Wednesday 18 October 2023

PICHANI WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI PAMOJA NA WANAHABARI WAKIWA KWENYE SEMINA ILIYOANDALIWA NA BENKI YA TIB


 Habari picha na Ally Thabiti

BENKI YA TIB YAELEZA FAIDA ZA UWEKEZAJI


 Kaimu mkurugenzi mkuu mtendaji wa Benki ya TIB, Lilian Mbassya amesema benki yao imeweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya nishati ambako imetoa pesa kwa TANESCO kwaajili ya umeme vijijini pamoja na umeme wa jua pia imewezesha TPDC katika sekta ya Gesi na Mafuta kwa kutoa kiwango kikubwa cha pesa imewezesha mamlaka ya maji hapa nchini kwa ajili ya kusimamia miradi ya maji miradi hiyo ikamilika wananchi watapata maji safi na salama zaidi ya laki tano (500,000) pia imewezesha ukuwaji wa kilimo ambako benki ya TIB imetoa matrekta mia mbili arobaini na tisa 249 pamoja na power tila kwa wakulima huku wakitoa mikopo kwenye sekta ya kilimo isiyokuwa na liba asilimia nne mpaka tano. 

Kaimu mtendaji mkuu wa benki ya TIB ametoa wito kwa wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari kuitangaza vyema benki ya TIB kwani inawezesha katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania mfano wakulima elfu kumi wamepata ajila kupitia benki ya TIB amesema haya wakatika akizungumza na wanahabari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Habari picha na Ally Thabiti

DART YATOA TAARIFA YA MABORESHO STENDI YA KIVUKONI

Mr. William Batambi mkuu wa kitengo idara ya mawasiliano na mahusiano kwa huma DART amesema ifikapo tarehe 20/10/2023 Dala Dala zinazoenda feri eneo la kivukoni azitoruhusiwa kufika eneo hilo ila mabasi yaendayo haraka ndiyo yatakayo ruhusiwa tu pamoja na bajaji maelekezo haya yametolewa kwa sababu kuna maboresho ya kituo cha mabasi yaendayo haraka kwa ajiri ya hawamu ya pili ya mladi ya mabasi ya Mbagala, awamu ya tatu mabasi ya Gongo la mboto, awamu ya nne mabasi ya Tegeta.

Habari picha na Ally Thabiti


 

Sunday 15 October 2023


 
TIBA SHUFAA YAWA MKOMBOZI KWA WAGONJWA  .Mkurungezi mkuu mtendaji wa Hospital ya Ocean Road , Dr Julius Mwasarage amesema Tiba shufaa inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutibu magonjwa mbali mbali , yakiwemo Magonjwa ya Saratani , kisukali , Magonjwa ya Moyo na Magonjwa mengineyo . Tiba shufaa ni matibabu ambayo yanatolewa kwa kushirikiana na Timu ya Madkatari , viongozi wa Dini pamoja na Jamii ,nchini Tanzania Hospital zipatazo 40 , zinatoa huduma za tiba shufaa huku hospital za kanda zinatoa Tiba shufaa  kwa Tanzania ziko Hospital 7.

Dr ameitaka jamii kuzingatia matibabu ya tiba Shufaapia ameeleza Magonjwa pia amesema seratani ya shingo ya kizazi ndio inaongoza kwa wanawake kwa asilimia 95 saratani ya matiti 15 , saratani ya Ngozi asilimia 10, watu wajitokeze kupata tiba shufaa  Dr julius ameongeza na kusema anampongeza sana Mh Rais Dr Samia Suruhu Hassani kwa kuweza kuweka fedha nyingi kwenye sekta ya Afya .

Ametoa wito kwa jamii kuweza kupima Afya zao mara kwa mara pia wawe na Bima za Afyan kwani matibabu ni Gharama mno.

Tiba Shufaa  iliaza kuazimishwa 2005 kila ifikapo mwezi wa kumi wiki mbili za mwazo , Dunia uwazimisha huduma za tiba shufaa., kwa tanzania imeazimishwa 14/10/2023  Hospital ya Ocean road.

Habari Picha na Ally Thabiti.

 NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstan Kitandula ameutaka uongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuwa na mikakati ya kusambaza miche ya miti ya matunda katika maeneo ya shule za Msingi na Sekondari nchini.


Kitandula aliyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea shamba la miti Longuza na Hifadhi ya Msitu wa Asili Amani wilayani Muheza Mkoani Tanga ambapo aliutaka pia wakala huo kuanzisha vitalu vya malihai kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ili watoto na vijana wajifunze umuhimu wa uhifadhi wa maliasili za misitu nchini.

Aidha pia Kitandula ameutaka uongozi wa shamba la miti Longuza kuweka mkakati wa kusambaza zao jipya la miti inayozalisha zao la mpira kwa vijiji ambavyo vinazunguka eneo la shamba hilo kwa kuwapa elimu wananchi wajiunge kwenye kilimo cha miti hiyo.

Vilevile Mhe Kitandula ameitaka TFS kuboresha hostel na kuongeza vitanda kwa ajili ya watalii ambao wanahitaji kulala kwenye hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani ili kuunga juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma katika sekta ya utalii.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa shamba la miti Longuza na Hifadhi ya Msitu wa Asili Amani kuwaandaa wananchi na mkutano wa wadau wa mazao ya Nyuki utakaofanyika mwaka 2027 Jijini Arusha.

“Fursa za mazao yatokanayo na nyuki sio asali na Nta peke yake badala yake wafundisheni wananchi mazao mengine yanayotokana na ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kunyanya kipato chao”Alisema

Awali akimkaribisha Naibu Waziri,Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhe Juma Irando alimueleza kwamva moja ya changamoto inayowasumbua ni wananchi kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji ambavyo vipi katika Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani kwa ajili ya shughuli za kilimo pamoja na uchumbaji madini.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa rai kwa Wakala huo wa Huduma za Misitu kuendelea kutoa elimu kwa zaidi ya uhifadhi katika msitu wa Amani ambayo ndio chanzo kikuu cha Maji yanayotumika Tanga na mji wa Muheza.

 Wizara ya Ardhi Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inahakikisha inatatua kero ya migogoro ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam inamalizika katika kipindi kifupi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mkoani Dar es salaam Jerry Slaa ambaye aliitwa jijini humo na Kamati Tendaji ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dar es Salaam.

Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na wataalamu wa ardhi kutoka halamshauri za Mkoa huo,kwa lengo la kujadili namna ya kuondoa tatizo la kero za urasmishaji wa ardhi zinazofanywa na baadhi ya makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha kutoka kwa wananchi huku yakishindwa kutekeleza majukumu yake.

"Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kushughukia kero ya Urasmishaji wa ardhi inayowakumba wananchi wa Mkoa huo,"amesema Slaa.

Amsema Serikali imepanga kupima na kutoa hati za ardhi milioni mbili na laki tano(2.5 milioni) kufikia 2025,hivyo lengo la serikali ni kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kwa mikoa yote ishirini na sita(mikoa 26) nchini na kuna makamishna wa ardhi wanaotoa hati ,hatua hiyo inayosaidia wananchi kupata hati zao bila usumbufu.

Waziri Slaa ametoa muda wa siku saba kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatatua kero hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam nakwamba baada ya hapo warejeshe majibu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam.

"Maelekezo yangu ya utatuzi wa kero ya Urasmishaji ni kuwa ,Naibu katibu Mkuu na Watendaji wenzako mlete taarifa kwa viongozi wa chama,kama kuna tatizo la fedha niambie ili tuone tunapata wapi fedha ili muweze kukamilisha kazi hii" amesema Waziri Slaa.

Aidha Waziri Slaa amesisitiza kwamba hataki kuskia kero za urasmishaji wa ardhi zinaendelea kujitokeza katika uongozi wake ambapo amesisitiza makampuni yanayojihusisha na urasmishaji huo yanapaswa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na yale yatakayoenda kinyume yachukuliwe hatua za kisheria .

Ameongeza kusema kwamba "Urasmishaji umekua tatizo kubwa katika simu kumi anazopigiwa na wananchi simu saba hadi nane zinahusu malalamiko ya urasmishaji wa ardhi.

"Nimekuja na timu yangu inayohusika na mambo ya ardhi napenda kuagiza kuhakikisha kero hizi zinashughulikiwa haraka sana".

