Thursday 28 September 2017

WANA HABARI WATAKIWA KUTEKELEZA KANUNI MPYA

Katibu mkuu kutoka wizara ya sanaa ,michezo , tamaduni  na habari amewataka wana habari wa kutii na kuzitekeleza kwa vitendo kanuni mpya za habari zitakazotumika . amesema haya jijini Dar es salaam wakati akiongea na wadau wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS




































WIZARA YA KILIMO YAJA NA MAJAWABU YA WAKULIMA

Waziri wa kilimo amesema wameamuwa kutatuwa vikwazo vinavyowakabili wakulima miongoni mwa vikwazo hivyo. ukosefu wa pembe jeo, mbegu bora, zana za kilimo,miundombinu , masoko na bei mzuri ya mazao. amesema haya kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa mwalimu Nyerere posta jijini Dar es salaam .waziri wa kilimo ametoa wito kwa wakulima kulima kilimo bora na chenye tija .  pia waziri wa kilimo  amewatoa ofu wakulima kwa kuwaambia kuwa pembe jeo zote zitauzwa kwa bei elekezi pia amekanusha uvumi ulioenea kwamba wakulima wa zao la korosho watapewa Salfa bule na si kweli

habari picha na  ALLY THABITI

Wednesday 27 September 2017

MABAHARIA WATOA KILIO CHAO SERIKALINI

Mwenyekiti wa jumuia ya mabaharia Tanzania  FRENKI CHUMA ameitaka serikali iweze kuludisha shirika la nasako lengo chombo hiki kiweze kutumika katika kuwatafutia kazi mabaharia Tanzania na nje ya nchi  . amesema haya jijini Dar es salaam walipo tembelewa na mkuu wa wilaya ya Ilala mama  SOFIA MJEMA

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

SERIKALI YATAKIWA KUWATENGENEZEA MAZINGIRA MABAHARIA

Kiongozi wa Meli kutoka jumuia ya mabaharia Tanzania  ameiomba serikali iwatengenezee mazingira wezeshi ya wao kupata ajira .Lengo waweze kujinusulu na wimbi la umasikini

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MKUU WA WILAYA YA ILALA KUWAKOMBOA MABAHARIA

Mkuu wa wilaya ya Ilala mama  SOFIA MJEMA  ameuwaakikishia uongozi wa jumuiya ya mabaharia nchini Tanzania anawatambua na atawasaidia kupata ajira mabaharia wote . pia ametoa wito kwa mabaharia wote wakajiendeleze kielimu ili waendane na soko la sasa

habari picha na  ALLY THABITI

HAPPY MAIKO AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

  Mwanafunzi aliye itimu chuo cha THE  TANZANIA INSTITUTE OF  BANKERS [TIOB] amesema elimu alioipata ataitumia vizuri ili nchi ya Tanzania iweze kufanikiwa katika kuelekea uchumi wa kati . ametoa wito kwa wasichana wasikate tamaa ya masomo

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MKURUGENZI WA CHUO CHA THE TANZANIA INSTITUTE BANKERS [ TIOB] AJA NA MBINU YA KIPEKEE

Mkurugenzi mtendaji  PETER wa chuo cha THE TANZANIA INSTITUTE BANKERS [TIOB] amesema wapo mbioni kuanzisha mfumo wa wanafunzi wao kusoma kwa kupitia mitandaoni . Lengo kuwapa nafasi wanafunzi ambao wapo makazini kwani wanafunzi wengi wanashindwa kusoma kwa kukosa muda

habari picha na  ALLY THABITI

WAITIMU WA CHUO CHA THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS[TIOB] WATAKIWA KUWA WAZARENDO

Mmoja ya viongozi mama  TUSE  amewataka waitimu wa THE TANZANIA INSTITUTE BANKERS [ TIOB] wakawe wazarendo katika utendaji wao wa kazi .Pia wafanye kazi kwa uhadirifu

habari pich na  ALLY THABITI

GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA AFUNGUWA MILANGO

Gavana wa benki kuu ya Tanzania  [BOT] BEENO NDULU  amewataka waitimu wa chuo cha  THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS [TIOB] wasisite kwenda kuomba kazi kwake na kwenye mabenki mengine . amesema haya kwenye maafari ya wanafunzi hawa Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam eneo la posta

