Sunday 25 June 2023

MSEMAJI WA SERIKALI ABAINISHA MAMBO MAZURI YA D.P WORLD

Gerson Msigwa amesema mafanikio tutakayopata kutoka kwa D.P world kiwango cha ukusanyaji kodi kitaongezeka kutoka tilioni 7.7 kwa mwaka hatimaye Tanzania tutakusanya tilioni 26 pia hajira za watanzania zitaongezeka kwa kiasi kikubwa vilevile tone za mizigo zitakuwa nyingi kuringanisha na sasa, ambako mizigo hii itabebwa na reli ya SGR vilevile upakuaji wa mizigo kwenye meri utafanyika kwa muda mfupi ukiringanisha na sasa.

Msingwa amesema Bandari yetu inachngia kodi kwa asilimia 37%  D.P World wakiwekeza kwenye bandari yetu utachangia bajeti kwa asimilia 67%. Pia meri zinazopo chelewa kutia nanga kwenye bandari yetu inalipa faini milini 60%

Meli zinakuwa zaidi ya ishirini D.P WORLD wakiwekeza kwenye bandari yetu hakutokuwa na uchelewedshwaji wa meri kuti mamga.

Msingwa ametoa wito kwa watanzania kuwapuuza na kuwabeza wanaopotoshwa uwekezaji wa T.P wor;ld kwenye bandari yetu kwa hawa D.P word wanabandali 190 Duaniani na wapo kwenye nchi 70 duniani, hivyo ni vyeama kumunga mkono Dr. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta D.P nchini Tanzania

haabrio kamili na ally Thabit

SHEKH JALALA AELEZA WASIFU WA MUFT TANZANIA

 Shekh Jalala amesema kipindi cha miaka nane cha mufti wa Tanzania amejifunza mambo mema na mazuri.

habari kamili na Ally Thabith

MUSSA HAJI ASHANGAZWA NA WANAOBEZA MAFANIKIO YA MUUNGANO NA MAPINDUZI YA MWAKA 1964

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar Mussa Haji Mussa, amesema kubeza na kudhihaki mafanikio yaliyopatikana chini ya Muungano na Mapinduzi ya mwaka 1964 haviwezi kuwa tiketi ya kufikia malengo ya kisasa ya Chama Cha ACT-Wazalendo.

Kauli hiyo aliitoa Naibu Katibu Mkuu huyo, wakati akizungumza katika mahojiano maalum huko Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar Gymkhana, alisema mafaniko yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ni kielelezo tosha cha wananchi wa Zanzibar kuendelea kuamini,kupenda na kuunga mkono sera na siasa za CCM inayosimamia Serikali zote mbili nchini.

Alisema tabia za viongozi wa ACT-Wazalendo za kubeza na kudharau hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa chini ya tunu za Muungano na Mapinduzi ya mwaka 1964,haziwezi kuwatengenezea uaminifu wa kisiasa kwa wananchi kwani ni porojo zisizokuwa na dhamira ya kuleta maendeleo nchini.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Mussa, alisema baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakijisahau kwa kutumia majukwaa ya kisiasa kueleza uongo,upotoshaji na kuchochea ubaguzi dhidi ya taifa badala ya kushauri  Serikali mambo yenye tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Chama cha ACT-Wazalendo wameishiwa na sera kwani badala ya kuibua hoja zenye mashiko na kuishauri Serikali mambo mema ya kuimarisha masuala mbalimbali katika nyanja za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni, wao wanabeza na kuzikashifu Serikali zilizowasomesha na Kuwapa madaraka waliyonayo hivi sasa.

Vyama vya upinzani nchini wanatakiwa wakae miaka zaidi ya 200 kutafakari kwa kina njia bora za kushindana na CCM katika medani za kisiasa katika dhana ya kidemokrasia kwani sisi kazi yetu ni kupanga,kufuatilia,kusimamia kisha kutenda kwa vitendo na hatimaye kutoa matokeo chanya yenye manufaa kwa wananchi wote”, alifafanua Mussa.

Mussa, alisema ACT-Wazalendo imeendelea kutumia vibaya haki ya mikutano ya hadhara kwa kukiuka dhamira ya ruhusa ya uwepo wa mikutano hiyo nchini iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, iliyokuwa na malengo ya kukuza demokrasia na ushindani wa kisasa na sio kauli za hoja za chuki dhidi ya Serikali.

Alisema hakuna mwananchi yeyote visiwani Zanzibar ambaye hakuguswa na dhulma,uonevu na ubaguzi wa utawala wa kigeni  kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964, hivyo wanasiasa wanaojitokeza hivi sasa wakaunga mkono hadharani utawala huo watakuwa na ajenda za siri za kutaka kurejesha utawala huo jambo ambalo haliwezekani kwa zama za sasa.

Pamoja na hayo alieleza kwamba kupitia Serikali zote mbili ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendelea kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa sambamba na kuendelea kufungua milango ya uwekezaji na diplomasia zenye tija na maslahi kwa nchi.