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu katika kikao hicho cha kamati tendaji cha CCM amesema kwamba Mkoa wa Dar es salaam umekua na tatizo la urasmishaji kutokana na kazi hizo kupewa makampuni binafsi ambayo yanakusanya fedha za wananchi nakutokomea nazo bila kufanya kazi hiyo kwa wakati.

Amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa waliona kumwita mheshimiwa Waziri wa Ardhi kuzungumzia tatizo hilo. 

Katika kikao hicho madiwani,wakuu wa wilaya na wataalamu wa ardha walifika tayari , kupokea maelekezo ili kuondoa tatizo hilo.

Watanzania wametakiwa waweze kuchangamkia kujiunga na huduma za bima kwani zinasaidia kutatua changamoto wanazoweza kukumbana nazo wakati wanapokubwa na majanga ya aina mbali mbali.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi wa TAKAFUL inayotolewa kupitia kampuni ya uwakala ya GALCO Insurance kwa kushirikiana na kampuni mama ya ZIC TAKAFUL LTD ambayo ni huduma ya bima yenye misingi na Sheria za kiislam .

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Bima nchini  (TIRA) Bi.Khadija Said  aliyasema hayo alipo fika kwenye hafla hiyo kumwakilisha Kamishina wa bima wa TIRA nchini Dkt.Baghayo A.Saqware ambapo  amezitaka wakala zinazotoa huduma za bima kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotolewa na mamlaka hiyo.

Bi . Khadija amesema kuwa kampuni zote za uwakala wa bima zinapaswa kuzingatia kanunu na sheria zilizowekwa na TIRA  iliwaweze kitoa huduma kwa wateja wao kwa kiwango na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha ameendelea kufafanua kuwa kwa mujibu wa mpango wa kuendeleza sekta ya fedha hadi kufikia mwaka 2030 matumizi ya bima yamelengwa kufikia asilimia 50 lakini mpaka sasa matumizi hayo ni asilimia kumi na tano pekee nakwamba uelewa wa matumizi ya bima umelengwa kufikia asilimia 80 mwaka 2030 ambapo kwa sasa .

Hata hivyo Bi. Khadija amezisisitiza kampuni na wakala za bima kuendelea kutoa elimu kwa watanzania waweze kuchangamkia.


"Huduma hii ya Bima ya  Takaful  mchakato wake umeanza rasmi mwaka 2008 kupitia kampuni ya ZIC Insuarance na imezinduliwa  rasmi  miezi mitatu iliyopita na Rais wa  serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein  Mwinyi,hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya Bima ya Misingi ya hesheria ya kislam TAKIFUL lakini huduma hii inatolewa kwa waislam na wakristo kwa ujumla"amesema

Takaful ambayo inasimama kama nguzo katika jamii na inasimama katika misingi ya kushirikiana pale ambapo kutakuwa na majanga au faida.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa makampuni ya GSM  Group yanayomiliki kampuni ya Galco Insuarance Ltd ,Benson Mahenya amesema huduma zao za bima ya Takaful sio sera ila ni ahadi ya kuwa wapo karibu na watu katika kutatua changamoto za kibiashara na kimaisha kiujumla .

"Tunafanya kazi katika misingi ya kweli na uwazi na kuhakikisha usawa katika utoaji wa huduma,tuna uzoefu wa miaka mitano sokoni na katika kipindi hiki tumeweza kutoa huduma kwa watu binafsi zaidi ya mia tano na makampuni zaidi ya kumi ,"amesema Mahenya .

Naye meneja Biashara  Emmanuel Bugabu  amesema kuwa Galco Insurance Brokers inashirikiana na makampuni mbali mbali ya kiwemo MAYZUH COMPAZNY LIMITED ilikutoa mafunzo kwa wafanyakazi  na kuhakikisha wana uelewa na huduma ya Takaful na wanashirikiana na pia na ZIC TAKAFUL LTD katika utoaji huduma hiyo ya bima ya misingi ya kiislam TAKAFUL.

