa Sidokwakuweza kumtafutia masoko ya kuuza bidhaa zake za vipochi na bidhaa zingine anazotengeneza kwa shanga na ameweza kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara ya kitaifa na kimataifa ambapo kumemjengea uwezo wa kibiashara na ameweza kunufaika kwa kukuwa kwa kipato cha uchumi wake pia ametowa wito kwa wafanyabiashara na watanzania wasisite kwenda sido kwa kupata elimu ya ujasiliamari 
baadhi ya bidhaa ya mjasiriamali Merry
Rasi Jeshi Beku akiongea na mwandishi wetu
Naye Rasi Jeshi Beku amesema sido ni mkombozi wa waanzilishi wa viwanda vidogovidogo hususa ni wanyonge na waliokata tamaa hili amelidhibitisha yeye baada ya kunufaika na elimu ya kutengeneza vikoi kutoka sido ambapo hapo awali alikuwa na malengo hayo lakini hakuwa na sehemu ya kuanzia hivyo ameshukuru na kuipongeza sido kwa kumuinua kwa namna moja au nyingine





wamesema hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba Dar Es Salaam habari picha na Ali Thabiti

Monday 16 July 2018

BENKI KUU YA TANZANIA (B.O.T) YA ELEZA NAMNA YA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI TANZANIA

Mchumi mwandamizi kutoka kurugenzi ya uchumi kutoka benki kuu ya Tanzania(B.O.T) mh Lusajo Mwamkemwa amesema wao wanajukumu lakudhibiti mfumuko wa bei wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya takwimu ambapo mfumuko wa bei unaweza kudumu kwa mwezi mmoja au miezi mitatu pia amesema mdhara ya mfumuko wa bei unaathiri maendeleo ya uchumi wa taifa.
Pia wao kama benki kuu huweza kusaidia njia mbalimbali kwaajili ya kudhibiti mfumuko wa bei  kwa kutoa elimu kupita redio,televesheni,magazeti na maonyesho mbalimbali ya kitaifa kama sabasaba na nanenane, amesama hayo kwenye maonyesho ya biashara ya 42 sabasaba jijini Dar es salaam habari picha na Ally Thabit

Tuesday 10 July 2018

MKE WA RAISI MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NCHINI TANZANIA ANENA MAZITO

Mke wa raisi mstaafu wa awamu ya nne nchini Tanzania mama Salma R Kikwete ameitaka jamii ya kitanzania kutowafungia ndani na kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu na badala yake wapeleke shule iliwapate elimu waweze kujikwamua kiuchumi na wasiwe tegemezi kwenye maisha yao, ameyasema haya wakati wa kukabidhii msaada mbalimbali katika shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliopo manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wakati wakipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa ubalozi wa Kuwait nchni kwaajili ya watoto wenye ulemavu shule ya msingi ya UHURU MCHANGANYIKO msaada huo uliwasilishwa na mh Jasem Al Najem barozi wa Kuwait nchini Tanzania  ambaye anamaliza muda wake Tanzania pia ameahidi ataendeleza ushirikiano wake na nchi ya Tanzania.habari picha na Ally Thabit
Mama Salma R Kikwete akitoneno wakati akipokea msaada katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam kulia mh Jasem Al Najem balozi wa Kuwait nchini Tanzania 

MHADHILI WA CHUO CHA KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE AWEKA MAMBO HADHARANI

Dkt Fillip Daninga ambaye ni mhadhili wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu  nyerere amesema kuwa "lengo la luanzishwa kwa chuo hiki kuandaa vijana kuongoza nchi hii baada ya kupata uhuru wa Tanganyika ambapo waliweza kufundishwa na mpaka sasa wanafundisha maswala ya maadili,uadilifu,nidhamu,siasa na uchumi ili kuweza kupata viongozi bora ambapo lengo hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa"

Dkt Fillip Daninga akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya 42 ya biashara sabasaba Dar es salaam
Pia vilevile hakusita kutaja baadhi ya viongozi nguli ambao walinufaika na elimu hiyo akiwemo raisi mstaafu wa awamu ya nne mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Kaduma,Mzee Fillip Mangula,mh Nape Nauye ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama Lindi na mh Isaya Mwita ambaye ni meya wa jiji la Dar Es Salaam
Hakusita kusema jinsi chuo kinavyo wafikia jamii kwa njia ya makongamano,matangazo ya radio na televisheni, kwa machapisho mbalimbali kwa njia ya vitabu,majarida na kielectronic pia wamejipanga kutoa elimu ya ngazi ya juu masters, amesemahayo kwenye maonyesho ya biashara 42 sabasaba Dar Es Salaam.habari picha na Ally Thabit