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WANAFUNZI WA THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS[TIOB] WAKIWA KWENYE MAANDAMANO

Pichani Gavana wa benki kuu Tanzania [BOT] akiongoza maandamano ya waitimu wa chuo cha  THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS [TIOB]


habari picha na  ALLY THABITI

Tuesday 26 September 2017

WATU WENYE ULEMAVU AWAPASWI KUTENGWA

Mmoja ya viongozi kutoka chuo cha  Sekomu ameitaka jamii ya  kitanzania na isio ya kitanzania kutowatenga ,kuwanyanyapaa na kutowabaguwa watu wenye ulemavu na badala yake wawe karibu nao na wawape elimu kwa kuwapeleka mashuleni. wao chuo cha Sekomu wannatoa mafunzo ya aina mbalimbali asa kwa walimu jinsi ya kuwafundisha na kuwaudumia watu wenye ulemavu wa aina zote .chuo hiki kipo mkoani Tanga  na kinnatoa mafunzo ya nukta nundu ni maandishi ya watu wenye ulemavu wa kutokuona  wanayatumia katika kuandika na kusoma

habari picha na ALLY THABITI

WAZAZI WATAKIWA KUTUMIA MAWAKALA WAZURI WA VYUO

Kiongozi wa Universities Scholaship amewataka wazazi na walezi wakitaka kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi wawatumie wao kwani gharama zao ni nafuu na watawapeleka kwenye zenye usalama zaidi na watapata elimu mzuri

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

CHUO CHA MOROGORO CHAJIVUNIA ELIMU BORA

NGAJA MUSA amesema chuo chao cha Morogoro kinatoa elimu bora na gharama nafuu. ivyo amewataka wazazi na walezi wawapeleke vijana wao kwenye chuo chao kwa elimu yenye tija na bora zaidi

habari picha na  ALLY THABITI

WAZANZIBAR WATAKIWA KUACHANA NA MILA NA DESTURI POTOFU

Mmoja ya viongozi wa chuo cha Zanzibar amewataka wazanzibar waache kuwaozesha watoto wao wakiwa na umri mdogo kwani wanawakatishia masomo. lengo la kuamasisha waweze kukitumia chuo chao kwaajili ya kupata elimu bora

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

URASIMISHAJI WA ARDHI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI

Kamishna wa ardhi MERY GASPA MAKONDO amesema wameamua kurasimisha ardhi Lengo kuondoa migogoro ya ardhi iliopo nchini Tanzania. na kuwafanya watanzania waondokane na ujenzi olela wa nyumba zao Mpaka sasa wameweza kurasimisha ardhi manspaha ya ILEMELA  jijini Mwanza,Kinondoni na Ubungo jijini Dar es salaam. amesema haya  kwenye mkutano uliofanyika hotel ya Kilimanjaro posta

habari picha na  ALLY THABITI

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA MAENEO SI HATARISHI

Katibu tawara msaidizi anaeusika na maswala ya miundombinu kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa  Dar es salaam MAIKO OLE MUNGAYA amewataka watanzania wasijenge maeneo ambayo sio hatarishi ili wasiweze kupata madhara  mbalimbali . ususani vifo vitokanavyo na mafuriko kwa kujenga kandokando ya mito, maziwa,mabwawa, baharini na mabondeni na sehemu za majangwa

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WATANZANIA WATAKIWA KUTIMIZA KANUNI YA AFYA YA MAZINGIRA

STIVINI KIBERITI  amesema ni vyema watanzania wote waweze kutumia kikamilifu kanuni za Afya ya mazingira ili Afya zao zipate kuimarika .wakifanya ivi wataondokana na maradhi ya Moyo na magonjwa ya milipuko ametoa rai kwa watanzania waachane na matumizi mabaya ya uvutaji wa Tumbaku kiolela. amesema haya kwenye viwanja vya Mnazi mmoja wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam kwenye siku ya Afya ya mazingira Duniani

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WILAYA YA ILALA YAJA NA MIKAKATI KABAMBE