Aidha, alisema UVCCM Zanzibar  itaendelea kulinda,kutetea na kujenga hoja imara juu ya kupinga kauli na vitendo vyote  visivyofaa katika michakato ya siasa za kidemokrasia vinavyofanywa na vyama vya upinzani kupitia majukwaa ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Pamoja na hayo Mussa, aliwapongeza Marais wote wawili ambao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 na kuibua miradi mikubwa ya maendeleo,inayoendelea kutoa fursa za ajira kwa vijana nchini.

habari kamili na Ally Thabit

RAIS SAMIA ANAONGEA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA DAWA ZA KULEVYA

KAMISHNA MWAKILEMA ASHIRIKI DORIA YA KUWASAKA SIMBA WALIOZUA TAHARUKI IRINGA

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, William Mwakilema ameungana na timu ya Mkoa wa Iringa kushiriki doria ya kuwasaka wanyama aina ya Simba wanaosemekana wametoka katika maeneo yao ya asili na kuvamia vijiji vilivyoko jirani na Hifadhi ya Taifa Ruaha na kuua mifugo kitu kinachosababisha taharuki katika maeneo wanayozurura.

Nilipata taarifa ya uvamizi wa wanyama hao katika vijiji vilivyoko mbali kabisa na hifadhi zaidi ya kilometa 25 lakini hadi sasa simba hao wameshaenda umbali wa zaidi ya kilometa 70 na wameshavuka barabara ya lami ya kutoka Morogoro, Iringa kwenda Mbeya na wako upande wa pili wa barabara wakiendelea kufanya uharibifu aliongeza Kamishna huyo.

“Baada ya uvamizi wa wanyama hao,timu ya askari 17 kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha na maafisa kutoka Kanda ya Kusini walifika kwa haraka kushirikiana na wenzetu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, TAWA na KDU kuwasaka Simba hao wasilete madhara zaidi” alisema Kamishna Makilema.

Aidha, Kamishna Mwakilema alisema kuwa kutokana na unyeti wa jambo hili tulifanya jitihada za kupata Helikopta na jana wasaidizi wangu wameruka nayo ila kutokana na hali halisi ya milima na makorongo marefu hawakuweza kuwaona. Pia nimeongea na mtu wa AWF pale Manyara Ranch ili kuweza kupata mbwa wa kunusa watusaidie kutambua harufu za Simba hao.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Veronica Kessy alisema kuwa wilaya imeingiwa na taharuki kubwa baada ya kupata taarifa ya uwepo wa Simba katika Kata ya Magoma na kuua ng’ombe. Kwa haraka niliwasiliana na wenzetu wa TANAPA na TAWA kuja kuwaondoa Simba hao.

Hata hivyo, Simba hao waliendelea kusonga mbele wakiua mifugo na hatimae kufika eneo la Kiponzelya karibia na mji wa Iringa. Hadi kufika tarehe 24.06.2023 Simba hao wameshaua ng’ombe 25, na kujeruhi wawili ambao wanaendelea kupatiwa matibabu, pia wameua mbuzi 5, kondoo 5, nguruwe 3 na kuku1 aliongeza mkuu wa wilaya huyo.

Mkazi wa kijiji cha Tanangozi Grayson Laurent Mtende alisema, “baada ya kupata taarifa za Simba kijijini kwetu tuliogopa kwa sababu Simba hawazoeleki na ni mnyama anayeogopwa hivyo tumesitisha kufanya kazi zetu mashambani kwa muda mpaka pale mamlaka zinazohusika na uhifadhi zitakapotuambia hali ni shwari”.

Simba hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 5 bado hawajaonekana na jitihada za kuwasaka zinaendele kwa kutumia magari, helikopta na jitihada za kupata mbwa wa kunusa zinaonyesha kuzaa matunda. Pia wananchi wanaendelea kuelimishwa njia salama za kujilinda na wanyama kwa kutokuwaruhusu watoto na watu wazima kwenda vichakani kuokota kuni, na wanapotoka nje nyakati za usiku watoke na tochi.

DKT. TAX AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA ITALIA JIJINI ROMA

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani ofisini kwake jijini Rome nchini Italia..

 

Akizungumza na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Italia na kuishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuiletea maendeleo kupitia elimu, afya, kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi wa buluu.

 

Mhe. Dkt. Tax ameihakikishia Italia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana nayo na kuhakikisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Italia unakuwa na kufikia ngazi ya juu.



Dkt. Tax amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa majadiliano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya Tanzania na Italia ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili kwa maslahi mapana ya pande zote.

 

“Nafahamu kuwa nchi zetu hazina mfumo wa majadiliano wa kisiasa na kidiplomasia licha ya kuwa na uhusiano mzuri wa siku nyingi, napendekeza tuanzishe mfumo wa majadiliano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya nchi zetu, mfumo huu utatumika kama jukwaa la kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya nchi zetu kwa maslahi ya pande zote,” alisema Dkt. Tax.

Habari kamili na Ally Thabith

MOFTI AELEZEA MIAKA MINANE NDANI YA BAKWATA

Mufti mkuu wa Tanzania (BAKWATA) ABUBAKARI BIN ZUBERI amesema ndani ya miaka nane anajivunia kuimalisha taasisi za kidini kuanzisha shule na vyuo vya kiislam kuongonisha waislam pamoja nawasio kuwa waislam na ujenzi wa msikiti wa kimataifa pamoja na ofisi za BAKWATA.


