Tuesday 9 January 2018

MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI AKABIDHIWA OFISI

Edwin mndolwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya  ya Wazazi Ccm ameahidi kulinda na kuzisimamia mali zote  za Jumuiya  za Wazazi ccm
Amesema hayo  kwenye makao  makuu ya Jumuiya ya Wazazi ccm Jijini Dar es salaam

Habari picha Na Ally Thabiti

KITUO CHA MSAADA WA KISHERIA CHA LAANI VIKALI ADHABU ILIYOTOLEWA NA TCRA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi mtendaji wakituo cha msaada  wa Kisheria LHRC bi Hellen Kijobisimba amesema wanalaani  vikali kitendo cha mamlka  ya  mawasiliano Tanzania kuvipiga  faini vyombo vitano vya  Habari ikiwemo Azam, star tv, channel ten, East AFrica na  ITV kwakutoa  taarifa  ya  tathmini ya  uchaguzi mdogo wa madiwani wa mwaka 2017  ambapo taarifa  hizo zilitolewa na  kituo hicho  hivyo ameitaka  TCRA kufuta adhabu hizo mara moja ambapo jumla ya Milioni Sitini zinatakiwa kulipwa na Vituo hivyo

Aidha bi Hellen ametoa wito kwa  wadau mbali mbali kuchangia  mfuko ambao utasidia kulipa faini  ambao utakuwa unasaidi vyombo vya Hbari Vinavyopigwa Faini

Habari Picha na Ally Thabiti

MAMLAKA YA MAPATO YA WATAKA WATANZANIA KULIPA KODI ZA MAJENGO

Mkurugenzi  wa huduma na  elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA  Richard Kayombo amewatatka  watanzania waanze kulipa kodi za majengo kuanzia sasa ili kuepusha  usumbufu kama uliotokea  mwaka jana,

 Amesema  hayo  wakati  wakutoa  taarifa za makusanyo na  mapato kwa mwaka 2017 kuanzia tarehe 1 mwezi 6 had mwenzi wa 12 ambapo  ni trilioni 7.87 ikilinganishwa  na sh trilioni 7.27 ambazo  zilikusanywa kipindi kama hicho katika  mwaka wa  fedha wa 2016/17  ambapo ni sawa  na  ukuaji wa asilimia 17.65

hata hivyo katika  mwezi wa Desember pekee  TRA ilikusanya jumla ya shilingi trilioni 1.66

aidha  bwana  Kayombo amewapongeza  wafanyabiashara wenye makampuni na wananchi  kwakulipa kodi  pia amewataka wananchi wadai risiti na  wafanyabiashara watoe Risit wanapouza  bidhaa zao.

Habari Picha Na Victoria Stanslaus