Thursday 16 May 2024

MATAPELI WA MTANDAONI WATIWA MBALONI

 Mkuu wa Jeshi la Police Kanda Maalum ya Dar es salaam  Jumanne Mulilo amesema wamewakamata watu 27 jijini dar es salaam ambao wamekuwa wakifanya utapeli kwa kutumia raini za simu za mkononi  ,matapeli hawa walikuwa wanatuma jumbe kwenye simu tofautitofauti ili watumiwe pesa .

Jeshi la Police linawashukuru wananchi kwa kutoa taarifa ambazo zimepelekea kukamatwa kwa matapeli hawa ,kamanda Mulilo amesema mpaka sasa jumla ya matapeli wanaotumia simu za mkononi kwaajili ya kutapeli watu wameshakamatwa 85 amesema haaya wakati akizungumza na wanahabari makao makuu ya Jeshi la Police kanda maalum jijini dar es salaam. 

Habari na Ally Thabit 

Wednesday 15 May 2024

DR LUCAS MAGANGA MTAFITI NIMR MBEYA AELEZA CHANJO KUMI 10 ZA UKIMWI


 Taasisi ya NIMR  Mkoa wa Mbeya inafanya tafiti kwenye magonjwa mbalimbali mfano marelia,ukimwi ,  Kifua kikuu ,kansa na magonjwa mengineyo Dr  Lucas Maganga mtafiti taasisi ya utafiti NIMR  Mbeya ameitaka jamii kuwa na uvumilivu kwa watu wanaofanya tafiti kwani tafiti autoi majibu ya hapo kwa hapo.

Ameitaka jamii watafiti wanapoenda kufanya tafiti zao wawape ushilikiano wa kutosha kwani utafiti unaitaji ushiliki mkubwa wa jamii , taasisi ya NIMR  Mbeya inafanya kazi ya utafiti kanda ya kusini pamoja na mkoa wa mbeya kwa ujumla ambako mwaka1990 taasisi hii ilikuwa na mashilikiano na wabia kutoka ujerumani na marekani lakini ilipofika mwaka 2008 taasisi  hii ya utafiti Mbeya ilichukuwa na taasisi ya utafiti NIMR  ambako kwa sasa inatambulika taasisi ya utafiti  NIMR  Mbeya.

Dr Lucas Maganga amesema taasisi ya NIMR  Mbeya imefanya tafiti za chanjo 10 za UKIMWI  lengo kupata tiba na namna ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI  kupitia chanjo hizi walizofanyia tafiti taasisi ya NIMR  Mbeya inajumla ya wataalam 170

Kupitia Tafiti zao Wana Mipango na Mikakati ya kufikia makundi yote kwa sasa watu wenye uziwi wana mtaalam mmoja ambaye anatumia Lugha ya Alama, taasisi hii inasaidia serikali katika kufanya mabadiliko  ya kisera kwenye sekta ya afya.

Habari picha na Ally Thabit 

KAMATI YA BUNGE INAYOSIMAMIA MASWALA YA UKIMWI,AFYA NA MAZINGIRA YATEMBELEA TAASISI YA UTAFITI IFAKARA INSTITUTE


 Mbunge wa Jimbo la Ndanda na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Ukimwi,Afya na Mazingira Devidi Mwambe akimwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hii kama amavyoonekana pichani akipata maelezo kutoka kwa mtafiti wa taasisi ya IFAKARA INSTITUTE  Kama wanavyoonekana pichani wakiwa kwenye banda. Ambako mtafiti huyu akimwelezea namna taasisi ya IFAKARA ilivyogundua inside ya kukabiliana na mbu lengo ni kutokomeza marelia nchini.

Habari picha na Ally Thabit .