Habari kamili na Ally Thabit

WATOTO YATIMA WASHIKWA MKONO

 katika kuelekeza sikuku ya Eid-Iladha mkurugenzi wa Dawa na tawhid ametoa nguo kwaajili ya watoto yatima eneo la malkasi

habari kamili na Ally Thabith

Sunday 18 June 2023

UN yalaani shambulizi la kigaidi nchini Uganda lililoua zaidi ya 41

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililoua makumi ya wanafunzi katika eneo la Mpondwe, magharibi mwa Uganda.

Farhan Haq, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Guterres amemshtushwa na shambulizi hilo la kinyama dhidi ya shule moja katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Amesema Katibu Mkuu wa UN ameguswa na ukatili huo wa magaidi wa ADF dhidi ya wanafunzi, ambapo amezinyooshea mkono wa pole familia za wahanga wa hujuma hiyo, serikali na taifa hilo kwa ujumla kufuatia unyama huo.

Wakati huohuo, duru za habari zinaarifu kuwa, idadi ya watu waliouawa katika shambulizi hilo la usiku wa kuamkia jana Jumamosi imefika 41, aghalabu yao wakiwa ni wanafunzi.

Msemaji wa polisi ya Uganda, Fred Enanga amesema jeshi la UPDF linawafuatilia wahalifu katika Mbuga ya Taifa ya Virunga.

Wanafunzi sita waliotekwa nyara na magaidi hao

wenye makao yao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaripotiwa kuwa katika msitu huo wa Virunga.

Wahalifu walioshambulia shule ya Sekondari ya Lubiriha Ijumaa usiku walipora na kuiba chakula na kuchoma moto mabweni ya shule hiyo iliyoko umbali wa kilomiita 2 kutoka kwenye mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Habari kamili na Ally Thabith

OTUBA YA WAZIRI KIVULI WA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MUUNGANO-ACT WAZALENDO 2023

 OTUBA YA WAZIRI KIVULI WA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MUUNGANO-ACT WAZALENDO NDG. PAVU ABDALLAH JUMA KUHUSU MPANGO WA BAJETI WA OFISI YA RAIS- MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24.

Utangulizi.
Wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiendelea kupitia, kujadili na kuidhinisha bajeti mbalimbali za Serikali, jana Jumatano tarehe 19 April 2023, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Ndg. George Simbachawene (Mb) aliwasilisha Bungeni mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

Mpango huo una jumuisha mafungu saba (7) ambao yanagusa, Ofisi ya Rais-Ikulu (Fungu 20 na 30); Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Fungu 33); Utumishi na Utawala Bora (Fungu 32); Sekretarieti ya Ajira (Fungu 67); Tume ya Utumishi wa Umma (Fungu 94); na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (Fungu 04); Kutokana na umuhimu wake ni tumeona lazima liwepo jicho la kumulika, kufuatilia na kutoa mtazamo mbadala katika mpango huu.

ACT Wazalendo katika kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Serikali, kupitia Waziri Kivuli wa Utumishi na Utawala bora imefuatilia na kuichambua hotuba hiyo kwa lengo la kuimulika ili kuona kwa kiasi gani imebeba matarajio ya wananchi katika kupata huduma na usimamizi wa rasilimali zao au vinginevyo. Kutokana na uchambuzi tulioufanya, tumekuja na maeneo saba (7) yenye changamoto na kuweka mtazamo mbadala wa ACT Wazalendo kuhusu hotuba hiyo ya Serikali, ambayo inaonyesha mambo ni yale yale.

Maeneo saba (7) ya uchambuzi wa ACT Wazalendo kuhusu Mpango na Bajeti ya Wizara ya Utumishi wa umma na Utawala bora kwa Mwaka wa Fedha 2023/24.

1. Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) iondoke Ikulu.

Katika uchambuzi wetu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 tuliofanya April 11, 2023 tulieleza maamuzi mabovu yaliyofanywa na Serikali mwaka 2016 kuhusu Wakala wa Ndege za Serikali.

Mosi, uamuzi wa kuipeleka TGFA kuwa chini ya Ofisi ya Rais Ikulu kutoka wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Pili, Wakala kuongezewa jukumu la kuratibu ununuzi wa ndege, kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na kusimamia mikataba ya ukodishwaji wa ndege hizo kwa niaba ya Serikali, mbali na jukumu lake la asili la kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine wa Kitaifa.

Tulieleza athari za uamuzi huo unathibitishwa na ripoti ya CAG, ambayo imeonyesha ATCL wanaendelea kupata hasara ya Shilingi bilioni 35 sambamba na Shirika hilo kuwa na mtaji hasi wa shilingi bilioni 158. Tuliweka wazi kuwa hasara inayopata ATCL kwa sehemu kubwa inatokana na mfumo wa umiliki wa ndege. Mfumo uliopo sasa ATCL haimiliki ndege. Ndege zote zilizonunuliwa na Serikali kwa fedha za walipa kodi zinamilikiwa na TGFA na kukodishwa kwa ATCL. Mfumo huu unaoleta hasara kwa taifa unatokana na uamuzi wa mwaka 2016.