BUNGE YAJA NA MIKAKATI MIZITO MASHULENI


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa mheshimiwa RITA KABATI amesema "kwamba wameamua kuja na mpango maluum wa kutengeneza vyoo kwa kila jimbo moja kwa lengo kuwasaidia wanafunzi wa kike na wanafunzi wenye ulemavu kutopa shida mashuleni pindi wanavyokwenda kujisaidia vyoo"
 
mhs Rita Kabati akizungumza na mwanahabari katika maonyesho ya biashara 42 sabasaba, Dar es salaam.
Pia wameamua kuwatafutia fursa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu Bi Rita Kabati amewapongeza wabunge wa Tanzania kwa kuunga mkono hoja za watu wenye ulemavu pamoja na watoto wakike ambao hupitia kwenye changamoto mashuleni amesema hayo kwenye maonyesho ya  biashara ya 42 sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar Es Salaam wilaya ya Temeke. Habari picha na Ally Thabit

Thursday 5 July 2018

WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA AWEKA HAZARANI MIKAKATI MIZITO

Wazirin wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO  amesema wamekuja na muongozo wa kuwatambuwa na kuwaweka pamoja wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri pia wameamua kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti ya mwaka huu kiasi cha zaidi ya bilioni30 kwaajili ya utafiti na ubunifu na mambo ya sayansi na teknorojia .Lengo kupata wataalam vifaa pamoja na mashine ili kufikia hazima Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati kama rais Magufuli anavyo elekeza  .Pia ametoa wito kwa tume ya sayansi na teknorojia kutumia fedha hizi kama inavyotakiwa. Pia ameipongeza tume ya sayansi na teknorojia kwa uhadilifu' uzarendo na kwa kwakufanya tafiti zenye tija kwa maslai ya Taifa na kwa kuandaa kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu


Habari picha na ALLY THABITI

WADAU WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAUNGA MKONO WABUNIFU

Wadau wa sayansi na teknorojia pichani wakionekana kuunga mkono jitiada zinazofanywa na serikali kwa kuanzisha muongozo wa kuwatambua wabunifu wadogowadogo na kuwafikia kwa ngazi ya halmashauri

habari picha na Ally thabiti

VIJANA WABUNIFU WATOA YA MOYONI KWA WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOROJIA

Mmoja ya kijana mbunifu amemuomba waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO wawawezeshe kwa hali na mali na kitaaluma ili wafikishe malengo yao ya kuwa wabunifu wa kimataifa  hamesema  aya alipotembelewa kwenye banda lake katika ukumbi wa mlimani city katika kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu baada ya kutembelewa na waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO

Habari picha na Ally Thabiti

WABUNIFU WAUNGA MKONO HAZIMA YA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Pichani mwana mama akimuelezea waziri wa elimu sayansi na teknorojia prof JOYCE NDARICHAKO namna walivyo buni mashine mbalimbali  Lengo ni kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati .amesema haya kwenye kongamano la sita la sayansi teknorojia na ubunifu  kwenye ukumbi wa mlimani city jijini dar es salaam

habari picha na  Ally Thabiti

Saturday 30 June 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUTOKATA TAMAA


Watanzania watakiwa kuto kata taama katika suala la kudai haki kwani haki ni msingi ambao kila mtanzania natakiwa kuipata hayo yamesemwa na Pili Mohammed Kuliwa msaidizi kisheria kutoa mkoa wa Lindi katika semia iliyofanyika Landmark hotel ,Ubungo jijini Dar es salaam , semina ambayo imeandaliwa kituo cha msaada wa kisheria LHRC, Semina hiyo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kisheria wasaidizi wote wa kisheria nchini.


Habari picha na ALLY THABIT

TFDA YAMSHIKILIA ALIYESAMBAZA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI KUHUSIANA NA DAWA YA PANADOL

Prince Mhina anayeshikiriwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa akiwa anezumza na waandishi wa habari katika ofisi za Mamlaka hiyo kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Agnes Sitta Kijo.
Mamlaka ya chakula na dawa imemshikilia aliyehusika na kusambaza taarifa mitandaoni Prince Mhina kuhusiana na dawa ya Panadol kutokuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Agnes Sitta Kijo amekanusha taarifa hizo za kwamba dawa ya panadol ukiimwagia maji inageuka kuwa kitambaa si zakweli, kwani dawa ya panadol ni salama kwa matumizi kama dawa nyingine.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Chakula na Dawa amesema kuwa bidhaa inayohusishwa na dawa tajwa ni kitambaa (tab towel) ambacho kimetengenezwa kwa muundo wa kidonge na juu hakuna lebo ya Panadol wala paracetamol kam inavyoelezwa na katika video inayosambazwa, na badhaa hii hutumika zaidi katika mahoteli au maeneo mengine.