TAASISI YA IFAKARA YAIMIZA USHIRIKIANO KWA WANANCHI


 Alex Limwagu Mtafiti wa Taasisi ya Ifakara amesema kongamano  la kisayansi  la 32  litasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mabadiliko ya kiutafiti nchini tanzania kwani watafiti wengi kutoka nchi mbalimbali wataeleza mbinu na njia wanazozitumia katika kufanya tafiti zao pamoja na teknolojia za kisasa za kufanyia tafiti.

 Ameipongeza na kuishukuru NIMR  kwa kuweka kongamano ili kwani litajenga mausiano mazuri na watafiti hapa nchini na nje ya nchi na kukuza ushirikiano wa kitafiti.

Ametoa wito kwa jamii kutoa ushilikiano pindi watafiti wanaitaji taarifa kwaajili ya utafiti pamoja na maeneo ya kufanyia tafiti mfano bila utafiti wa kuuwa mbu kwa kutumia dawa using fanyika mpaka Leo mazalia ya mbu yangekuwa  mengi na kusingekuwa na tafiti ya kutibu marelia watu wengi wangekufa kwaajili ya marelia. 

Amesema haya kwenye kongamano la 32 la watafiti wa sayansi lililoandaliwa na NIMR  kwenye ukumbi wa mwalimu nyerere  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

KAMATI YA UKIMWI AFYA MAZINGIRA YA BUNGE YAPONGEZA TAFITI ZA NIMR


 Mbunge wa Mkoa wa Lindi Devidi Mwambe ambae amemwakilisha Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ukimwi na afya mazingira amesema tafiti zinazofanywa na NIMR  zinafaida kubwa Sana ,kwani tafiti hizi zinatatuwa changamoto katika jamii na zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha na kuandaa sera kwenye sekta ya afya.

Mbunge Mwambe ameipongeza NIMR  kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufanya tafiti zenye tija na mafanikio makubwa ikiwemo namna ya kukabiliana na HIV na magonjwa mengine . Swala la tafiti kuwekwa kwenye maandishi ya nukta nundu kwaajili ya wasioona ni muhimu pia matumizi ya Lugha za alama kwa wenye uziwi ni vyema yazingatiwe.

Amesema haya kwenye kongamano la 32 la utafiti wa  kisayansi  uliofanyika ukumbi wa mwalimu nyerere  jijini dar es salaam. 

Habari picha na Ally Thabit 

TCRA YAKUTANA NA WADAU WA HABARI

 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tcra Mwandisi Kisaka amesema lengo la kukutana na wadau wa habari ni kuweza kujadili changamoto wanazokutana nazo ili serikali iweze kufanyia kazi.

Habari na Ally 

Tuesday 14 May 2024

NAIBU WAZIRI MKUU AIPONGEZA NATIONAL INSTITUTE FOR MEDICAL RESEACH (NIMR)


 Dr Doto Mashaka Biteko amesema tafiti zinazofanywa na  National Institute  for Medical Reseach (NIMR) zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta mbalimbali nchini tanzania Pia tafiti hizi zinawezesha serikali kufanya maamuzi sahihi kupitia tafiti zao na kupelekea kupatikana maendeleo kwa haraka na kwa kasi nchini tanzania .

Naibu Waziri Mkuu Dr Doto Mashaka Biteko amesema serikali itaendelea kutoa fedha nyingi kwenye National  Institute for  Medical Reseach (NIMR) wafanye tafiti zao za sayansi  kwa kisasa kupitia teknolojia mpya kwani tafiti zao zimeboresha huduma za kiafya nchini na kupelekea kuwepo na madiliko ya sera za afya.

Pia serikali itaendelea kuboresha miundombinu kwenye mahabarata wanazofanyia tafiti na kuongeza wafanyakazi kwenye taasisi  pamoja na kuboresha maslai yao.amesema haya kwenye kongamano la 32 lililojuisha watafiti wa kisayansi  kutoka mataifa mbalimbali duniani ambako linafanyika jijini dar es salaam  ukumbi wa mwalimu nyerere. 

Habari picha na Ally