Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Dar es Salaam umeanza zoezi la kuwaondoa wapangaji waliolimbikiza madeni ya kodi ya pango.
Akizungumza na wandishi wa habari Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Bernard Mayemba amesema zoezi la kuwaondoa wapangaji hao linafata taratibu zote za kisheria.
"Utaratibu wa huu kuwandoa wadaiwa sugu wa kodi ya pango unaongozwa na dalali ya makahama ambaye ni Twins Auction Mart, kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wapangaji wetu kutolipa kodi ya pango na kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni wengi wakiamini kwa kuwa ni nyumba za Serikali hawawezi kutolewa licha ya kuwa na madeni hayo" amesema Mayemba
Pamoja na hatua wa kuwaondoa kwa nguvu kwenye nyumba hizo Mayemba amesema TBA imeazima kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wote lengo likiwa ni kuhakikisha wanalipa madeni yao yote.
"Wadaiwa hao wenye madeni makubwa, wameifanya TBA kushindwa kutekeleza mipango ya ukarabati wa nyumba zilizopo na kujenga nyumba mpya zitakazopangishwa au kuuzwa kwa watumishi wa umma na wananchi wanaokabiliwa na changamoto ya makazi" amesisitiza Mayemba.
Vile vile ameeleza juu ya maboresho yaliyofanywa na TBA kupitia mfumo mpya wa kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) ambapo mfumo huo utakuwa unatoza riba ya 20% kwa mpangaji atakae kaa zaidi ya miezi 3 bila kulipa kodi ya pango. Riba hiyo itaendelea kila mwezi kwa kiwango mfuto ( automatically) cha 20% mpaka deni litakapokamilika kulipwa.
Zoezi ya kuwaondoa wadaiwa sugu katika mkoa wa Dar es Salaam litadumu kwa muda wiki tatu ambapo litafanyika katika nyumba na majengo yote yanayosimamiwa na TBA
No comments:
Post a Comment