Tuesday 31 August 2021

MKURUGENZI WA UN GLOBAL COMPACT KUWAFUTA CHOZI WENYE ULEMAVU


 Marsha Yambi Mkurugenzi wa UN GLOBAL COMPACT amesema Report walioitoa ya HUMAN RIGHTS AND BUSINESS 2020/21 Wataakikisha inawafia watu wenye Ulemavu wa Aina zote .

Kwa upande wa wasio Ona watachapishiwa Kwa maandishi ya nukta Nundu, Kwa sasaivi wataandaa Kwa njia ya sauti .

Amesema Lengo la kutoa report hii Waajili wasikiuke Haji za binadamu Kwa wafanyakazi wao .Marsha Yambi amewashukuru LHRC,TPSF,ATE pamoja na taasisi zingine Kwa ushirikiano wao .

Habari picha na Ally Thabiti

WAKILI WA KUJITEGEMEA PRISCA CHOGERO ATOA TANO KWA LHRC

Prisca Chogero Wakili wa Kujitegemea ameupongeza Uongozi wa LHRC Kwa kutoa ripoti ya HUMAN RIGHTS AND BUSINESS REPORT 2020/21 TANZANIA MAINLAND kwani changamoto za waajiliwa zitatatuliwa.

Pia amewataka wafanyakazi watoe taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili makazini .pia ametaka kuwepo Kwa Sera za Ajira Kwa watu wenye Ulemavu vitekelezwe Kwa vitendo.

Nakuwepo na miundombinu rafiki Kwa waajiliwa wenye Ulemavu .

Habari picha na Ally Thabiti



PICHANI GARI LA THAMANI YA MILIONI 10 KWA MSHINDI WA MISS EAST AFRICA


 Kama Inavyoonekana Pichani hili Ndio GARI Aina ya Nisan Ndio GARI inayo waniwa na Walimbwende.

Habari picha na Ally Thabiti

TAASISI YA INQABA BIOTEC KUWAFIKIA WATU WENYE ULEMAVU


 Kenneth Mbwanji,MSc Regional Director amesema katika utambuzi wa vina 7(DNA) wataakikisha namna yakuwafikia watu wenye Ulemavu Lengo wawe na uelewa wa pamoja  na namna ya kutambuwa umuhimu wa maswala ya vina 7.

Ametoa wito kwa watu wenye Ulemavu kushiriki kikamilifu kwenye utambuzi wa vina 7 (DNA).

Habari picha na Ally Thabiti

JESSICA MSHAMA AIPONGENZA TCCIA


 Mkurugenzi wa NAKUWA NA TAIFA LANGU ameipongeza TCCIA Kwa kuweza Kuwainua Wàjasilia Mali wadogo  kupitia taasisi Yake NAKUWA NA TAIFA LANGU  atatoa elimu Kwa watu wenye Ulemavu .

Habari picha na Ally Thabiti

VIGEZO VYA KUSHIRIKI MISS EAST AFRICA


 Raisi wa Mashindano ya MISS EAST AFRICA Rena Collist amesema kwenye Mashindano ya MISS EAST AFRICA Sheria,Kanuni na Taratibu za Mashindano zitazingatiwa . 

Pia watakuwa wanaangalia tabia za washiriki, urefu,elimu ambako mshiriki anatakiwa awe amemaliza kidato cha 4 na kuendelea .swala la uraia utazingatiwa kutokana na nchi anayotoka . Ameongezea Kwa kusema kuwa Mashindano haya yatakuwa yanafanyika kila mwaka na yatakuwa Kwa kila nchi.

Habari picha na Ally Thabiti

MISS EAST AFRICA YAJA NA DONGE NONO


 Jolly Mutesi Makamu wa raisi amesema wameamuwa kuleta Mashindano ya MISA EAST AFRICA Lengo kuwawezesha wasichana waweze kujikwamuwa kiuchumi na kuibuwa vipaji vyao . 

Zawadi ambazo watazitoa ni kiasi cha shilingi milioni 140 pia Fedha hizi watakazo zipata wataweza kuanzishwa biashara zao . 

Jolly Mutesi amesema nchi zipatazo 16 za kiafrica zitashiriki ikiwemo Kenya,Uganda,Burundi,Sudani ya Kusini , na Tanzania wenyeji wa Mashindano.

