Thursday 30 November 2023

AFRICAN CONTEXT OF WOMEN'S LAND RIGHTS

 


WIZARA YA ARDHI YAIPONGEZA LIBERTY SPARKS

 Naibu katibu mkuu wa wizara ya Ardhi, nyumba maendeleo na makazi Dr. Pendo Makokolo amesema Liberty Sparks utafiti walioufanya ni mzuri kwani serikali itatumia report hii walioizindua kwaajili ya kuboresha sera, sheria, kanuni na taratibu ambazo zinamnyima mwanamke haki ya kumiliki ardhi.

Dr. Pendo amepongeza kwa kusema kuwa watafanya maboresho na kwenye mabaraza ya ardhi lengo kuweza kuweka mifumo thabit ili mwanamke aondokane na manyanyaso na matesho anapodai haki ya kumiliki ardhi.

Habari kamili na Ally Thabit

MWENYEKITI WA BODI WA LIBERTY SPARKS

 Mwenyekit i wa Liberty Sparks ni vyema Serikali kuwapa elimu na uelewa wanawake waweze kumliki ardhi pia bunge litenge bajeti ya kutosha nakuweka mifumo rafiki kwenye mabaraza ya ardhi pamoja na mahakamaza. Yote haya yatafanyika migogoro ya Ardhi itapungua kwa kiasi kikubwa na wanawake watapa fursa yakuweza kumiliki ardhi

Mwenyekiti wa bodi wa taasisi ya LIBERTY SPAERK Dr Tumsifu amesema utafiti unaonesha kwenye ripoti yao asilimia 10% ya watanzania wanahati za Ardhi.

habari kamili na Ally Thabit

MKURUGENZI WA LIBERY SPARKS ATOA NENO JUU YA REPORT WALIOITOA

 Evans ni mkurugenzi wa Liberty Sparks amesema wamefanya utafiti na kugundua kuwa wanawake wanakosa haki ya kumiliki ardhi nchini Tanzania hii yote kutokana na mila na desturi dhidi ya wanawake pia sheria ya mwaka 1967 haimpi haki mwanamke kumiliki ardhi hivyo upitia utafiti yaiomba serikali kuweka mazingira wezeshi ili mwanamke kumiliki ardhi ambapo mwanamke huyu itamsaidia kwa kiasi kikubwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kulima na shughuli zinginezo.

habari kamili na Victoria Stanslaus 

LIBERTY SPARKS YAJA NA RIPOTI YA UMILIKI WA ARDHI KWA WANAWAKE

 Dr. Samwel ni mshauri na mtafiti wa taasisi Liberty Sparks amesema wameamua kufanya utafiti kwa namna wanawake wanavyopata changamoto kwenye kumiliki Ardhi nchini Tanzania ambako kwa vijijini imekuwa ni tatizo kubwa sana ndio maana wameamua kufanya utafiti huu lengo serikali iweze kubadili sela, sheria, kanuni na taratibu kandamizi dhidi ya wanawake katika kumiliki ardhi.

Habari kamili na Ally Thabith

UGANDA YAIPONGEZA TEMINATE KWA MKUTANO WA ELIMU

 Mwakirishi kutoka Uganda John Samwel amesema mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu nchini Tanzania utasaidia kwa kiasi kikubwa kukua kwa elimu Tanzania na Africa kiujumla.

Habari picha na Ally Thabith




TBA YAANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU DAR ES SALAAM

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Dar es Salaam umeanza zoezi la kuwaondoa wapangaji waliolimbikiza madeni ya kodi ya pango.


Akizungumza na wandishi wa habari Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema zoezi la kuwaondoa wapangaji hao linafata taratibu zote za kisheria.