Habari picha na ALLY THABIT

Thursday 28 June 2018

Mshindi wa airtel awatoa mchecheto watanzania

Venus Malima ni mshindi wa mchezo wa kubahatisha ameishukuru airtel pamoja na sportpesa kwa kuungana hivyo amewatoa hofu watanzania kuwa michezo inayoendeshwa kupitia airtel na sportpesa ni ya ukweli na uhakika hivyo amewataka watanzania wote waweze kushiriki kwani yeye mwanzo hakuamini lakini baada ya kupata zawadi ameamini,amesema haya wakati akikabidhiwa zawadi ya smartphone makao makuu ya airtel
Habari pichana Ally Thabit
                                         Airtel yadhihirisha ubora wake 
Meneja wa uhusiano wa airtel Jackson Mbando amesema airtel wameamua kuungana na sportpesa kwenye michezo ya kubashiri lengo ni watanzania waweze kuachana na kutumia makaratasi pamoja na vibanda ubiza badala yake watumie simu za kisasa zinazojulikana kama smartphone na waweze kujishindia zawadi mbalimbali pia wajikwamue kiuchumi ,na simu za smartphone zitumike katika mambo yao mbalimbali,amesema hayo wakati akiwapatia washindi wa michezo ya kubahatisha wapatao ishirini na moja kwa kuwapa zawadi za smartphone,tv na tiketi za kutazama mechi mbalimbali za ligi kuu kwenye makao makuu ya airtel
Habari picha na Ally Thabit

Kamishna wa jeshi la uokaji na zimamoto awatoa hofu watanzania 

Kamishna wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema wamejipanga vizuri katika kukabiliana na majanga ya moto kwasababu wanavifaa bora na vya kisasa vya kuzimia moto na uokoaji.

Pia amewataka wakurugenzi na wakuu wa wilaya wote nchini tanzania kuweka vifaa vya kuzimia moto kwenye mabweni na shule zote,amesema haya jijini Dare es salaam kwenye hafla ya kumpongeza mkuu wa wilaya ya kahama kwa kuweza kufanikiwa uweka vifaa vya kuzimia moto wilaya kwake

Habari picha na Ally Thabit

Wajasiriamali waipa tano airtel

Josephine Mbona Msusa anaishukuru kampuni ya simu ya airtel kwa kuweza kuwapa mafunzo ya kompyuta ambapo wao wajasiriamali itawasaidia kuuza na kusambaza bidhaa zao kwa njia ya mtandao

Amesema hayo kwenye shule ya msingi kijitonyama wakati wa ufungaji wa mafunzo haya yaliyoandaliwa na airtel yaitwayo airtel fursa
Habari picha na Ally Thabit

Tuesday 5 June 2018

KAIMU MKURUGENZI WA RASILIMALI ZA MAJI ATOA SIRI NZITO

Kaimu Bi Naomi Lupimo amesema "wameweza kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya mabonde ya maji kwasababu yakuwa na sera nzuri ya mwaka 2002 kanuni bora na sheria namba 11 ya mwaka 2009".

Bi Naomi Lupimo" wizara yake ya maji inashirikiano mzuri na wizara nyinginezo katika kutunza, kulinda,kuhifadhi na  kuboresha vyazo vya maji pamoja na mabonde ya maji dhidi ya wachafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyazo vya maji" amesema hayo katika kilele cha madhimisho siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jiji Dar es salaam.
habari picha na ALLY THABITI

SUMATRA YA ELEZA JINSI YA KUTUNZA MAZINGIRA

Salum Pazi kutoka SUMATRA amesema "wamechukua jitihada za kutuza mazingira kwakutengeneza vyoo stand za mabasi na daladala na kuweka vifaa vya kutunzia takataka ndani ya mabasi lengo abiria wasitupe takataka barabarani madirishani pia wanatoa elimu kwa abiria juu ya kutunza abiria vilevile wameahidi watazidi kuyatunza mazingira" amesema hayo kwenye maonyesho ya siku mazingira dunian katika viwanja vya mnazi mmoja jiji Dar es salaam.
  habari picha nALLY THABIT


Tuesday 22 May 2018

BANK YA DCB YA TANGAZA NEEMA NZITO.
Akielezea neema hiyo Mkurugenzi wa benki DCB (godfrei ndalwahwa),wata toa mikopo kwa masharti nafuu kwa wajasiliamali vijana na wanawake ilikuweza kujikwamua kiuchumi na kimaisha,pia amezitaka almashauri kupeleka fedha zao kwenye benki hiyo.
Amesema hayo kwenye maonyesho ya siku nne ya wajasiliamali kwenye viwanja vya manazi moja yalio andaliwa na manispaa ya ilala pia wanatoa mikopo ya nyumba.
habari picha na ALL THABITI
habari picha na ALL THABITI


