Tuesday 31 October 2017

WAKAZI WA KINONDONI WATAKIWA KUTII SHERIA ZA MAZINGIRA BILA SHURUTI

Afisa mazingira kutoka halmashauri ya Kinondoni  ARUBATI MGEBUSO  amewataka wananchi wa kinondoni na watanzania kwa ujumla kufuata na kuzitekeleza sheria za utunzaji wa mazingira ili kuwa na mazingira safi , bora na salama kwaajili ya afya zetu . amesema mafunzo alioyapata kutoka baraza la mazingira  [NEMKI]  atayatumia katika kuelimisha jamii

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

UBUNGO YAIPA TANO BARAZA LA MAZINGIRA

Afisa mazingira kutoka halmashauri ya Ubungo EZRA GUYA amesema kutokana na mabadiliko ya kiteknorojia katika uchafuzi wa mazingira mafunzo anayo yapata kutoka baraza la mazingira [NEMKI] yatamuwezesha kukabiliana na uchafuzi wa mazingira waaina yeyote . amesema viwanda vilivyojengwa kwenye makazi ya watu katika halmashauri ya Ubungo ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira katika jamii .Pia maji taka na kelele mbalimbali ni vyanzo vikuu vya uchafuzi wa mazingira

habari picha na  ALLY THABITI

MIPANGO MIJI MIBOVU NIKIKWAZO CHA USAFISHAJI MAZINGIRA

Afisa mazingira wa halmashauri ya Ilala  NEEMA SITA MAJIJA  amesema wao Ilala wanakabiliwa na tatizo la ujengwaji nyumba bila mpangilio ivyo ni kikwazo kikubwa kwao pindi wapoenda kusafisha mazingira . kwani magari mengi ayafiki maeneo usika

habari picha na  ALLY THABITI

WANANCHI WA TEMEKE KUNUFAIKA NA ELIMU YA MAZINGIRA

MOTONGORI CHACHA  afisa mazingira kutoka wilaya ya Temeke amesema mafunzo alioyapata  kutoka baraza la mazingira [NEMKI] atatumia kwa kuelimisha wakazi wa Temeke ili waepukane na uchafuzi wa mazingira

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

AFISA MAZINGIRA WA KIGAMBONI ANENA MANENO MAZITO

KIARUZI  afisa mazingira wilaya ya kigamboni amewataka wananchi wa kigamboni watunze mazingira yao juu ya uchafu.Lengo wawe na afya bora ili wakuze uchumi wao na Taifa  .pia itasaidia serikali pesa za madawa kupeleka kwenye maendeleo mengine ya Taifa

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

UCHAFUZI WA MAZINGIRA WAUNDIWA MIKAKATI MIZITO

Mkurugenzi mtendaji wa  uzingatiaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira NEMKI  RUTHI RUGWISHA  amesema wameamuwa kutoa mafunzo na mbinu za kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa maafisa mazingira katika halmashauri hapa nchini . Lengo kuondoa na kutokomeza uchafuzi wa mazingira  amesema haya kwenye mafunzo ya maafisa mazingira wilaya ya kinondoni eneo la makumbusho jijini Dar es salaam .washiriki 33 kutoka kwenye halmashauri zote jijini Dar es salaam zote5 zimeshiriki. ametoa rai kwa washiriki kutumia mafunzo aya katika kutunza nakuboresha mazingira na kusimamia sheria ya mazingira kwa uweredi zaidi


habari picha na  ALLY THABITI

YANGA YAWAPOKONYA TONGE MDOMONI SIMBA

Mashabiki wa Yanga  wakishangilia baada ya CHIRWA  kusawazisha gori kwenye timu ya simba katika uwanja wa uhuru

habari picha na  ALLY THABITI

TIMU YA SIMBA YAJIMWAYA MWAYA

Pichani mashabiki wa timu ya simba wakishangilia goli lililofungwa dhidi ya Yanga  na KICHUYA katika  uwanja wa uhuru

habari picha na ALLY THABITI 

TFS NI SHIDA NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbarari  KIVUMA HAMISI MSANGI  amesema TFS ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu katika halmashauri .ivyo ameiomba serikali ifute TFS