"Utaratibu wa huu kuwandoa wadaiwa sugu wa kodi ya pango unaongozwa na dalali ya makahama ambaye ni Twins Auction Mart, kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wapangaji wetu kutolipa kodi ya pango na kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni wengi wakiamini kwa kuwa ni nyumba za Serikali hawawezi kutolewa licha ya kuwa na madeni hayo" amesema Mayemba

Pamoja na hatua wa kuwaondoa kwa nguvu kwenye nyumba hizo Mayemba amesema TBA imeazima kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wote lengo likiwa ni kuhakikisha wanalipa madeni yao yote.

"Wadaiwa hao wenye madeni makubwa, wameifanya TBA kushindwa kutekeleza mipango ya ukarabati wa nyumba zilizopo na kujenga nyumba mpya zitakazopangishwa au kuuzwa kwa watumishi wa umma na wananchi wanaokabiliwa na changamoto ya makazi" amesisitiza Mayemba.

Vile vile ameeleza juu ya maboresho yaliyofanywa na TBA kupitia mfumo mpya wa kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) ambapo mfumo huo utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kila mwezi kwa kiwango mfuto ( automatically) cha 20% mpaka deni litakapokamilika kulipwa.

Zoezi ya kuwaondoa wadaiwa sugu katika mkoa wa Dar es Salaam litadumu kwa muda wiki tatu ambapo litafanyika katika nyumba na majengo yote yanayosimamiwa na TBA

Tuesday 28 November 2023

MKURUGENZI WA TAMWA AINISHA MIKAKATI MIZITO

 Mkurugenzi wa TAMWA Dr Rose Rubein Amesema baada ya uzinduzi wa report TAMWA inamipango yakutoa elimu kwa wamiliki na wakurugenzi wa vyombo vya habari pamoja na  mameneja lengo kuondoa maswala ya ukatili dhidi ya wanahabari wanawake kwenye vyombo hivyo pia TAMWA inawataka wanahabari wanawake kupaza sauti na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa.




Habari picha na Ally Thabit

NAIBU WAZIRI WA HABARI NA TEKNOLOGIA ATOA NENO KWA TAMWA

 Naibu waziri wa habari na teknolojia amesema TAMWA iongeze kasi kubwa katika kupambania kundoa ukatili  vya habari kwa wanawake ambako ripoti waliotoa tamwa inaonesha asilimia 64% ya wanahabari ya wanaume wamepewa mikataba kwenye vyombo vya habari na wanawake asilimia 36% wamepewa mikataba huku asilimia 74% ya wanahabar wanawake wanafanyiwa ukatili wa kinondo kwenye vyombo vya habari.

anaipongeza tamwa kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwepo kushiriki kwenye mabadiliko ya sera, sheria, kanuni na taratibu na kuishauri serikali ya Tanzania ameitaka kuongeza idadi ya wanachama wao ambako kwa kipindi ambacho wanatimia miaka 36 wana wanachama 250.


Habari picha na Ally Thabith

MTANDAO WAELIMU WAPONGEZWA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE

Raisi mstaafu wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete amepongeza mtandao wa elimu Tanzania kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kukuza elimu nchini naye kwa upande wake katibu mkuu wa wizara ya elimu Dr Charles Msonde amesema inashirikiana na mtandao wa elimu katika kuboresha miundo mbinu na kuwa jengea uzoefu walimu, naye mwenyekiti wa mtandao wa elimu Tanzania nae Dr Faraja Nyarandu amesema wameamua kuumpa tuzo Raisi Mstaafu Dr Jakaya Kikwete kwakuweza kukuza sekta ya elimu wakati akiwa Raisi na baada ya kustaafu nae mkurugenzi mtandao wa elimu amesema wanagusa makundi yote wakiwemo wenye ulemavu kwenye sekta ya elimu mfano ujenzi wa vyoo kutoa vifaa vya kujifundishia kwa wasioona.

Haya yote yamesemwa tarehe 27.11.2023 wakati wa ufunguzi wakongamano linalohusu maswala ya elimu ambako nchi saa zimeshiriki chini ya waaandaaji mndao wa elimu Tanzania.

Habari kamili na Ally Thabit

Thursday 23 November 2023

IIDADI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU MITIHANI YA DARASA LASABA YAONGEZEKA

Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Dkt. Said A. Mohamed amesema kiwango cha ufanyaji mitihani kwa watu wenye ulemavu wa darasa la saba imeongezeka kupita wanafunzi 4583 kwa 2023 ambako kwa mwaka jana walikuwa 4221 pia amesema ufahuru wao umeongezeka kwa kiasi kikubwa hii yote ni kwaajili ya juhudi na jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kujenga miundo mbinu rafiki na bora pamoja na vifaa kwa wanafunzi wenye uhitaji maarumu.

Ametoa wito kwa jamii kutowafungia ndani watu wenye uremavu wawapeleke shule ili wapate elimu.

Habari na Ally Thabiti

THRDC YAAZIMISHA MIAKA 75

Mratibu wa THRDC Onesmo Eli Ngurumo amesema wataendelea kufanya kazi ya kuwatetea watetezi wa haki za binaadamu katika maadhimisho ya miaka 75 wameamua kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanachuo kwa ajili ya kuweka nguvu katika kueondoa maswala ya ukatili wa kijinsia katika Tanzania. Nae kwa upande wake mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku amewataka wanaharakati kurudi nyuma katika kupaza sauti zidi wanaowakandamiza watu.

Habari na Victoria Stanslaus

MCHUANO MKALI WASICHANA NA WAVURANA MATOKEO YA DARASA LA SABA


 

Wednesday 22 November 2023

BRELA YAKABIZI VIFAA VYA MICHEZO KWA CHANETA



 Habari na Ally Thabiti

WAKALA WA MAJENGO KUKUSANYA BILIONI 7.8

Mtendaji Mkuu  Daudi Kandolo wa Wakala wa Majengo Tanzania amesema tarehe 01/12/2023 watakusanya madeni kwa watumishi wanaoishi kwenye nyumba za wakala wa majengo ambao wanao daiwa kodi amesema kupitia kampuni ya Dalali ambako imepata mmlaka ya mahakama itakusanya madeni kwa watumishi wote ambao wamepanga na wanao daiwa kodi kwenye nyumba za TBA Tanzania nzima watakao shindwa kulipa watafukuzwa kwenye nyumba hizo na watapelekwa mahakamani ili waweze kulipa mikoa inayoongozwa kwa kudaiwa kodi na TBA Dodoma, Arusha na Mbeya.

Mtendaji Mkuu Daud Kandolo wa TBA amewataka wapangaji wote kutoa ushilikiano na zoezi hili litakuwa ndani ya mwezi mmoja ambako kiasi cha Bilioni 7.8 zitakusanywa na ile mikoa kinara inayodaiwa kodi Dodoma, Arusha na Mbeya itakusanywa Bilioni 1.4.

Habari na Ally Thabiti

MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE UMIELEZA MAFANIKIO

Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa mfuko wa sawa kwa wote Justina wameweza kuwapa elimu wasichana 954 kwa kuwapa mafunzo ya tehama pia wameweza kutoa vifaa vya tehama kwa shule mbalimbali ikiwemo na shule za watu wenye ulemavu. mfuko wa mawasiliano sawa kwa wote imeweza kujenga minara 758 kwa Zanzibar wameshajenga minara 42 huku wakijenga miundo mbinu kwenye hospitali kwa ajili ya tiba mtandao, amesema lengo ni kujenga minara Tanzania nzima ambako mnara mmoja unajengwa kwa kiasi cha Milioni 350.

Habari na Ally Thabiti

Wednesday 15 November 2023

RAISI WA ZANZIBAR AMEZITAKA NCHI ZA KIAFRIKA KUWEKA NGUVU KWA WANAWAKE

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi amewataka mawaziri wa fedha wa afrika kuweza kuwawezesha wanawake fedha ili waweze kujikwamua kiuchumi

Pia amewataka mawaziri wa Afrika wa wizara ya maendeleo ya jamii kuwatafutia wanawake fursa za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi waondokane na maswala ya ukatili wa kijinsia huku wakizitaka nchi hizo kupitia kwenye mabunge yao kutenga bajeti wenye usawa wa kijinsia na kuweka sera bora kwaajili ya wanawake naye waziri wa Mwigulu Mchemba amesema kupitia mkutano huu Tanzania itajifunza namna ya kuwainua wanawake kiuchumi pia nitahamasisha nchi nyingine zitenge bajeti zenye usawa wa kijinsia kama ilivyo Tanzania kwaupande wake waziri wa maendeleo ya jamii Dr. Doris Gwajima amempongeza Rais Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwainua wanawake kiuchumi, watu wenye ulemavu vijana, wazee na makundi mengineyo na kwakuweza kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia na kuwepo kwa sera na sheria rafiki kwa wanawake na makundi mengineyo.

habari kamili na Ally Thabit

ANNA KIPYA AIPONGEZA TGNP

Mwanaharakati Anna Kipya amesema TGNP imefanya kazi katika kuleta uchechemuzi wa mabadiriko ya usawa wa kijinsia mpaka ukatiri umepungua Tanzania.

Habari kamili na Ally Thabith

WALIOKUMBWA NA MAFURIKO KUJAZWA MAPESA

 Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengelo amesema wakazi wanaoishi mbonde mto msimbazi, jangwani na magomeni mtaa wa sunaa watapewa kiasi cha milioni nne ikiwa ni fidia kwaajili ya kupisha mradi wa bonde la mto msimbazi.


habari kamili na Ally Thabith

Tuesday 14 November 2023

TGNP YATOA MAAZIMIO KWENYE TAMASHA LA 15

Mwenyekiti wa Bodi TGNP kushirikiana na ASAS za kiraia waitaka serikali kuweza kulejesha mchakato wa katiba mpya, kutenga bajeti yenye mlengo wa kijinsia kutoa sheria za ndoa za utotoni aya yametolewa kwenye kilele la tamasha la kinsia mabibo jijini Dar es Salaam 10/11/2023.

Habari na Ally Thabiti

DR VARELIA MILINGA PROGRAM MENEJA WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA AMEWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUPIMA AFYA ZAO

Program Maneja wa Magonjwa yasiyoambukiza wa wizara ya Afya Dr. Varelia Milinga amewataka watu kujitokeza kwa wingi vinjwa vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupima afya zao bure na kupewa matibabu pamoja na elimu namna ya kukabiliana na magonjwa yasio ambukiza kwa upande wao NHIF wamesema magonjwa yasiombukiza yanatumia fedha nyingi sana katika matibabu kwa mwaka 2021 - 2022 kiasi cha fedha ya Kitanzania Bilioni 32.4 zimetumika kutibu magonjwa ya Kansa ukilinganisha na nyuma kiasi kilikuwa kidogo, kwa upande wa magonjwa ya fido zimetumika Bilioni 35.4 ukilinganisha na miaka ya nyuma NHIF wametoa witoa wito kwa jamii wajiunge na bima za afya.

Habari na Ally Thabiti

MAWAZIRI 22 KUTOKA NJE YA NCHI KUJADILI USAWA WA KIJINSIA TANZANIA

Waziri wa Maendeleo ya jamii Doris Gwajima amesema tarehe 15 - 17 /11/2023 mawaziri 22 kutoka nchi za Rwanda, Zambia, Uganda na zinginezo wanakutana jiji Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili maswala ya usawa kijinsia pamoja na kuweka mikakati ya uwekezaji katika maswala ya kijinsia, nae Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba amesema kwenye mkutano huu mawaziri wa fedha watajadili namna gani ya kutenga bajeti zenye usawa wa kijinsia kwenye nchi zao.

Habari Ally Thabiti

MEA WA DAR ES SALAAM AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA KUPIMA MAGONJWA YASIOAMBUKIZA

 


Omary Kumbilamoto Mstahiki mea wa Jiji la Dar es Salaam amewataka wananchi wote wa Dar es Salaam na mikoa jirani wajitokeze kwa wingi kupima afya zao na kupata huduma bure kwa magonjwa yasioambukiza viwanja vya mnazi mmoja kuanzia tarehe 14/11/2023 mwisho tarehe 18/11/2023 pia kutakuwepo na utoaji wa elimu wanamna kukabiliano na magonjwa yasiyoambukiza mfano kansa, Figo, Kisukali, Presha na mengineyo.

Omary Kumbilamoto ameshukulu wizala ya afya kwa kutoa huduma hii bure kwani wataokoa maisha ya watu wengi pia amemshukuru mweshimiwa Rais Dr. Samia Saluhu Hassan kwa kuweka kutoa vifaa tiba kwa wizara ya afya.

Habari picha na Ally Thabiti 

Wednesday 8 November 2023

MAKAMO WA RAIS WA AFRIKA KUSINI AIPONGEZA TGNP MTANDAO

 Aliyekuwa Makamo wa Rais nchini Afrika Kusini mwaka 2005 na mkurugenzi mkuu wa UN Woman mstaafu Bi. Phumzile Mlamdongeuka amesema TGNP Mtandao katika kuhazimisha miaka 30 tangu iazishwe mwaka 1993 imeweza kuwakomboa wanawake zidi ya ukatili wa kijinsia pia imewezeshe mabadiliko ya sera, sheria na miongozo iliyokuwa kandamizi nchini Tanzania zidi ya wanawake kufutwa pia imewajengea uwezo wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwa viongozi nchini Tanzania pia ameutaka uwongozi wa TGNP Mtandao nchini Tanzania kwenye tamasha lao la 15 liendelee kupaza sauti zidi ya mila na destuli potofu na kandamizi kwa wanawake.

kwa upandewake mkurugenzi mkuu mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amesema wameweza kupaza sauti ya pamoja katika kupinga ubaguzi, ukatili, na unyanyaswaji wanawake nchini Tanzania, tamasha la TGNP Mtandao limeweza kuwafikia watu elfu 35 Tanzania nzima na watu elfu 7 kwenye wilaya 32, kwenye kanda zote sita watu 1500 wamefikiwa kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa TGNP Mtandao gema akilimali amewataka watanzania na wasio watanzania kuweka nguvu za pamoja katika kumkomboa mwanamke nae mkurugenzi mkuu mtandaji wa Woman Found Bi. Rose Malando ametaka asasi mbalimbali kuweza kutumia na kuzitafuta fedha kwa ajili ya kuweza kumkomboa mwanamke kielimu, afya, ardhi na maji. Ambako kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano nukta sita ziliweza kutolewa kwaajili ya kufanya harakati ya kumkomboa mwanamke.

Habari na Ally Thabiti

TRA KUTOA TUZO KWA WALIPA KODI

Mkurugenzi Mkuu wa Elimu kwa Uma na mawasiliano TRA Richard Kayombo amesema tarehe 24/11/2023 watatoa tuzo kwa walipa kodi nchini Tanzania mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu Dr. Dotto Biteko tuzo hizi zitatolewa Mlimani City lengo la kutoa tuzo hizi ni kuwamasisha watu kulipa kodi kwa hiari. Kauli mbiu inasema Kodi kwa maendeleo tuwajibike, Richard Kayombo amesema tarehe 09/11/2023 jumla ya shule hamsini na tisa (59) zitafanya mjadala kuhusu maswala ya kodi kwenye chuo cha kodi lengo la kuwashilikisha wanafunzi kuwajengea uwezo na uwelewa ili wawe walipakodi wazuri baadae, Tarehe 18/11/2023 kutakuwa na mbio za kilometa 5 na 10 ambako zitafanyika katika viwanja vya Jimkana bule.

TRA imetoa wito kwa wadau wote kushiriki kwenye mbio hizi

habari na:  Ally Thabiti