Monday 10 April 2023

IRINGA WASHUKURU KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO



Picha 2: Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) Regina Kipemba akishirikiana na Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gerson Mpondo kumfanyia mwananchi kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam kutoka JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH.

Picha 3: Mtafiti wa Taasisi ya Moyo jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuuliza maswali ya ufahamu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo mkazi wa Iringa Christina Chibona kabla ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.Picha 1: Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Epheta Edward akimpima wingi wa sukari mwilini mkazi wa Iringa Magreth Sanga wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

 Iringa washukuru kupata huduma za matibabu ya moyo 

Na: Genofeva Matemu – Iringa

06/04/2023 Wananchi wa Mkoa wa Iringa wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuwezesha huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo kuwafikia kwa karibu kwani wananchi wengi hawana uwezo wa kufuata huduma za kibingwa mahali zilipo.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali waliofika katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH).

Akizungumza baada ya kupatiwa matibabu ya moyo mkazi wa Iringa Mzee Nicholas Kinyamagoha alisema hakuwahi kufanya uchunguzi wa moyo wake tangu kuzaliwa kwake kutokana na huduma hizo kuwa mbali na sehemu anayoendesha maisha yake.

Mzee Nicholas alisema baada ya kusikia ujio wa madaktari bingwa wa moyo Mkoani Iringa akaona ndio fursa pekee anayoweza kutumia kuchunguza moyo wake kwani kutokana na umri wake kuwa zaidi ya miaka 60 yupo katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo.

“Nashukuru leo nimefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kupata fursa ya kupimwa moyo wangu, awali walishangaa kuona shinikizo langu la damu kuwa juu lakini baada ya kuwaeleza taarifa mbaya niliyopokea wakati nikiwa kwenye foleni kusubiri matibabu walinipa muda wa kupumzika na kuchunguzwa tena shinikizo langu la damu”, alisema Mzee Nicholas.

Mzee Nicholas alisema ikiwezekana huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza ambayo sio rahisi kuyapata katika Hospitali zilizopo mikoani ziwe zinatolewa angalau mara moja kwa mwaka ili wananchi wapate nafasi ya kutibiwa kwa wakati pale wanapokutwa na magonjwa hayo.

“Nimefurahi sana leo nimepima moyo wangu kwa mara ya kwanza, nimeweza kujua namna ya kujikinga ili nisipate magonjwa ya moyo na nimesisitizwa nisiache kutumia dawa za shinikizo la damu ambazo nimekuwa nikizitumia kwa miaka miwili sasa”, alisema Mzee Nicholas.

Akizunguma kwa nyakati tofauti mkazi wa Iringa Felister Chang’a alisema mwaka 2020 alikuwa na dalili za kupumua kwa shida, maumivu makali upande wa kushoto wa kifua yaliyoenda hadi mgongoni hivyo kufika katika moja ya Hospitali zilizopo Iringa na kupimwa moyo lakini majibu yalitoka kuwa hana shida ya moyo.

Felister alisema baada ya uchunguzi aliofanyiwa mwaka 2020 alipewa dawa za maumivu na kuendelea na maisha lakini mwaka huu zile dalili zimerudi na hakuwa na chakufanya kwani hapo awali alishaambiwa sio shida ya moyo.

“Niliposikia ujio wa madaktari bingwa wa moyo kutoka JKCI kwakweli nilifurahi sana kwani naamini leo naenda kupata suluhu ya tatizo nililinalo kwasababu ninapopata maumivu ya kifua na kushindwa kupumua kunanifanya nishindwe hata kufanya shughuli zangu”, alisema Felister.

“Jana nilimleta mtoto wangu hapa kwa ajili ya kutibiwa, baada ya kufika hapa nikaona bango linaloonyesha uwepo wa madaktari bingwa wa moyo nikakumbuka mimi pia nahitaji kumuona daktari wa moyo kutokana na hali yangu ya maumivu ya kifua, nashukuru sijakutwa na shida ya moyo wameweza kunichunguza na kuona tatizo la vidonda vya tumbo”, alisema Felister.

Akiongea kwa furaha Felister amewashukuru Madaktari bingwa wa moyo kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wananchi wa Iringa kwani bila ya wao kufika asingejua kama maumivu anayoyapata yanasababishwa na vidonda vya tumbo.

Naye mkazi wa Songea aliyesafiri kufuata huduma za matibabu ya moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Zamda Bakari alisema baada ya kusikia ujio wa madaktari bingwa wa moyo hakuona shida kusafiri kutoka Songea kufuata huduma hiyo kwani amekuwa akihitaji kuchunguza moyo kwa muda mrefu.

“Nilimpoteza baba yangu kwa kifo cha ghafla na baada ya kufuatilia tuliambiwa alipata shambulio la moyo hivyo kumsababishia kupata kifo cha ghafla, baada ya kifo cha baba yetu nimekuwa makini nikisikia huduma za kibingwa za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza nawiwa kuchunguza afya yangu ili nijitambue”, alisema Zamda.

Zamda aliwashauri wananchi wanzake kupima afya zao mara kwa mara pale wanapopata nafasi kwani kumpoteza mtu wa karibu kwa kushindwa kujua kama alikuwa anaumwa inaumiza.