Tunashangaa katika hotuba ya bajeti ya wizara hii kwa mwaka wa fedha 2023/24, tumeendelea kuona Wakala wa Ndege za Serikali inaratibu mpango wa ununuzi wa ndege na kuzikodisha kwa Kampuni ya Ndege ya Taifa (ATCL). Licha ya kushauriwa kutoendelea na uamuzi huu. ACT Wazalendo tunaona Serikali inataka kuendelea kuisababishia hasara ATCL kwa kung’ang’ania kutekeleza uamuzi mbovu wa huko nyuma.
Aidha, bado tunaona uamuzi uliofanywa kuhusu Wakala wa Ndege za Serikali kuwekwa chini Ofisi ya Rais Ikulu ni uamuzi usiofaa.

Kwasababu haukufanywa kwa ajili ya manufaa ya umma badala yake ulilenga kuzuia uwazi na uwajibikajika katika mikataba ya ununuzi wa ndege. Kitendo kilichopelekea kurudisha nyuma jitihada za kudhibiti ubadhirifu na ufisadi katika manunuzi ya ndege ambayo sasa yanalalamikiwa hata na Rais mwenyewe.
Hivyo basi, ACT Wazalendo tunarudia wito wetu wa kuitaka Serikali kuirejesha TGFA wizara inayohusika na Uchukuzi ili kudhibiti ubadhirifu na wizi kwa kuimarisha uwazi, kwakuwa bajeti ya wizara ina kaguliwa na ripoti yake inakuwa wazi.

Pili, tunaitaka Serikali imwagize CAG kufanya ukaguzi maalumu wa manunuzi ya Ndege tangu tulipoanza kununua ndege mwaka 2016.

Tatu, tunaitaka Serikali ifanye mapitio ya mikataba yote ya manunuzi ya ndege kwa lengo la kuiboresha kwenye mapungufu.

2. Kanuni mpya za mafao bado zinaumiza wazee wetu wastaafu.

Wizara ya Utumishi na Utawala bora pamoja na majukumu mengine ina wajibu wa kuhakikisha nidhamu, maadili na utendaji wa watumishi wa umma nchini. Suala la utendaji na nidhamu linahusiano wa karibu sana na ustawi, haki na maslahi ya watumishi hao.

Kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya watumishi wa umma wanaostaafu kupunjwa mafao yao tangu kuanza kutumika kwa kanuni mpya ya kikotoo cha mafao Julai 01, 2022.

Kanuni mpya ya ukokotoaji wa asilimia 33 na kikotoo cha 1/580 badala ya 1/540 kinapunguza malipo ya mkupuo (lumpsum) ya kiinua mgongo cha mtumishi anayestaafu kwa asilimia 50.5 ukilinganisha na kanuni za awali (kabla 2018).

Itakumbukwa kuwa ujio wa kanuni hizi, zilitokana na mvutano mkubwa mwaka 2018 baada ya Serikali kupeleka Bungeni muswada wa kanuni za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoambatana na kanuni mpya za kukokotoa mafao ya wastaafu. Kanuni hii (kikotoo) ilipingwa na wafanyakazi, wanaharakati na wanasiasa kila kona kwa hoja za wazi kabisa.

Kurejeshwa kwake mwaka jana (bila mwafaka wa pande mbili) ndio imeanza kuleta kelele, vilio na masikitiko kama sio kushusha hamasa na ari ya watumishi wengi nchini. Huku kikiwa na marekebisho madogo tu ya asilimia za mkupuo kutoka 25 iliyopendekezwa na Serikali yenyewe, hadi asilimia 33 lakini bado haiendi kuwasaidia wastaafu badala yake inaenda kuwaumiza.

Sisi, ACT Wazalendo tunaendelea kupinga utekelezaji wa kanuni hizi. Tunaamini hatupaswi kuwaadhibu wazee wetu kwa kukubali kanuni hizi kandamizi kuendelea kuwapunja mafao yao. Aidha, hatukubaliana na uamuzi wa Serikali kuwabebesha watumishi wanaostaafu mzigo wa gharama kwa makosa ya utendaji mbovu wa menejimeti za mifuko na madeni ya Serikali.

Hivyo, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kulipa madeni yote (Kiasi cha Shilingi trilioni 1.4) inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mkupuo mmoja ili kuiwezesha mifuko kujiendesha na kuhudumia wanachama wake kwa wakati.

Pia tunaitaka Serikali kurejesha kanuni za mwaka 2017 ambazo zinatoa mafao ya malipo ya mkupuo kwa 50%, kikokotoo kuwa ni 1/540, umri wa kuishi baada ya kustaafu ni miaka 15.5 na 50% inayobaki ya mafao ya mtumishi iwe pensheni ya kila mwezi.

3. Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

Katika mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2023/24 wizara ya utumishi imeendelea na jukumu la kuratibu na kusimamia Miradi ya Maendeleo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Sisi, ACT Wazalendo katika kuangazia jukumu hili, tumekuwa tukielezea changamoto, hoja na mapendekezo ya namna bora ya kusimamia fedha za TASAF kufuatia na malalamiko mbalimbali tuliyoyapokea kutoka kwa wananchi.

Mosi, kuhusu utaratibu mpya wa Serikali maeneo mbalimbali nchini wa kuwafanyisha kazi ngumu wazee na watu wenye ulemavu kama kigezo cha kupatiwa fedha hizo za Tasaf. Wanufaika hao wanalazimishwa kufanya kazi za nguvu kama vile kuchimba mitaro, mabwawa, kufanya usafi kwenye shule au kufyatulishwa matofali badala ya kupatiwa fedha hizo kama ruzuku kutokana na kundi lao.