habari picha na  ALLY THABITI

STENDI NI KIKWAZO CHA KODI MJINI MOSHI

Mbunge wa Moshi mjini JAFARI MAIKO   ameiomba serikali iwatengenezee stendi kubwa ya mabasi ya Moshi mjini  ili waweze kukusanya kodi nyingi kwaajili ya kuendeleza miradi mbalimbali. Pia ameitaka serikali inapotunga sheria iwashilikishe wadau mbalimbali lengo ziwe rafiki na zitekelezeke

habari picha na ALLY THABITI

WAZIRI JAFU ATOA MAAGIZO MAZITO

Waziri wa serikali za mitaa[TAMISEMI]  amewaagiza wakurugenzi,mameya na wenyeviti wa halmashauri kutumia vizuri fedha zilizotolewa na serikali kwaajili ya maendeleo . pia amewataka kusimamia vifaa tiba na dawa zinazosambazwa kwenye halmashauri hapa nchini . amesema aya kwenye mkutano mkuu wa 33 wa ALAT

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

Monday 30 October 2017

MKURUGENZI WA BARAZA LA SANAA AMSHITAKIA WAZIRI

Mkurugenzi mtendaji wa baraza la sanaa nchini Tanzania [BASATA] MARTINI KAYANDA  amemwambia waziri MWAKIEMBE  kuwa wasanii wanatapeliwa kwa kiasi kikubwa na kusababisha maisha yao kuwa duni . na badala yake wanaonufaika na kazi zao ni matapeli

habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI WASANII NGURI WAMEUDHURIA MKUTANO WA BASATA NA WAZIRI MWAKIEMBE

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

BASATA YAKATA NGEBE ZA WASANII

Baraza la sanaa nchini Tanzania[BASATA] limeamuwa kuwakutanisha wasanii na waziri MWAKIEMBE lengo waeleze changamoto zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi au majawabu ya kutosha na kuwafungulia mirango wasanii kwa waziri MWAKIEMBE . haya yamesemwa na afisa habari wa Basata

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

MSANII WA SANAA ATOA NENO ZITO

Msanii WILISONI WISO  ameitaka jamii ya kitanzania kuenzi sanaa za michoro kwani inatija kubwa kwa jamii na Taifa kwa kukuza pato la kifedha. Pia ameiomba serikali iwatumie wasanii wa michoro katika kutengeneza viwanda kwani viwanda vya michoro vinalipa

habari picha na  ALLY THABITI

MSANII NGURI AMWAGA MACHOZI MBELE YA WAZIRI

Mzee JANGARA  ni msani nguri amemuomba waziri wa sanaa,michezo ,habari na utamaduni  waziri  MWAKIEMBE awaboreshee maslai na awatengenezee mazingira ya kupata staiki zao kwa kazi walizofanya  miaka ya zamani. amesema haya kwenye jukwaa la sanaa lililoandaliwa na Basata ambako waziri MWAKIEMBE mgeni rasmi uwanja wa Taifa  wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam

habari picha na  ALLY THABITI

MISITU HATARINI KUTOWEKA NA KUANGAMIA

Mkurugenzi tendaji wa shirika la misitu barani Afrika GODIWINI KOWERO  amesema kutokana na mafunzo yanayotolewa vyuoni barani Afrika  kuna hatari kubwa ya kuangamia kwa misitu .Ivyo wameamuwa kuja na mitaara mipya ya kufundisha mavyuoni lengo kunusuru misitu ya bara la Afrika

habari picha na  ALLY THABITI

UTUNZAJI WA MISITU KUNUSURU KILIMO

 Dokta WILISONI KASORO  amesema tukizuia ukataji wa miti ovyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuto momonyoka kwa ardhi .ivyo kutawezesha kuwepo kwa ardhi yenye rutuba na kupatikana kwa mvuwa za uakika na atimaye kutakuwepo na mavuno ya kutosha