Afsa tawara kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala  JABRI OMARI MAKAME amesema wameamuwa kuja na mikakati ya kudhibiti uchafuzi wa hewa kwa kutenga eneo la kuvutia sigara lililopo viwanja vya Mnazi mmoja .pia wanatoa elimu kwa jamii jinsi gani ya kutunza mazingira .amesema haya kwenye uzinduzi wa siku ya Afya ya mazingia  ambako kauli mbiu inasema  dhibiti uchafuzi wa hewa kwa Afya ya jamii

habari picha na ALLY THABITI

RAIS WA TFF APOKEA DONGE NONO LA FEDHA

Rais wa TFF WALLACE KARIA  akipokea cheki yenye thamani ya shilingi milioni 325000000 kutoka benki ya KCB .nae mkurugenzi mtendaji wa benki ya KCB COSMAS KIMARIO akikabidhi cheki

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MAKABIDHIANO YA MKATABA

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya KCB  COSMAS KIMARIO akimkabidhi  mkataba wa  mwaka mmoja wa udhamini wenza wa Ligi kuu soka Tanzania bara  wenye thamani ya shilingi milioni 325000000 .rais wa shilikisho la mpira wa miguu WALLACE KARIA akipokea mkataba huu kwenye hotel ya Serena jijini Dar es salaam

habari picha na ALLY THABITI

RAIS WA TFF AWATOA MCHECHETO WADHAMINI

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania [TFF] WALLACE KARIA  amewataka wadhamini mbalimbali wajitokeze kwa wingi kuidhamini na kufadhili mchezo wa mpira wa miguu hapa Tanzania. Lengo kuinua na kukuza vipaji  kwa vijana wanaocheza mpira wa miguu nchini Tanzania na kuwaakikishia ajira ya kudumu na atimae itasaidia kukuwa kwa uchumi. Pia amewatoa ofu na mashaka pindi wakavyotoa fedha zao za ufadhiri na udhamini .amesema haya  wakati wa kutilia saini na benki ya KCB kwenye hotel ya Serena jijini Dar es salaam

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

Monday 25 September 2017

BENKI YA KCB YAIJAZA MAPESA TFF

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya KCB COSMAS KIMARIO  amesema wameamua kudhamini ligi kuu soka Tanzania bara kwa mwaka 2017/18 kwa kiasi cha shilingi milioni 325000000 .lengo kukuza mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini Tanzania

habari picha na ALLY THABITI

Sunday 24 September 2017

VIJANA WATAKIWA KUACHA TAMAA

SALUM amewataka vijana wa kitanzania kuachana na tamaa ya kwenda nje ya nchi kwa njia aramu kwani yeye amekumbana na maswaibu mengi baada ya kuzamia na kwenda nchini Ubirigiji. pia amewasii vijana wa kitanzania wasitumie madawa ya kulevya kwani nikishawishi kikubwa katika uvunjaji wa amani

habari picha na  ALLY THABITI

WAKIMBIZI NI KIKWAZO

Mwakilishi mkazi wa shirika la uhamiaji duniani  KASIM SUFI  amesema swala la idadi kubwa ya wakimbizi imekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi zinazowaifadhi wakimbizi. ivyo amezitaka nchi ambazo zinamapigano ya kivita ziache mala moja .pia amezitaka zilete amani na utulivu pamoja na kuzitaka zingine ziendeleze kulinda na kudumisha amani zao ikiwemo Tanzania . amesema  wao shirika la uhamiaji duniani lipo katika wakati mgumu wa kuwaandikisha wakimbizi amesema haya kwenye viwanja vya mwembe yanga wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kwenye siku ya amani ambako uhazimishwa kila mwaka tareha 23mwezi9

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

JESHI LA POLISI TANZANIA LATANGAZA VITA KALI

Kamishna wa jeshi la polisi jamii  MUSA ALLY MUSA  amesema kwaniaba ya mkuu wa jeshi la polisi Tanzania kamanda SIRO  watapambana kwa ali na mali mtu, kikundi cha watu au taasisi kitakacho subutu kuvuruga amani iliopo Tanzania  watachukuliwa atua kali za kisheria .amesema haya kwenye nviwanja nya mwembeyanga wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kwenye siku ya maazimisho ya amani ambako uhazimishw kila mwaka tarehe 23/9

habari picha na ALLY THABITI

ULEMAVU SI KIKWAZO CHA MAENDELEO

BIBI MARIAM  ameitaka jamii kuamini kuwa ulemavu sio kikwazo cha maendeleo ivyo vyema kuwatengenezea mazingira rafiki na wezeshi watu wenye ulemavu lengo wajikwamue kiuchumi