"Nia yetu ni kukuza mwamvuli wetu wa huduma  za bima kwa watu wote wakiwemo mtu mmoja mmoja , wanafamilia,wafanyabiashara na makampuni  au taasisi mbali mbali,nakusisitiza kuwa wafanyakazi wa Galco Insuarance wamepata elimu ya kutosha kutoa huduma kwa wateja" amesema Bugabu

 Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema, Serikali imefikia uamuzi huo baada va kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika.

“Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nie.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa
6 usiku”

 

Mfanyabiashara maarufu wa maduka ya simu jijini Arusha aliyefahamika kwa jila moja la Mallya amekutwa amefariki kwenye gari yake katika eneo la Maegesho ya Magari (CITY CAR WASH)huku mwili wake ukiwa umeharibika.

Tukio la kugundulika kwa mwili wa marehemu limetokea mapema leo baada ya waosha magari kusikia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani yagari hilo Askari polisi walifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo uliokuwa kwenye gari aina ya SCUDO lenye namba T 466 AUB lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo.

Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa marehemu Malya amekuwa na desturi ya kufika eneo hilo na kuegesha gari lake na kisha kwenda bar iliyopo eneo hilo kwa ajali ya kula chakula na kunywa.

Mwenyekiti wa eneo hilo maarufu kwa wauzaji wa magari (madalali) ,Alex Kahel alisema alipata taarifa asubuhi ya leo oktoba 13, kuhusiana na tukio hilo na baada ya kufika aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya mfanyabiashara huyo.


 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muuungano na Mazingira, Seleman Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe mkoani Pwani, amekabidhi mifuko 600 ya sarufi kwa  madiwani wa kata za wilaya hiyo kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Shikizi.

Aidha Waziri Jaffo ametoa mitungi ya gesi 126 kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya na mkoa ikiwa ni jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kutunza  mazingira.

Waziri Jaffo amekabidhi  mifuko ya saruji na mitungi ya gesi kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya kilichohudhuriwa  na Katibu wa Chama hicho Mkoa Waziri Jaffo alisema lengo ni kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.

Amesema tayari katika Jimbo la Kisarawe Shule zimejengwa katika maeneo mbalimbali na ni shule nzuri,ila kwa baadhi ya vitongoji bado hivyo wanaendelea na mchakato huo kuhakikisha kila kitongoji kinakuwa na shule shikizi.

“Leo nimetoa mifuko ya cement kwa shule 4 ambapo kila moja imepata matofali 150 yatasaidia kufyatulia matofali na kuanza ujenzi wa madarasa hata mawili mawili,”amesema na kuongeza

“Hii ni kuonesha Wananchi ni namna gani Chama cha Mapunduzi kinavyotekeleza ilani zake na kuhakikisha kila kitongoji kinapata shule hata vile vitongoji vya mbali kama cha Kimelemeta,”amesema.

Katika kikao hicho, hoja mbalimbali ziliibuliwa zenye lengo la kuboresha huduma kwa wananchi likiwemo suala la maji  katika kata sita, Katibu wa CCM mkoa, Bernard Ghaty anatoa maelekezo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Pwani,Bernard Ghaty amesema kipindi wanatoa ahadi katika ilani ya CCM waliwaambia Wananchi watadhibiti ukataji wa miti hovyo na kutengeneza mazingira ambayo ni Suluhu.

Alisema kwa vitendo Waziri Jaffo ameweza kutekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha amegawa majiko ya gesi kwa watendaji wa CCM pamoja na wadau wengine ili wakawe mifano kwa watu wengine kuhakikisha wanatunza mazingira.

“Ni jambo la heshima,msingi na kuigwa kw akufata mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nchi inatunza mazingira na kuiga mfano wa Waziri Jaffo katika kuhakikisha

 Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Bw. Peter Mwevila amesema swala la mawasiliano baina ya watoa huduma za afya ni muhimu katika kupata vipimo sahihi vya mgonjwa.

Bw. Mwavila ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo katika majengo ya Taasisi ya Saratani Ocean Road alipokuwa akiwasilisha mada inayosema “Sample Collection” katika uwasilishaji wa “Continues Medical Education” (CME).

Aidha Bw. Mwevila ameongeza kuwa katika uchukuaji wa “sample” kutoka kwa mgonjwa ni lazima kuzingatia maelekezo ya kila kipimo kinachohitajika kwa kuwa kila kipimo kina utaratibu wake.