Habari picha na Ally Thabiti

BASATA YABARIKI MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA


 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Matiko Mniko amewataka watanzania ususani wanawake kuanzia miaka 18 mpaka 26 kujitokeza Kwa wingi katika kushiriki Mashindano ya MISS EAST AFRICA  kwani wataweza kuitangaza Tanzania na kuwavutia watu kuja kutalii na kuwekeza .

Ambako itapelekea watu kupata Ajira na kujikwamuwa kiuchumi . Katibu wa Baraza la Basata amewatoa hofu washiriki wote wa  shindano la MISS EAST AFRICA  kuwa zawadi za shilingi milioni 140 zipo na Hari yenye thamani ya milioni110 lipo . Kwani Basata  mikataba yote wamepitia na watailinda .

Habari picha na Ally Thabiti

Sunday 29 August 2021

MRATIBU WA MAFUNZO YA KIIISLAM MTANDAONI ABAINI MBINU


 Mahadhi Mratibu wa Mafunzo ya Uongozi Mtandaoni Kwa Waislamu amelishukuru Baraza la Kiislamu tanzania (BAKWATA) Kwa kumpa ushirikiano amesema Mafunzo haya ya Mtandaoni yatawajengea uwezo Viongozi wa BAKWATA katika kusimamia miradi Yao .

Nae Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakari Zuberi amewataka Waislam nchini Tanzania kutumia Mafunzo haya kwaajili ya kupata Ujuzi na maarifa mbalimbali. 

Ambako kwenye Mafunzo haya Wanafunzi 232 wamehitimu na wengine 450 wanaendelea kupata Mafunzo .ambako Mafunzo haya gharama Yake no shilingi elfu500000 ya kitanzania . Mratibu Mahadhi anapatikana jengo la GSM eneo la Lumumba Golofa ya 6.

Kwa Mawasiliano zaidi 0764 244867.

Habari na picha na Ally Thabiti

JATU PLC KUTOKOMEZA UMASIKINI TANZANIA


 Mkurugenzi wa Kampuni ya JATU PLC  ndugu Peter Isare amewataka watu kujiunga na JATU iliwaweze kujinasua na wimbi la umasikini ambako akijiunga na JATU atapata fursa mbalimbali ikiwemo kupata mashamba makubwa ya kulinda .

Na pia watatafutiwa Masoko ya mazao Yao ndani ya nchi na nje ya nchi .

Habari picha na Ally Thabiti

SIMBA YAJA KIVINGINE

 Kaimu Afisa Habari wa Simba Ezekieri Kamwaga amesema Timu ya Simba imeamuwa kuzinduwa App Yao Lengo wanachama ,wapenzi na mashabiki wa Simba wapate taarifa zilizo sahihi na Kwa wakati sahihi.

Ambako wanachama wa Simba watatoa shilingi elfu 2000.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA ATOA NENO KWA RITA


 Prof Paramagamba Kabudi Waziri wa Katiba na Sheria amewataka Rita kutoa vyeti vya ndoa Kwa njia ya kieletroniki pia wasajili Viongozi wa Kidini watakao wanafungisha ndoa .

Kwani Kiongozi wa Kidini asiyekuwa na Cheti cha kufungisha ndoa aluusiwi kufungisha ndoa popote pale. Huku akitoa wito kwaRita  kuwafikia watu wenye Ulemavu kwenye huduma wanazozitoa amesema haya jijini Dsm. 

Habari na Ally Thabiti

SERIKALI YATENGA BILIONI 149.7 KWAAJILI YA WATU WENYE MAISHA DUNI

 Zakaria Muyenji Kutoka TIRA amesema serikali imeamuwa kuwafikia watu wenye Maisha duni Kwa kutenga kiasi cha Fedha bilioni 149.7 .Lengo watu wenye Maisha duni waweze kupata bima ya Afya . 

Nae Kwa Upande wake Janeti Hiza  Kutoka wizara ya Fedha amezitaka Kampuni za bima zitoe huduma za bima ya Afya Kwa gharama nafuu.

Habari na Ally Thabiti

WAZIRI WA MICHEZO AFANYA ZIARA

 Waziri wa Michezo ,Sanaa, Habari na Utamaduni Inosenti Bashungwa amerizishwa na maandalizi ya Timu ya Taifa ya Tanzania  amesema wazazi na walezi waweze kutunza vipaji vya watoto wao . Pia kutakuwa na shule za kufundishia Michezo Kwa kila Mkoa kutakuwa na shule moja .