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

KAMPUNI YA VODACOM YAJA KIVINGINE

Moja ya viongozi wa Vodacom amesema kampuni yao ya Vodacom imeweza kufanya vizuri katika soko la isa. Pia wameweza kuchagua viongozi huru akiwemo mama  MAGRETI KONGO na mwanamke mmoja kutoka Kenya na Afrika kusini. pia amewapongeza wanaisa  kujitokeza kwa wingi nkwenye mkutano wao mkuu wa isa .kwani hii ni chachu ya mafanikio na maendeleo makubwa ya kampuni yao ya  Vodacom . na inaonyesha wanakubalika kwa kiasi kikubwa na kuaminiwa

habari picha na ALLY THABITI

WATANZANIA KUJAZWA MATIRIONI YA PESA

Mwenyekiti wa kampuni ya Vodacom ALLY MAFURUKI amesema kiasi cha shilingi Tirioni 26 watawapa watanzania kwa njia ya gawio .Lengo kuwafuta jasho wanaisa wa Vodacom na watumiaji wa Vodacom amesema haya kwenye mkutano mkuu wa wanaisa ambao umefanyika wilaya ya Temeke kwenye uwanja wa mpira wa Taifa jijini Dar es salaam


habari picha na ALLY THABITI

WANAWAKE WAPIGWA JEKI KIUCHUMI

Muadhiri mwandamizi kutoka taasisi ya sayansi ya bahari NARRIMAN JIDDAWI  amesema wanasaidia wanawake kwa kiasi kikubwa katika kujikwamuwa kiuchumi kwa kuwafundisha wanawake jinsi ya kutumia mikoko,matumbawe,pomboo,na kulima lulu kwa kuwauzia watalii ili wajikwamuwe kiuchumi.

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

TANZANIA YA VIWANDA KUNASULIWA NA TAFITI

Mwenyekiti wa maandalizi wa mkutano wa wanajumuiya wa wanasansi Prof YUNUSI MGAYA  amesema mkutano huu wa 10 ambao umejumuisha wanajumuiya wa kisansi utajadili tafiti mbalimbali zilizofanyika katika bahari ya Indi. ambako utasaidia kwa kiasi kikubwa  Tanzania kufikia Tanzania ya viwanda . Kwani tafiti za gesi zitasaidia kuendesha viwanda vyetu na tafiti za samaki zitasaidia kuanzishwa kwa viwanda vya kuchakata samaki hapa nchini . amesema haya kwenye  ukumbi wa mikutano ya kimataifa mwalimu Nyerere posta jijini  Dar es salaam

habari picha na VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MBUNGE WA VITI MAALUM MBONI MLITA WA ANDENI VIJIJINI AKITOA ZAWADI KWA SHULE ZILIZO FANYA VIZUR


SERIKALI KUWAONDOWA VIJANA KWENYE WIMBI LA UMASIKINI

Mbunge wa viti maalum Andeni vijijini  MBONI MLITA  amesema serikali imeamuwa kurasimisha shuuri ambazo sio rasmi kuwa rasmi .Lengo vijana wajiajili na kuwaajili wenzao ili wajikwamue na wimbi la umasikini .amesema haya wilaya ya Temeke viwanja vya chuo cha Duce jijini Dar es salaam

habari picha na  ALLY THABITI

TAASISI ZAJA KUWAKOMBOWA VIJANA

CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI ZAPATIWA UFUMBUZI

Mratibu wa miradi mashuleni NOERE MAODHI amesma wameamuwa kupeleka miradi kwa wanafunzi kwenye shule za secondary mbalimbali. Lengo kuwajengea uwezo wanafunzi ili kuvumbuwa vipaji vyao na kuviendeleza baada ya kumaliza elimu ya secondary. Pia kuwafanya wanafunzi wajitolee katika kwa kupitia vipaji vyao kazi hii imeanza mwezi wa tatu mwaka2017 na kumalizika mwezi wa kumi  .kwa kujumuisha shule 50 za secondary na shule 12 zimepata tuzo kati ya shule 50 .wakipata wazamini wa kutosha wataelekea mikoani Pia wameishukuru serikali  kwa kuwaluusu kupeleka miradi hii mashuleni