Pili, fedha hizo sasa hivi zinatolewa kwa ubaguzi au kutumika vibaya na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ili kujinufaisha kisiasa kwa kuwatisha watu wenye vigezo vya kunufaika na TASAF kuwa hawatonufaika iwapo hawatajiunga na CCM au kuwaondoa kwenye mfumo ikiwa watakuwa Wapinzani wa CCM. Aidha, kutoeleweka kwa viwango wanavyopaswa kupewa wanufaika kwa mwezi au kipindi maalum inatoka bila utaratibu unaoeleweka hivyo kukwaza lengo la fedha hizo.

Katika mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imeiombea fedha cha Shilingi bilioni 218.9 kwa ajili ya walengwa TASAF nchini. Kutokana malalamiko ya wanufaika juu hoja hizi ni wazi wapo watu wanaopaswa kunufaika na fedha hizi watachwa nje ya mfumo huo.

ACT Wazalendo tunaendelea kumtaka Waziri mwenye wizara (Utumishi na utawala bora) husika kufuatilia kwa karibu, kujitokeza kutoa ufafanuzi na kuchukua hatua za kumaliza changamoto hizo Nchi nzima. Pia, CCM iache kulaghai watanzania fedha hizi ni za mkopo kutoka Benki ya Dunia na wahisani wengine, zinalipwa na watanzania wote bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kwa kuwa watakatwa kupitia kodi mbalimbali, haikubaliki kuona watu wa chama au wasiokuwa wanachama wanabaguliwa.

Mwisho, tunaona ili kumaliza tatizo hili ni lazima Serikali iimarishe mfumo wa hifadhi ya jamii ili kutoa pensheni kwa wazee wote badala ya kutegemea fedha za Mkopo ambazo zinaweza kusitishwa mara moja.

4. Ubadhirifu wa fedha za Umma.
Sekta ya Utumishi wa umma ni muhimu sana kwenye mapambano dhidi ya ubadhirifu au kuchunga matumizi mazuri ya fedha za umma. Ingawa, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora ina wajibu huo. Bado tumeendelea kuona upotevu wa fedha, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma kwenye Ofisi, Idara na Halmashauri mbalimbali nchini.

Hoja ya ubadhirifu imekuwa ikirudiwa rudiwa kwenye ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Katika ripoti ya mwaka 2021/22 iliyotoka mwaka huu imeonyesha hali imendelea kuwa mbaya zaidi kuhusu upotevu wa fedha na ubadhirifu.
Mathalani hoja za ukaguzi zinazonyesha ubadhirifu kwa Wizara ya TAMISEMI peke yake zina thamani ya Shilingi bilioni 975. Vilievile, kuna matumizi mabaya ya fedha kwenye wizara ya Ujenzi na uchukuzi hoja za ukaguzi inafikia thamani ya Shilingi trilioni 4.6. Aidha, matumizi mabaya ya fedha za Mkopo wa UVIKO 19 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yameonekana kiasi cha shilingi bilioni 212.1 sawa na asilimia 17.06 ya fedha zote za mkopo zilitolewa ambazo ni shilingi Trilioni 1.24.

Katika hotuba ya Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na utawala bora iliowasilishwa na Ndg.Waziri George Simbachawene haijaongelea kuhusu hatua ambazo zitachukuliwa juu ya watu waliotajwa kwenye ubadhilifu wa fedha za umma hii inaonyesha kwa namna gani serikali inashindwa kuwajibika na kuwachukulia hatua stahiki watu waliohusika katika ubadhilifu wa fedha hizo

ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote waliohusika katika ubadhilifu wa fedha hizi.

5. Kutomalizwa kwa madai ya muda mrefu ya malimbikizo ya mishahara ya Watumishi wa umma.

Katika uchambuzi tulioufanya mwaka jana (2022) wa bajeti na ripoti ya CAG tulionyesha kuwepo kwa malimbikizo ya muda mrefu ya mishahara, madeni na stahiki zilizotakiwa kulipwa kwa Watumishi wa Umma kiasi cha Shilingi bilioni 429.80 mwaka 2020/2021 kutoka shilingi bilioni 334.15 mwaka wa fedha 2019/2020. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 28%. Malimbikizo hayo yalitokana na watumishi kutolipwa kwa wakati, malimbikizo ya mishahara ya waajiriwa wapya, waliopandishwa madaraja, makato na posho za watumishi.

Katika taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2022/23 iliyotolewa na Waziri Bungeni ni imeonyesha kuwa Serikali imelipa jumla ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 119,098 yenye thamani ya shilingi bilioni 204.42. Hii ni hatua inayoleta matumaini kwa watumishi wa umma na wafanyakazi nchini. Ingawa, tumepatwa na mshangao kuona katika mwaka huu wa fedha hakuna mpango ulioanishwa wa kibajeti wa kumalizia malimbikizo yaliyobaki ambayo zaidi ya asilimia 50 ya madai (shilingi bilioni 225.5).
ACT Wazalendo tunarudia wito wetu kwa kuitaka Serikali kumaliza kwa mkupuo madai malimbikizo ya watumishi kupitia mfumo wa hatifungani maalum. Aidha, tunasisitiza Serikali kuyatambua madeni haya katika takwimu za deni la taifa na kuimarisha mfumo wa kulipa madai ya watumishi ambao utahakikisha kuwa madeni mapya hayatoozalishwa tena siku za usoni.