Pamoja na hayo Bw. Mwevila ameongeza kuwa iwapo sample imecheleweshwa kufikishwa kwenye maabara au “sample” imehifadhiwa katika kifaa kisicho sahihi, itabidi kuchukuliwa “sample” nyingine ili kupata vipimo hitajika.

Taasisi ya Saratani Ocean Road imekuwa ikitoa fursa kwa idara na vitengo vya ndani na nje ya Taasisi katika kuwasilisha mada mbalimbali kwa watumishi wake, ili waweze kujenga uelewa wa pamoja.

 Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo ametembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kuzungumza na baadhi ya watumishi, huku akiupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa kusimamia vizuri pesa zinazotolewa na serikali kwaajili ya miradi mbalimbali.

Dkt. Mollel amesisitiza kuwa ujenzi wa jengo mfano la Cyclotron ukiliangalia kwa nje unaweza Sema limegharimu kiasi kidogo sana cha pesa ila kwa ndani ndio utagundua thamani ya pesa iliyotumika kuwa inaendana na ubora na umadhubuti wa jengo lenyewe.

Dkt. Mollel ameomba uharaka wa umaliziaji wa jengo hilo ufanyike kwani watanzania wanahitaji huduma zake mapema iwezekanavyo huku serikali ikitaka uwekezaji wake uanze kuleta tija kwa wananchi.

Nae mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage, amemhakikishia Dkt. Mollel kumalizika mapema kwa ujenzi huo kwani kwa upande wa jengo limekamilika kwa Asilimia tisini na nane wakati mashine tayari zimekwishasimikwa kwa asilimia Mia moja huku ukisubiriwa utaratibu wa kuunganisha umeme pekee ili mashine hizo zianze kutumika kama inavyotakiwa.

Jengo hilo limekusanya mashine mbili kubwa ambazo ni PET-CT SCAN pamoja na CYCLOTRON (kiwanda cha kutengeneza mionzi) ambapo kwa sasa kwa Tanzania nzima kitakuwa ni kimoja tu, ambacho kitakuwa kikitengeneza mionzi ambayo itatumika kwa Taasisi huku mingine ikipelekwa kwenye hospitali nyingine kwaajili ya kusaidia wahanga wa huko. Kwa sasa Taasisi inanunua mionzi hiyo kutoka Afrika ya Kusini huku gharama zake zikiwa kubwa mno ukilinganisha na uwezo wa watanzania wenyewe, hivyo kukamilika kwa usimikaji huo kutakuwa msaada mkubwa sana kwa Tanzania na Afrika mashariki na kati kwa ujumla.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wananchi kufanya uchunguzi wa awali wa kupima Saratani ya Matiti ili kujua hali zao na kupata matibabu mapema kwa wenye changamoto hiyo

Waziri Ummy ameyasema hayo Octoba Mosi, 2023 wakati akimuwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kwenye Maadhimisho ya Mwezi wa Saratani ya Matiti yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani takribani Elfu Arobaini na Mbili (42,000) kila Mwaka ndio wanafika katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Pia, Waziri Ummy amesema taarifa ya mwaka 2022/2023, inaonesha kuwa Taasisi ya Saratani Ocean Road ilihudumia wagonjwa wapya takriban 8,779 na asilimia 13 ya wagonjwa hao sawa na wagonjwa 1,141 walikuwa na Saratani ya Matiti.

Sambamba na hayo, Waziri Ummy amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wizara ya Afya kufunga mashine za CT-Scan katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na mashine za Ultrasound katika Hospitali zote za Halmashauri nchini.

Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha matibabu kwa kutuletea vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya uchunguzi wa Saratani mbalimbali ikiwamo PET-CT huku maahine ya Cyclotron ikiwepo kwaajili ya kuzalisha mionzi tiba itakayo tumika hapa kwenye Taasisi huku bakaa ikipangwa kupelekwa kwenye maeneo mengine kwaajili ya kusaidia watanzania wengine.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa kumia mabapo watu duniani kote huungana kupingana na ushambulizi wa aina yoyote wa Saratani hii huku ikiwasaidia wananchi waliokwisha athirika na ugonjwa huo kupata matibabu