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WANAFUNZI WATIWA MOYO

Kijana  ANTONI  amewataka wanafunzi wa kitanzania wasikate tamaa  na badala yake wachangamkie fursa za miradi  zinazoletwa na taasisi mbalimbali .Ivyo watafanikiwa katika maisha yao katika kujiajili amesema haya kwenye viwanja vya chuo cha Duce wilaya ya Temeke wakati wa taasisi ya GREAT HOP walipotoa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri katika miradi waliopeleka kwenye shule izi .Mfano ufugaji wa kuku na utengenezaji wa sabuni pamoja na keki

habari picha na  ALLY THABITI

WANAFUNZI WAONYESHA UWEZO WAO

Mwanafunzi wa shule secondary ya Tambaza wa kidato cha tano TATU AMEDI  amesema wameonyesha uwezo mkubwa  katika kutoa elimu ya uzazi kwa wanafunzi wenzao. kupitia taasisi ya  GREAT HOP ivyo wamewasaidia wanafunzi wenzao kuepukana na mimba za utotoni pia ameipongeza taasisi hii kwa kuleta mradi huu

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

Monday 23 October 2017

WATU WA VIWANDA WATAKIWA KUUNDA KAMATI MADHUBUTI

Kiongozi kutoka osha amewataka watu wenye viwanda kuunda kamati za afya kwaajili ya wafanyakazi wao  ili iwasaidie pindi watakapo pata ajali kazini

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

SEKTA BINAFSI KUMUOKOA RAIS MAGUFULI

Kiongozi wa sekta binafsi JEMSI SIMBEYI amewataka wafanya biashara wa kitanzania kwenda na kasi ya rais MAGUFULI  ili wajenge viwanda vingi kwani wakifanya hivi watamsaidia rais MAGUFULI  kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati

habari picha na  ALLY THABITI

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA AKIJUMUIKA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA BODI YA UTALII

Habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

PICHANI MAKAMU WA RAIS

Makamu wa rais mama SAMIA SURUHU HASANI  akitoa zawadi kwa makampuni ya utalii na kuwataka wawe chachu ya maendeleo

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

ZANZIBAR YAWATOA OFU NA MASHAKA WATALII

Mkurugenzi wa bodi ya  utalii visiwani Zanzibar amewataka watalii watembelee kwenye vivutio vyao kwani ni vizuri na kuna usalama wa kutosha

habari picha na  ALLY THABITI

WATANZANIA WAASWA JUU YA UJENZI

Moja ya viongozi wa bodi ya usajili wa  wabunifu majengo na wakadiliaji majenzi amewataka watanzania wawatumie kwaajili ya ujenzi wa majengo yao

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

WAIGIZAJI WATAADHARISHWA

Mwanafunzi wa chuo cha sanaa Bagamoyo amewaonya waigizaji katika matumizi ya rugha na mavazi wanayo vaa kwani ayaendani na maadili ya kitanzania


habari picha na VICTORIA STANSLAUS

VIWANDA KUJA TANZANIA

Kiongozi wa kampuni ya vinyago amesema safari wanazoenda wafanya biashara wa kitanzania  nchini China zitaleta viwanda vingi

habari picha  na ALLY THABITI

CHADEMA YASEMA KATIBA MPYA NI KIZA KIZITO

Prof MWESIGA  kutoka CHADEMA  amesema swala la katiba mpya imekuwa nikiza kinene kwasababu rais  MAGUFULI  sio kipaumbele chake

habari picha na  ALLY THABITI

KATIBU MWENEZI WA CCM ASAMBAZA SUMU NZITO

Katibu mwenezi wa CCM AMFREY POLEPOLE  amewataka watanzania waachane na mawazo ya mchakato na ujio wa katiba mpya kwani sasa ni muda wa kuinyoosha nchi tu na badala yake watu wauishi ukatatiba

habari picha na ALLY THABITI

KATIBU MWENEZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO AIPIGA KIJEMBE CCM