6. Mfumo wa ajira na upungufu mkubwa wa watumishi wa umma nchini.
Serikali kupitia wizara hii ndio inayoratibu masuala ya ajira ya watumishi wa umma kwa taasisi za Serikali kuu, idara na halmashauri. Mwenendo wa miaka mitano (5) hadi sasa unaonyesha kutoridhisha kiwango uwiano kati ya maombi ya vibali vya ajira kwa taasisi mbalimbali na ajira zinazoidhinishwa na kutolewa na Serikali.

Hii ina maana kuwa mahitaji ya watumishi katika taasisi, idara na Ofisi za umma na kasi ya ajira zinazoidhinishwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma haviwiani (haviendi sambamba). Mathalani mahitaji ya watumishi kwa Serikali Kuu na Idara kwa mujibu wa ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2021/22 inaonyesha kuwa kwa miaka mitatu yaani 2019/20, 2020/21 na 2021/22 mahitaji (vibali vilivyoombwa) vilikuwa 77,703, huku mpango wa kuajiri wa Serikali ulikuwa kuajiri watumishi 24,948. Lakini Serikali iliweza kutoa vibali 25, 602. Mwenendo wa jumla ya uajiri wa Serikali ukilinganishwa na mahitaji ni asilimia 35 tu. CAG anasema kuwa “Tatizo la upungufu wa Watumishi wa Umma bado ni kubwa na linasababishwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kushindwa kutoa vibali kwa wakati. Hii inapelekea Taasisi za Umma kutofikia malengo ya kiutendaji.”

Aidha, hali ya upungufu wa wafanyakazi imezikumba zaidi Mamalaka za Serikali za Mitaa ambazo pia vibali vya kuajili vinategemea kupitia wizara hii. Hii inapelekea ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani kwenye sekta ya elimu na afya umeathirika kutokana na Watumishi waliopo kuzidiwa na majukumu.

ACT Wazalendo tunaitaka Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutoa vibali vya ajira kwa taasisi zinazohitaji wataalamu lakini pia kuhakikisha wataalamu wanaopatikana wana vigezo vya taaluma zao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

7. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanyiwe ukaguzi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007. Sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Sura ya 329 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

TAKUKURU inaingia kwenye kundi la taasisi zilizowekwa chini ya Ofisi ya Rais Ikulu kiasi cha kushindwa kumulikwa ufanisi wake kwa kuwianisha na matumizi inayofanya. TAKUKURU inatengewa fedha na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria zilizoanzisha TAKUKURU inapaswa kukaguliwa kila mwaka lakini tangu mwaka 2007 ilipoanzisha haijawahi kukaguliwa.

Kutokana na uzoefu wa utendaji, historia na tafiti mbalimbali licha ya kuwa ni chombo kilichoanzishwa ili kuimarisha uwajibikaji na kuchunga matumizi mazuri ya rasilimali yapo malalamiko na tuhuma za matumizi mabaya ya Ofisi kwa baadhi ya watumishi, ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma.

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuweka taarifa za fedha zinazojitegemea za TAKUKURU sio kufichwa kwenye fungu la 20 la bajeti. Pia, tunaitaka Serikali kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuifanya ukaguzi TAKUKURU kama sheria zinavyotaka na taarifa yake iwe wazi kwa umma.

Hitimisho
Mpango wa utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Menejimeti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka 2023/24 unaonyesha bado mambo ni yale yale. Dhana ya utawala bora inazidi kudorora kufuatiwa na hoja za ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma katika ofisi mbalimbali za Serikali kuu, idara na Halmashauri nchini. Aidha, kuendelea kuruhusu kutumika kwa kanuni mpya ya kikotoo cha mafao kwa watumishi wanaoenda kustaafu kunaporomosha ari na utendaji wa watumishi. Vilevile, suala la matumizi ya fedha za maendeleo ya jamii kutowekewa utaratibu mzuri kutaendelea kuchomwa fedha hizo bila kuleta matokeo tarajiwa.

Wizara ya Utumishi inapaswa kumulika uwajibikaji wa Serikali kwa kuimarisha vyombo vya kuisimamia serikali kama vile Ofisi ya Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Pia kuimarisha taasisi za usimamizi na ulinzi wa sheria kama vile, Usalama wa taifa, Tume ya Maadili ya Utumishi wa umma

TAARIFA KWA UMMA

Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Miundombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023 (Intergovernmental Agreement – Iga, between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai concerning Economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania). Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne tarehe 06, Juni saa 7:30 mchana katika Ukumbi wa Msekwa ‘D’, Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma. Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

Azimio hilo linaweza pia kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, DODOMA


habari kamili na Ally Thabit

UVCCM MKOA DAR ES SALAAM YATEMA CHECHE KWA WANASIASA UCHWALA

 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Bi Nasra amewataka wanasiasa nchini Tanzania waache kumbeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fursa kwa wawekezaji nchini Tanzania D.P. World kwakuja kuwekeza kwenye bandari zetu nchini Tanzania.