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA YAWAONYA VIKALI WANA HABARI

ABDALLAH NGARAWA  kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania [TCRA]  amesema mwana habari yeyote ambae atatoa habari za uchochezi atachukuliwa hatuwa za kisheria .pia amewataka wanahabari waandike habari zao kwa staa.amewaasa wanahabari kutokubali kutumika katika kuvuluga amani nchini Tanzania amesema haya kwenye ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam uliopo posta

habari picha na  ALLY THABITI

WANAFUNZI WAPEWA MONGOZO

Makamu mkuu wa shule ya secondary sent JOSEPH amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi waliomaliza na wasasa wa shule ya sent JOSEPH ni kuwajengea umoja ambao utakuwa wakudumu na wenye tija na masrai mapana kwa wanafunzi, shule na Taifa kwa ujumla . kwani umoja wao utakuwa wa maendeleo

habari picha na ALLY THABITI

ERICK SHIGONGO ANENA KWA UCHUNGU YALIO MOYONI MWAKE

ERICK SHIGONGO amesema vijana wa kitanzania wamekuwa wavivu na wazito katika kujifunza  maswala ya kitecnorojia na kusoma vitabu mbalimbali. ndio maana wanashindwa kujikwamuwa kiuchumi amesema haya siku ya kuwakutanisha wanafunzi wa secondary sent JOSEPH  kwenye viwanja vya KARIM JEE ametoa rai kwa wanafunzi wa sent JOSEPH na Tanzania kwa ujumla wasikate tamaa na wasibweteke

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WATANZANIA WATAKIWA KUTOWAFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU

ELIKA KISA  amesema ni vyema jamii kutowaficha ,wabagua, kuwanyanyapaa na kuto watenga watu wenye ulemavu ivyo ni vyema kuwapeleka mashuleni na kuwapa fursa mbalimbali ili waondokane na utegemezi katika maisha yao

habari picha na  ALLY THABITI

KAMPUNI YA BEACON FINANCIALS LTD YATANGAZA NEEMA

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya BEACON FINANCIALS LTD BRIAN CHUWA amewaakikishia wanafunzi waliomaliza shule ya secondary sent JOSEPH  kuwapatia ajira pia amewataka wajifunze tecnorojia ya kisasa ndipo watakapofikia malengo yao

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

SHULE YA SECONDARY SENT JOSEPH YAPEWA TANO

Moja ya viongozi kutoka nje ambaye mgeni rasmi ameupongeza uongozi wa shule ya secondary sent JOSEPH kwa kuunda na kuwatengenezea umoja wanafunzi waliomaliza .kwani wanafunzi hawa watafaidika kiuchumi na kimaendeleo katika kutafutiana ajira

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WANAFUNZI WA SENT JOSEPH WAFUNDWA

Moja ya wazazi wa shule ya sent JOSEPH MARIAM amewataka wanafunzi waliomaliza na waliopo sasa wawe na nidhamu ,uadilifu na umoja ndipo watakapofikia malengo yao .ametoa rai kwa wazazi na walezi wawapeleke watoto wao mashuleni. amesema  haya siku ya kuwakutanisha wanafunzi wa sent JOSEPH  kwaajili ya kuwajengea umoja wao kwenye viwanja vya KARIM JEE posta jijini Dar es salaam

habari picha na  ALLY THABITI

SHULE YA SECONDARY SENT JOSEPH YAJA KIVINGINE

Sister TIODORA amesema wameamua kuwakutanisha wanafunzi waliomaliza shule sent Joseph lengo kuwatengenezea umoja wao ili waweze kusaidiana

habari picha na  ALLY THABITI

TAASISI YA UONGOZI YAAIDI MAZITO

Mkurugenzi wa taasisi ya Uongozi  JOSEFU SEMBOJA amesema wataendeleza mambo mazuri yaliofanywa na bodi iliopita .Pia watabuni njia bora na nzuri katika kuwashawishi viongozi waliopo serikalini kujiendeleza kimasomo na kujifunza mara kwa mara katika maswala ya Uongozi. amewataka viongozi wa serikalini waitumie vizuri na kikamirifu taasisi ya Uongozi Tanzania ili kuleta tija ya ukuaji wa uchumi na kuelekea Tanzania ya viwanda kwaajili ya kumuunga mkono rais MAGUFULI . amesema haya jijini Dar es salam kwenye ukumbi wa mwalimu Nyerere uliopo posta .wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya taasisi ya Uongozi yenye jumla ya wajumbe8