Katibu mwenezi wa chama cha ACT WAZALENDO ADO SHAIBU  amekitaka chama cha mapinduzi CCM kiache kung'ang'ania katiba iyopo pia amemtaka rais  MAGUFULI  aendeleze mchakato wa katiba mpya

habari picha na ALLY THABITI

UCHUMI WA TANZANIA WAPAA KILELENI

Kiongozi kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania  amesema uchumi wa Tanzania kwasasa umekuwa kwa asilimia 4.3 ukilinganisha na kipindi kilichopita . vyakula vya nafaka,mkaa,gesi na vinywaji vimepanda  na kuwezesha kukua uchumi wa nchi

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

TAASISI YA UONGOZI YATOA DOZI NZITO KWA WAKURUGENZI NA MAMEYA

Mwezeshaji kutoka taasisi ya Uongozi ZAINABU MURO  akiwapa mafunzo wakurugenzi ,mameya pamoja na wenyeviti kuusu uongozi kwenye mkutano mkuu wa ALAT

habari picha na ALLY THABITI

WILAYA YA KILINDI KULETA MAAJABU

Mwenyekiti wa wilaya ya Kilindi mkoani Tanga  MUSSA MDOE  amewatoa ofu wakazi wake kwa kuwaambia kuwa watapata huduma bora za kiafya  kwani wanatengeneza ospitali bora na za kisasa . amesema haya kwenye mkutano mkuu wa ALAT jijini  Dar es salaam

habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI WAFANYA BIASHARA WA KITANZANIA

Hawa ndio wafanya biashara wa kitanzania walioenda China kwaajili ya mafunzo ya viwanda

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

ZITO KABWE ATOA MANENO MAZITO JUU YA BILIONI MIA 700

Kiongozi mkuu wa chama cha  ACT WAZALENDO  ZITO ZUBERY KABWE  ameionya serikali waache kuwadanganya watanzania kuusu kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barki.kwani akuna ukweli wa kulipwa bilioni mia700 pia amewaonya waandishi wa habari kuacha mara moja kusambaza taarifa za uongo kuusu kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barki . Pia amesema takwimu zinazotolewa na BOT pamoja na TRA  ni za kupikwa  kwani uchumi wa Tanzania unazidi kuporomoka siku adi siku

habari picha na ALLY THABITI

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAWAKOMBOA WAKULIMA WA ZANZIBAR

Chama cha ACT WAZALENDO  chasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima wa karafuu visiwani Zanzibar eneo la Pemba kulejeshewa mashamba yao 86 ya Karafuu ambayo alikuwa yameshikiliwa na waziri wa kilimo wa Zanziber  HAMADI RASHIDI 

habari picha na  ALLY THABITI

PICHANI VIONGOZI WENYE MABENKI WAKIWA NA TUSE JUMBE


MABENKI YATAKIWA KUCHANGAMKIA WA KABAMBE

Mkurugenzi wa chama cha wenye mabenki Tanzania  TUSE JUMBE  amewataka wenye mabenki watumie mfumo wa kusoma kwa kutumia mtandao wa simu au komputer kwani unafaida ya kutunza mda,gharama,na kusoma kwa uhuru.Pia amewataka wafanyakazi wa kwenye mabenki kusoma na kujifunza kwa kutumia mitandao. Lengo la kuleta mfumo huu wenye mabenki wawe na wafanyakazi wengi wenye ujuzi mkubwa

habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

BASATA YATEMA CHECHE KWA WASANII

Mkurugenzi wa baraza la sanaa nchini Tanzania amewataka wasanii kutunga na kuimba nyimbo zenye maadili


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AIPA TANO UN

Naibu waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania  ameipongeza UN kwa kuleta maendeleo nchini Tanzania na kupeleka miradi mikubwa mkoani Kigoma . serikali ya Tanzania imewaakikishia ushirikiano mwema

habari picha na ALLY THABITI

UN YAJA KIVINGINE MIAKA 72

Mwakirishi mkazi wa UN nchini Tanzania  amesema miaka 72 watakayo azimisha tarehe 24 mwezi 10 mwaka 2017 wanajivunia kwa kuleta mafanikio makubwa kwenye jamii ya kitanzania kwa kukuza uchumi, kuboresha afya,miundombinu na elimu. Ivyo amewaaidi watanzania watashirikiana nao bega kwa bega.Lengo kuleta mabadiliko zaidi


habari picha na  VICTORIA STANSLAUS