HABARI PICHA NA ALLY THABITI

ZITO KABWE ATEMA CHECHE



Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Kiongozi Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe leo April 10 kimechambua ripoti ya CAG ambapo pamoja na mambo mengine kimeitaka Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti


Akiongea na Waandishi wa Habari, Dar es salaam leo, Zitto Kabwe amenukuliwa akisema “CAG amefanya ukaguzi wa Akaunti ya Deni la Taifa na kueleza kwamba hadi Juni 30, 2022 lilikuwa Shilingi trilioni 71 ambapo ni ongezeko la 11% kutoka deni la shilingi trilioni 64.5 lililo ripotiwa mwaka 2020/21”

“Uchambuzi wetu unaotokana na Ripoti ya CAG unaonesha kuwa katika mwaka huu wa ukaguzi Serikali ilichukua mikopo ya ndani kwa 30% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano”

“Vilevile mikopo ya nje yenye masharti nafuu iliyochukuliwa na Serikali ilikuwa 33% zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge, mwenendo huu unaonesha Serikali kutojali na kudharau Mamlaka ya Bunge, tunaitaka Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti”

HABARI PICHA NA
ALLY THABITI

MSIKITI WA MANYEMA YA MUENZI MTUME MUHAMMAD

Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Sheikh Jongo amesema lengo la kumkumbuka Mtume Muhammad kwenye mwenzi mtukufu wa Ramadhani kwenye chungu cha kumi na saba (17) ni kukumbuka vita ya Badri ambako vita hii ndiyo ilibainisha haki na batri hivyo ni vyema waislamu kuipigania dini ya kiislamu kwa hali na mali Sheikhe Jongo amesema kuanzia mwakani kisa cha vita badri kwenye msikiti wa manyema itaazimishwa kwa awamu mbili kuanzia swala ya adhuri na swala ya Alhasili nae sheikh mziwanda ameupongeza msikiti wa manyema kwa kumuenzi na kumkumbuka Mtume Muhammad kupitia vita ya Badri kwani adisi na Quruan vimesesomwa baada ya swala ya Alhasili na kupata kisa cha Abou Sufian na wafuasi wake hii ni Elimu tosha na kubwa sana.

Habari na ALLY THABITI

STEVEN NYERERE AWATAKA WATANZANIA KULEJESHA MATUMAINI KWA MSICHANA JACKLINE

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama ongea na mwanao Steven Nyerere amewtaka watu kujitokeza kwa wingi kumsaidia binti aliyepata ulemavu kwenye ajali ya gari Jackline iliaweze kulejesha furaha na matumaini kwenye maisha yake, amempongeza msanii Diamond Platnumz kwa kusaidia binti huyu mwenye ulemavu.
Habari na ALLY THABITI

MWENYEKITI CCM KATA YA KISUTU AELEZA MAMBO MAZURI

Mwenyekiti wa CCM kata ya Kisutu amesema katibu wa CCM aliyemaliza muda wake wilaya ya Ilala amefanya mambo mema na mazuri.

Habari na ALLY THABITI

TUME YA MADINI YAWAGUSA WATU WENYE ULEMAVU

Mkurugenzi wa Biashara na Mazingira kutoka tume ya madini amesema leseni wanazozitoa wachimbaji madini wanazingatia makundi yote, pia amsema mkutano ulioandaliwa na STAMIKO itasaidia kukuza sekta ya madini.

Habari na ALLY THABITI

MENEJA MRADI GIZ ATOA NENO

Sudi Samwil Mejena Mradi wa GIZ amsema taasisi yao imetoa fedha kwa taasisi tatu za Kitanzania lengo waende wakakabiliane na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Habari na Ally Thabiti

TARURA WILAYA YA DODOMA YAJA KIVINGINE

Meneja wa Tarura wilaya ya Dodoma Mjini Emmanuel Mfinanga amesema wamejenga madaraja ya kutosha pamoja na makaravati pia wemejenga barabara kwenye kiwango cha rami na changarawe hayo ndiyo mafanikio waliyoyapata chini ya Rais Dr. SAMIA SULUH HASSAN.

Habari na ALLY THABITI

NBS YAWAFUNDA WATENDAJI NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA

 Ofisi ya Taifa ya takwimu imekutana na watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa wa mkoa wa Dar es salaa lengo kueleza namna ya kutumia takwimu za sensa.

Habari na ALLY THABITI

RAIS KIKWETE USO KWA USO NA HAKI JINAI

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza tume ya haki jinai kwa kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali, nae Waziri Mkuu Mstaafu Walioba pamoja na Paramaganda Kabudi wameitaka tume ya haki jinai kutoacha mawazo ya watu nae kwa upande wake Sheikh Issa Ponda pamoja na jaji mstaafu Miyayo wamesema kuwepo kwa tume ya haki jinai kutakuwa ni suluisho kwa kupatikana haki.

Habari na ALLY THABITI

SACP ATANGAZA VITA DAR ES SALAAM

 SACP Kamanda Jumanne Mulilo wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema yeyote atakayejihusisha na ualifu jeshi la Polisi litamkamata na kumchukulia hatua kari.

Habari na ALLY THABITI