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

TANEA YAJA KIVINGINE

Mkurugenzi mtendaji wa TANEA AIZAKI WANGO amesma wamekuja na mikakati imara madhubuti katika kufanya tasmini ya miradi mikubwa lengo kuisaidia serikali kuelekea tanzania ya viwanda na uchumi wa kati . amesema haya kwenye ukumbi wa mwalimu Nyerere uliopo posta jijini Dar es salaam wakati wa kuzindua mpango mkakati wao wa TANEA

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

TUME YA KUDHITI UKIMWI YAITAKA SERIKALI KUTOA PESA KWA WAKATI

RICHADI S.NGIRWA mkurugenzi wa sera ,mipango na utafiti amesema ili kufikia malengo yakutokomeza Ukimwi Tanzania ni vyema serikali itoe fedha kwa wakati

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

IFIKAPO ELFU 2030 UKIMWI KUWA ISTORIA NCHINI TANZANIA

Kiongozi kutoka tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania  amesema ifikapo mwaka 2030 Ukimwi ahutakuwepo na asilimia kubwa ya watanzania watakuwa wanatumia vidonge vya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi . amesema haya jijini Dar es salaam kwenye makao makuu ya tume ya kudhibiti Ukimwi

habari picha na  ALLY THABITI

Thursday 21 September 2017

MIKOA VINARA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania JUMANNE amesema mkoa wa Njombe ,Iringa na Mbeya ni mikoa inayoongoza kwa kiasi kikubwa katika maambukizi ya Ukimwi Tanzania . Ivyo amesema zinaitajika jitiada za makusudi katika kuondoa maambukizi ya Ukimwi kwa mikoa hii na mingine . lengo kuokoa vizazi vinavyokufa na ugonjwa wa Ukimwi. ameipongeza mikoa ya Tanga, Rindi na Mtwara kwa kuwa na kiwango kidogo sana  cha maambukizi ya Ukimwi

habari picha na  ALLY THABITI

Wednesday 20 September 2017

SEKTA BINAUSI YATETA NA SERIKALI

Kiongozi wa sekta binausi  JEMES SIMBEYI  ameiambia seikali ikitaka kufanikiwa kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati ihakikishe inatengeneza miundombinu  ya usafirishaji kwenye majiji ya Tanzania . Pia amesema shirika la Tazara  likiboleshwa kikamilifu litasaidia kukuza uchumi wa Tanzania . ametoa wito kwa wadau wa sekta binausi kushiriki kwenye mikutano ya kimataifa  lengo kuchangamkia fursa zinazojitokeza . amesema haya kwenye mkutano wa siku mbili ulio wajumuisha wadau wa mataifa mbalimbali Duniani  jijini Dar es salaam  KILIMANJARO  hotel

habari picha na  ALLY THABITI

WAZIRI WA UCHUKUZI AKILI KUWEPO KWA MATATIZO SEKTA YA ANGA

Waziri wa uchukuzi prof  MAKAME MBARAWA  amesema uhaba wa marubani, viwanja vya ndege na ndege ni kikwazo na tatizo kubwa  katika sekta ya anga nchini Tanzania .ametoa rai kwa wadau na jamii kuungana na serikali katika kunusuru sekta ya anga .amesema haya kwenye ukumbi wa mwalimu NYERERE uliopo posta na kumpa maagizo moja ya viongozi wa TCAA


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI NAIBU WAZIRI ANTONI PITA MAVUNDE AKIONYESHA KITABU CHA TAFITI ALICHOKIZINDUA

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

SERIKALI KUNUSURU TAFITI

Naibu waziri wa kazi ,ajira, vijana na watu wenye ulemavu  ANTONI PITA MAVUNDE amesema serikali imejipanga kikamilifu katika kuziwezesha tafiti na wafanya tafiti kifedha lengo kuwa na tafiti zenye tija na zenye kutatua changamoto za watanzania .amesema haya kwenye chuo cha CBE

habari picha na  ALLY THABITI

WAANDISI WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA

Mwenyekiti wa waandisi wa Reli ya Tanzania na Zambia [TAZARA] amesema kwaniaba ya waandisi wenzake wanaipongeza serikali ya Tanzania chini ya rais  MAGUFULI  kwa ujenzi wa reli ya kisasa  kwani ukikamilika utatatua matatizo ya usafirishaji mizigo na abilia kupitia reli

