Tuesday, 5 September 2017

TAASISI ZINATAKIWA ZIWAFIKIE VIJANA WALIO PEMBEZONI MWA TANZANIA

Mdau anaepinga maswala ya ukatili wa kijinsia JOYCE KIRIA amezitaka taasisi na mashirika yanayotoa elimu na mafunzo kuusu afya ya uzazi na elimu ya uzazi wa mpango kwa vijana waende pembezoni mwa Tanzania ususani vijijini wakatoe elimu na mafunzo kwani vijana wanaoishi vijijini wanakumbwa na matatizo makubwa asa mimba za utotoni, kubakwa,maambukizi ya ukimwi na magonjwa ya zinaa  na atimae kupelekea vifo vya vijana kwa wingi kutokea endapo wakipatiwa mafunzo na elimu tutaokoa nguvu kazi kubwa ya Taifa asa vijana na tutafanikiwa kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati JOYCE KIRIA  ametoa rai kwa vijana wachache wanaopata fursa ya mafunzo na elimu juu ya afya ya uzazi waitumie vizuri na waelimishe wenzao amesema haya kwenye ukumbi wa mwalimu  NYERERE uliopo posta jijini Dar es salaam

habari picha na ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment