Wednesday, 8 November 2023

MAKAMO WA RAIS WA AFRIKA KUSINI AIPONGEZA TGNP MTANDAO

 Aliyekuwa Makamo wa Rais nchini Afrika Kusini mwaka 2005 na mkurugenzi mkuu wa UN Woman mstaafu Bi. Phumzile Mlamdongeuka amesema TGNP Mtandao katika kuhazimisha miaka 30 tangu iazishwe mwaka 1993 imeweza kuwakomboa wanawake zidi ya ukatili wa kijinsia pia imewezeshe mabadiliko ya sera, sheria na miongozo iliyokuwa kandamizi nchini Tanzania zidi ya wanawake kufutwa pia imewajengea uwezo wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwa viongozi nchini Tanzania pia ameutaka uwongozi wa TGNP Mtandao nchini Tanzania kwenye tamasha lao la 15 liendelee kupaza sauti zidi ya mila na destuli potofu na kandamizi kwa wanawake.

kwa upandewake mkurugenzi mkuu mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amesema wameweza kupaza sauti ya pamoja katika kupinga ubaguzi, ukatili, na unyanyaswaji wanawake nchini Tanzania, tamasha la TGNP Mtandao limeweza kuwafikia watu elfu 35 Tanzania nzima na watu elfu 7 kwenye wilaya 32, kwenye kanda zote sita watu 1500 wamefikiwa kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa TGNP Mtandao gema akilimali amewataka watanzania na wasio watanzania kuweka nguvu za pamoja katika kumkomboa mwanamke nae mkurugenzi mkuu mtandaji wa Woman Found Bi. Rose Malando ametaka asasi mbalimbali kuweza kutumia na kuzitafuta fedha kwa ajili ya kuweza kumkomboa mwanamke kielimu, afya, ardhi na maji. Ambako kiasi cha dola za kimarekani bilioni tano nukta sita ziliweza kutolewa kwaajili ya kufanya harakati ya kumkomboa mwanamke.

Habari na Ally Thabiti

No comments:

Post a Comment