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MENEJA WA NMB RICHADI MAKUNGWA AKIKABIDHI CHEKI

Meneja wa NMB  RICHADI MAKUNGWA  amewakabidhi viongozi wa tawara za mitaa Tanzania [ALAT] cheki ya shilingi milioni 100 kwenye ofisi za ALAT jijini  Dar es salaam .kwaajili ya kuwezesha mkutano mkuu wa ALAT  jijini MBEYA ambao utafanyika tarehe 2 na 5 mwezi wa 10 mwaka 2017

habari picha na  ALLY THABITI

ALAT YAJA NA MWELEKEO MPYA

kaimu katibu mkuu wa ALAT wa Taifa  amesema wameamua kuja na mwelekeo mpya  ili kuendana na kasi ya rais  MAGUFULI katika kulinda na kusimamia rasilimali za nchi .Pia ALAT  inamuunga mkono rais  MAGUFULI  kwa kuamia  Dodoma  na amezitaka halmashauri zote apa nchini kutenga fedha kwaajili ya maendeleo ya nchi. kaimu katibu mkuu wa  ALAT  Taifa  ABDALLAH NGODU  amesema tarehe 6 ya mwezi wa 10 ya mwaka 2017 itakuwa nisiku pekee ya kujadili  TARULA [Wakala wa barabara kwenye halmashauri nchini Tanzania]

habari picha na  ALLY THABITI

ALAT YATOA MAAGIZO MAZITO KWA HALMASHAURI

Kaimu mwenyekiti  wa ALAT  Taifa  STIVINI PITA  amesema halmashauri zote nchini zitenge ardhi kwaajili  ya viwanda vidogovidogo lengo kumuunga mkono rais  MAGUFULI  katika kuelekea Tanzania ya viwanda .Pia ardhi ni chachu ya maendeleo amesema haya jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza kuwa tarehe2 na 5 mwaka2017 utafanyika mkutano mkuu wa therathini 33 wa ALAT jijini  MBEYA  .ambako mgeni rasmi atakuwa rais  MAGUFULI  lingo la mkutano kuweka mikakati ya elfumbili 2017 na 2018 . Kauli mbiu ya mkutano huu Ardhi ni chachu ya maendeleo na halmashauri zitenge ardhi kwaajili ya viwanda vidogo vidogo .Kaimu mwenyekiti STIVINI PITA  wa  ALAT  ameishukuru benki ya NMB  kwa kuwapa cheki ya shilingi milioni 100

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

JUMUIA YA TAWARA ZA MITAA TANZANIA ALAT YAAIDIWA MAZITO

Meneja wa benki ya NMB  RICHADI MAKUNGWA  amesema watazidi kuisaidia jumuia ya tawara za mitaa Tanzania [ ALAT]  . lengo iweze kutatua changamoto zinazo wakabili  amesema haya kwenye ofisi za  ALAT  baada ya kuwakabidhi  viongozi wa  ALAT cheki ya shilingi milioni 100 kwaajili ya kuwezesha  kufanyika kwa mkutano mkuu wa  ALAT  . tarehe 2 na 5 mwezi wa kumi  mwaka 2017 jijini  MBEYA. meneja wa NMB amesema watazidi kuifadhiri na kuidhamini  ALAT

habari picha na  ALLY THABITI

Tuesday 19 September 2017

SEKTA YA RELI YAPATA MSUKUMO MPYA

MASANJA K. KADOGOSA  ni mkurugenzi wa kampuni ya reli Tanzania amesema mkutano umeweza kusaidia sekta ya reli kupiga hatua kwani  wadau wengi kutoka nje ya nchi wamesema wataisaidia sekta hii kupiga hatua

habari picha na  ALLY THABITI

WAGENI WAIPONGEZA TANZANIA

Moja ya washiriki kwenye mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali wa ujenzi wa reli na barabara  aipongoza serikali ya Tanzania kwa kuboresha na kuimarisha miundombinu ya reli na barabara kwa kiwango cha kimataifa

habari picha na  ALLY THABITI