Habari Kamili na Ally Thabiti

WAKALA WA BARABARA TANROAD YATOA FURSA KWA WAKANDARASI WAZAWA

Meneja miradi wa Tanroad Benamungu amewataka wakandarasi nchini Tanzania wachangamkie fursa za miradi ya Barabara.

habari kamili na Ally Thabit

JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM LATANGAZA VITA KALI

 Mkuu wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ASP Mulilo Jumanne amewataka wote waliokuwa na mipango yakuandamana tarehe 19/06/2023amewataka waache mara moja kufanya maandamano hayo endapo wakiuka maagizo ya maelekezo ya jeshi la polisi hatua hatua kali zitachukuliwa dhidi yao pia jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu kumi , ambao walikuwa wanahujumu miundo mbinu ya mawasiliano maeneo ya Mkuranga, Chanika na sehemu zingine. Ambapo wamekatwa wakiwa na Betry za minala ya simu yenye samani ya shilingi 163,000,000 na magari mawili ambayo yalikuwa yanatumika kufanyia uharifu. Juma ya Betri za minala simu ni 68

Habari kamili na Ally Thabit

REA NA WAKANDARASI WASAINI NYONGEZA YA KAZI KATIKA MIKATABA ILI KUONGEZA KILOMETA MBILI ZA UMEME KWA VIJIJI 4,071


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) tarehe 16 Juni, 2023 imesaini nyongeza ya kazi (Addendum) katika mikataba ya kupeleka nishati ya umeme vijijini ambapo sasa vijiji 4,071 vitapata nyongeza ya kilometa mbili za umeme wa msongo mdogo.

Tukio hilo la kusaini nyongeza ya kazi katika mikataba hiyo ya kupeleka umeme vijijini, liliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi, Hassan Saidy pamoja na Wakandarasi 21 kutoka ndani na nje ya nchi huku pia likishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Janet Mbene pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo katika ukumbi wa Ngome, Jijini, Dar es Salaam.

Baada ya hafla hiyo, Mhandisi Hassan Saidy alisema, hitaji la nyongeza ya kazi ya kupeleka umeme vijijini, lilianza kutolewa na makundi mengi ya watu, wakiwemo Waheshimiwa Wabunge pamoja na Wananchi wenyewe.

“Serikali ilisikia maombi yao, tunashukuru walitupa fedha na mwaka huu, tukaamua kuongeza kilometa mbili katika kila kijiji.”

“Mtakumbuka kuwa awali, kila kijiji kilipata kilometa moja (1) za umeme ambazo ni sawa na nguzo ishirini (20), sasa baada ya kusaini nyongeza hii, kupitia Mradi wa Kupeleka Nishati Vijijini Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili (REA 3, II), hadi mwezi Desemba, 2023 vijiji hivyo 4,071 vitapata kilometa mbili zaidi.” Amekaririwa Mhandisi Saidy.

Mhandisi Saidy amesema Watu wengi wameona umuhimu wa umeme katika kuleta maendeleo


pamoja na kubadilisha maisha yao kijamii na kiuchumi na kuongeza kuwa nyongeza hiyo ya kazi italeta mabadiliko makubwa kwa Watu.

“Jumla tumeongeza zaidi ya kilometa 8,000 kwa Mradi mzima wa REA 3, II kwa hiyo vijiji 4,072 vilivyopata umeme kwa kilometa moja (1), sasa kila kijiji kitapata kilometa mbili (2) zaidi.” Alisema Mhandisi Hassan Saidy, Mkurugenzi Mkuu wa REA.

Habari picha na Ally Thabit

MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 20 WATATULIWA -TARANGIRE



Mgogoro wa ardhi baina ya Hifadhi ya Taifa Tarangire na Kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro Mkoani Manyara uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 umefikia tamati baada ya kuwekwa mipaka mipya ya Hifadhi ya Taifa Tarangire ambapo wananchi wa Kijiji hicho wamepatiwa eneo la kilomita za mraba 17.77 sawa na ekari 4392.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Afisa Misitu Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Michael Gwandu, aliwataka wananchi wanaopakana na maeneo ya hifadhi kuheshimu mipaka iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ambayo serikali inalazimika kutumia gharama kubwa kuitatua.

Afisa Wanyamapori Mkuu ambae pia anashughulikia kitengo cha utatuzi wa migogoro ya maeneo yaliyohifadhiwa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Fransis Kauzeni, alisema zoezi hilo linatekelezwa kufuatia ushauri wa Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta iliyoundwa na serikali ili kukusanya maoni kuhusu migogoro kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi.

Bw. Pellage aliongeza kuwa eneo hilo litasaidia wananchi hao ambao walishaanza kulitumia kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo kilimo, malisho na makazi.

Na kuongeza kuwa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo linazingatia kutokuingilia mfumo wa ikolojia na kubainisha kuwa mojawapo ya maagizo ya Baraza la Mawaziri baada ya uamuzi wake ni kuwekwa alama za kudumu zinazoonekana ili iwe rahisi kila mmoja kuona mpaka wake.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tarangire Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi – Beatrice Kessy, amesema kamati hiyo ilishauri kilomita za mraba 17.77 ambazo ni sawa na hekari 4,392 zimegwe katika eneo la hifadhi na kurejeshwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Aidha, Kamishna Kessy alisema eneo linalowekwa mpaka huo lina urefu wa kilomita 10 ambalo wanatarajia kuweka vigingi 30 na hadi sasa wameweka vigingi 22 na kuwa zoezi hilo lililoanza Juni 12,2023 litakamilika kabla ya Juni 30.