Waziri Bashungwa amesema watu wenye Ulemavu wanashirikishwa kikamilifu kwenye Michezo yote . 

Habari na Ally Thabiti

JENI LIYATUU ATOA NENO KWA JAPAN

 Mratibu wa Mradi wa KAIZEN Jeni Liyatuu anaipongeza nchi ya Japan Kwa kuleta mradi wa KAIZEN nchini Tanzania kwani mradi huu umeongeza tija ya uzalishaji katika Viwanda vyetu.

Na umewajengea Uwezo mkubwa na mzuri katika maswala ya Utawara Bora Kwa Viongozi na usimamizi mzuri wa Lasilimali watu na Fedha , Jeni Liyatuu amewataka vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa za mradi wa KAIZEN.

Nae Waziri waViwanda na Biashara Zanzibar amesema mradi wa KAIZEN umeweza kuleta chachu ya kukuwa Kwa Uchumi Zanzibar ivyo ameitaka nchi ya Japan iendelee na mradi huu kwani unaleta maslai mapana katika nchi ya Tanzania .

Habari na Ally Thabiti

TUME YA MWIGULU YAINGIA MZIGONI

 Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameki Mchemba amezinduwa Tume ya kufuatilia matumizi ya Fedha,bajeti inavyopangiliwa na namna ya mifumo ya ukusanyaji wa mapato  .

Lengo la Tume hii kuanzishwa iweze kuibuwa vyanzo vipya vya mapato ,kufuatilia matumizi ya Fedha za serikali na kuangalia makisio ya bajeti ya Tanzania .

Waziri Mwigulu Mchemba amevitaka Tume hii kubaini changamoto zinazowakabiri wafanya biashara na wake na mapendekezo ya namna ya kuwashawishi watu kutokukwepa Kodi. 

Nae Mjumbe wa Time ya Mwigulu prof Osolo amesema Tume Una Wajumbe 10 itafanya KAZI ndani miezi 6 na ameahidi Kwa niaba ya wenzake kuja na majibu ya kutosha .

Habari na Ally Thabiti

Tuesday 24 August 2021

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI AWA NA MATUMAINI NA KAIZEN

 William Olenasha Naibu Waziri wa Uwekezaji Tanzania amevitaka Sekta binausi nchini Tanzania watumie fursa zinazopatikana kwenye mradi wa KAIZEN Pia amewataka watanzania kutumia mradi wa KAIZEN kwani wataweza kujikwamuwa kiuchumi  na wataweza kupata Ujuzi wa Aina mbalimbali . 

Naibu Waziri wa Uwekezaji amesema serikali inafanya mabadiliko ya Sera na Sheria Lengo kuendana na uendeshaji na mradi guy wa KAIZEN ili kusiwe na mkwamo katika uendeshaji mradi wa KAIZEN. 

Nae Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Joketi Mwengelo ameapongeza nchi yaJapani Kwa kuleta mradi waKAIZEN kwani utaleta chachu ya kukuwa Uchumi Kwa watanzania na nchi ya Tanzania  amewataka watanzania kuchangamkia fursa hii.

Huku akiwataka vijana kuto kata tamaa.

Nae Jeni Liatuu kiongozi wa mradi wa KAIZEN  amesema watamfikia kila mtanzania Lengo Kuwajenga uwezo na kuwapa maarifa ya namna ya kujikwamuwa kiuchumi na kuondokana na umasikini .amesema haya jijini Dsm.

Habari na Ally Thabit

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AWAITA WAWEKEZAJI

 Prof Kitlo Mkumbo Waziri wa Viwanda na Biashara amewataka watu kujitokeza Kwa wingi katika kuwekeza kwenye Viwanda 20. Pia amewataka  SIDO na NDC kuendeleza Viwanda walivyokabidhiwa na wizara ya Viwanda na Biashara .

Nae Mkurugenzi wa TEMLO prof Frederick  Kaimba amesema wameamuwa kutengeneza mashine za kutengeneza Sukari . Lengo kuwafikia Wajasilia mali wadogo na Kuwainua wakulima wa miwa na kuondoa uhaba wa upatikanaji wasukari Tanzania. 