BENKI YA CRDB YAJA KIVINGINE.
Afsa biashara wa tawi la vijana aitwe ZAINABU MANORO wa benki ya CRDB amesema wameamua kutoa huduma kwa wajasiliamali wakiwa na lengo la kuwawezesha kiuchumi kwa kuanzisha huduma ya FAHARI HUDUMA pamoja na mikopo kwa wajasilia mali mojamoja na vikundi na mikopo nafuu na rahisi kwa wajasiliamali wanawake, amesema hayo kwenye viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maonyesho ya ujasiliamali.

habari picha na ALL THABITI



























LETSHEGO YA WATOA HOFU WATANZANIA.

Afisa mahusiano wa LETSHEGO amewataka watanzania kujiunga na benki yao kwani umeenea kwakwakiasi kikubwa na wanatoa mikopo kwa bei nafuu nawanapatikana morroko jijini dar es salaam.
habari picha na ALL THABITI



MADIWANI WALAANI VIKALI MASHAMBULIO.

Madiwani wa manispaa ya kinondoni wamelaani vikali shambulio waliofanyiwa na mfanya biashara aliefahamika kwa jina la ALFONSI BEATA.Shambulo hilo lilitokea katika eneo la coco beach wakati kamati ya biaashara ilipo fika ilikufanya ukaguzi.
habari picha na ALL THABITI















MANISPAA YA KINONDONI YA MWAGA MABILIONI YA PESA.
Mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni BENI SITA,amesema kua kiasi cha bilioni 14 imetengwa kwaajili ya ujenzi wa eneo la coco beach wakiwa na lengo la kuwezeza kipato kuingia katika manispaa huku akiwato hofu wafamya biashara wadogo hasa watu wakipato cha chini.

habari picha na ALL THABITI





Monday 21 May 2018

Tuesday 9 January 2018

MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI AKABIDHIWA OFISI

Edwin mndolwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya  ya Wazazi Ccm ameahidi kulinda na kuzisimamia mali zote  za Jumuiya  za Wazazi ccm
Amesema hayo  kwenye makao  makuu ya Jumuiya ya Wazazi ccm Jijini Dar es salaam

Habari picha Na Ally Thabiti

KITUO CHA MSAADA WA KISHERIA CHA LAANI VIKALI ADHABU ILIYOTOLEWA NA TCRA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi mtendaji wakituo cha msaada  wa Kisheria LHRC bi Hellen Kijobisimba amesema wanalaani  vikali kitendo cha mamlka  ya  mawasiliano Tanzania kuvipiga  faini vyombo vitano vya  Habari ikiwemo Azam, star tv, channel ten, East AFrica na  ITV kwakutoa  taarifa  ya  tathmini ya  uchaguzi mdogo wa madiwani wa mwaka 2017  ambapo taarifa  hizo zilitolewa na  kituo hicho  hivyo ameitaka  TCRA kufuta adhabu hizo mara moja ambapo jumla ya Milioni Sitini zinatakiwa kulipwa na Vituo hivyo

Aidha bi Hellen ametoa wito kwa  wadau mbali mbali kuchangia  mfuko ambao utasidia kulipa faini  ambao utakuwa unasaidi vyombo vya Hbari Vinavyopigwa Faini

Habari Picha na Ally Thabiti

MAMLAKA YA MAPATO YA WATAKA WATANZANIA KULIPA KODI ZA MAJENGO

Mkurugenzi  wa huduma na  elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA  Richard Kayombo amewatatka  watanzania waanze kulipa kodi za majengo kuanzia sasa ili kuepusha  usumbufu kama uliotokea  mwaka jana,

 Amesema  hayo  wakati  wakutoa  taarifa za makusanyo na  mapato kwa mwaka 2017 kuanzia tarehe 1 mwezi 6 had mwenzi wa 12 ambapo  ni trilioni 7.87 ikilinganishwa  na sh trilioni 7.27 ambazo  zilikusanywa kipindi kama hicho katika  mwaka wa  fedha wa 2016/17  ambapo ni sawa  na  ukuaji wa asilimia 17.65

hata hivyo katika  mwezi wa Desember pekee  TRA ilikusanya jumla ya shilingi trilioni 1.66

aidha  bwana  Kayombo amewapongeza  wafanyabiashara wenye makampuni na wananchi  kwakulipa kodi  pia amewataka wananchi wadai risiti na  wafanyabiashara watoe Risit wanapouza  bidhaa zao.

Habari Picha Na Victoria Stanslaus