Ujenzi wa Mashine hizi umefikia asilimia 40. Kiasi chabilioni 19 zitakuwa zimeokolewa kutokana na upatikanaji wa Mashine hizi. Mashine zitauzwa Kwa shilingi milioni Mia mbili hamsini.amesema haya jijini Dsm 

Habari na Ally Thabiti

Thursday 5 August 2021

MO ATOA MABILIONI KWA SIMBA

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mo Deuji ametoa kiasi cha bilioni 20 kwaajili ya Uwekezaji Simba na amewataka wanasimba waendelee kumuunga mkono na watasajili wachezaji wa kimataifa .

Habari na Ally Thabiti 

CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI CHAWAKWAMUWA WANANCHI NA UMASIKINI

 Prof Mwabless Malila  amewataka watu kujiunga na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatoa elimu bora ambako mtu  akimaliza kusoma anapata Ajira .

Pia Chuo hiki kupitia mradi wa UNDP kimewakwamuwa kiuchumi wakazi wa kanda ya Ziwa Kwa kuwapa elimu ya Viazi Lishe na Wavuvi WA kanda ya Ziwa wameweza kufundishia namna ya kutengeneza mabarafu .

Ambako Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatoa elimu Kwa gharama nafuu Kwa ngazi ya Cheti,Diploma,Shahada ya Kwanza na zinginezo .

Chuo kinapatikana Mwanza eneo la Kisesa na Bwilu na Kwa Dodoma eneo la Miuji mjini ambako Hosteri zipo za kutosha  .prof Mwabless Malila ametoa wito kwa watu kukitumia Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kwa elimu,utafiti na ushauli amesema haya kwenye Maonyesho ya 16 ya Vyuo Vikuu yalioandaliwa na TCU ambako yamefanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dsm.

Habari na Ally Thabiti 


HAJI MANALA AMKALIA KOONI MO NA KUMSHIKA PABAYA


Aliye kuwa Msemaji wa Simba Haji Manala amemtaka Mwekezaji wa Simba amlipe pesa zake na  aache kuwaongopea Wana Simba kuwa ametoa pesa za Uwekezaji ndani ya Simba  si  kweli .

Amemtaka C.o wa Simba Barbra Hassani Aache kumfuatilia na kumpaka matope .

Habari picha na Ally Thabiti 

GLOBAL LINK EDUCATION YAJA KIVINGINE KIELIM


 Neema Mabula Meneja wa Tawi la Dsm Kutoka Global link Education amesema wanatoa mkopo wa  fedha wa asilimia 50 mpaka asilimia 70 kwaajili ya elimu .

Na wanawatafutia Wanafunzi fursa ya kwenda kusoma nchi za China ,Indiana nchi zinginezo Kwa gharama nafuu .Pia wanawatafutia Wanafunzi Vyuo vya hapa Tanzania  .

Global link Education wanapatikana Arusha,Mwanza,Mbeya eneo la Mwanjelwa, Dodoma,Zanzibar na Dsm  amesema haya kwenye Maonyesho ya Vyuo Vikuu viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dsm .

Habari picha na Alloy Thabiti 

TAWA YAWATA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA


 Mwenyekiti wa Bodi ya Tawa Jenelali  Mstaafu Hamisi Semfuko amewataka watanzania kujitokeza kwenye Uwekezaji wa Wanyama Poli ambako mwaka 2018 Tawa ilianzisha mchakato wa Uwekezaji .

Ametoa wito kwa watanzania waishio kwenye vijiji kutunza ,kulinda na kuhifadhi maeneo ya Hifadhi ya Wanyama Pol . Kwani watanufaika kiuchumi .

Amewataka makampuni ya kitanzania kujitokeza kwenye Uwekezaji wa Wanyama Poli kwani kwenye Kampuni 10 zilizojitokeza Kampuni 1 ya watanzania.

Habari picha na Ally Thabiti

MSANII WA KIMAREKANI AMWAGA MAMILIONI TANZANIA


 Msanii Kameko Tarnez Kutoka Marekani amekuja nchini Tanzania kwaajili ya kutafuta vipaji vya waimbaji ambako tarehe11 mwezi wa 10 mwaka 2021 shindano litaanza.

Huku Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 11 fedha ya kitanzania pia Kwa sasa atazinduwa I. P . Yake  na atarekodi nyimbo na Daimondi na Ally kiba pamoja na Amonaizi .

Amewataka watanzania kulinda na kudumisha Amani iliyopo na waendelee kuwa na umoja na amewataka wamuunge mkono Kwa ujio wake hapa Tanzania .

Habari picha na Ally Thabiti