Pia, aliongeza mgogoro huo wa zaidi ya miaka 20 ulisababisha shughuli za uhifadhi, doria, uwekezaji na shughuli za wananchi kushindwa kutekelezwa, hivyo wanaamini baada ya kuisha kwa mgogoro mahusiano baina ya hifadhi na wanakijiji yataboreka zaidi ikiwa ni pamoja na shughuli za uhifadhi na utalii zitaendelea.

“Mgogoro huu umechelewesha maendeleo ya wananchi na shughuli za uhifadhi na utalii katika upande huu wa Kusini mwa Hifadhi ya Taifa Tarangire, kwa sasa shughuli za utalii zitafanyika kwa sababu hata ukimpa mwekezaji kuwekeza itanufaisha jamii na kusaidia kuendeleza uchumi wa kijiji na kuchangia kwenye pato la taifa,kuliko ilivyokuwa awali ambapo huwezi hata kuendeleza shughuli za utalii mfano kuanzia walking safari,” alisema Kamishna Kessy.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kimotorok,Elias Pamelo, amesema wanatarajia baada ya mgogoro kuisha ujirani baina yao na hifadhi hiyo utaimarika na kuomba serikali kuangalia namna ya kusaidia maeneo machache ambayo bado yako nje ya kijiji hicho kurudishwa kwao.

“Mgogoro huu na sisi kama wananchi tunatamani uishe kwa sababu ni wa muda mrefu ila tunaomba serikali kwenye mapungufu ni kidogo hivyo tutakapopata nafasi tena licha ya kuwa tumepewa eneo kubwa ambalo awali lilikuwa la hifadhi ila kuna eneo ambalo limeonekana ni la hifadhi na tulikuwa tunatumia kwa ajili ya malisho,makazi na mashamba tungeomba hilo tuongezewe,”amesema

Naye, mzee wa mila la kabila la kimasai Laigwanan,Loserian Siria, alishukuru serikali kwa utatuzi wa mgogoro huo na kuomba kuangalia namna serikali inaweza kuongeza eneo kwa ajili ya kijiji hicho ambalo limeonekana kuwa ndani ya hifadhi huku kukiwa na maboma kadhaa ndani yake.

Habari Picha na Ally Thabiti

MAHUJAJI 3000 KUTOKA TANZANIA KWENDA KUHIJI MAKKA

 Mahujaji 3000 kutoka Tanzania wanatarajia kwenda Hijja Saud Arabia katika mji wa Makka siku ya kesho juni 18,2023 ikiwa ni sehemu ya kutekeleza nguzo tano ya dini ya kiislam.

Afisa habari na Mratibu wa safari ya hijja Sheikh Khamis Tembo katika msikiti wa Mwinyi jijini Dar-es-salaam amesema,ibada ya hija inawakati maalumu pamoja na taratibu za maandalizi ambapo kimsingi tayari zimekamilika.

Pia ametoa wito kwa Mahujaji kuwa na subira katika yale waliyowaelekeza pamoja na kuwatakia heri katika safari hiyo muhimu ya kutimiza nguzo ya tano ya Uislamu.



Habari Picha na Ally Thabith

Monday 12 June 2023

WAAMIAJI WAJIVUNIA PASSPORT MTANDAONI

Mlatibu mkuu wa Uhamiaji Azizi amesema uwombaji passport kwa njia ya mtandao kumeleta faida kubwa sana ikiwemo kuondoa urasimu, rushwa, na kuokoa muda kwa wateja na jeshi la uwamaji Bw. Azizi Kilondomala mlatibu wa jeshi la uwamiaji amesema wanamikakati ya kuwafikia watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa upande wa elimu naye Juma Dau Mlatibu msaidizi wa jeshi la Uhamiaji ameipongeza serikali kwa kuja na passport mtandaoni.


Habari na Ally Thabiti

Yanga SC waandika rekodi nyingine, ‘Mabingwa ASFC 2023’


Ni Club ya Young Africans wameandika rekodi nyingine ya kuchukua kombe la Shirikisho la Azam Sports katika fainali iliyochezwa lleo Juni 12, 2023 Mkoani Tanga katika Dimba la Mkwakwani baada ya kuibuka kwa ushindi wa goli moja dhidi ya Azam FC.






Spika Dkt Tulia awasili nchini Morocco


 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Marrakesh, nchini Morocco leo tarehe 12 Juni, 2023.

Dkt. Tulia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Kibunge wa Majadiliano kuhusu Dini mbalimbali (Conference on Interfaith Dialogue) utakaofanyika nchini humo Juni 13 – 15, 2023.

Aidha, katika Mkutano huo Mhe. Dkt. Tulia ameambatana na Waheshimiwa Wabunge Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Esther Matiko pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa Mwihambi ndc.


Hbari picha na Ally Thabiti

TANESCO YAZINDUA UMEME WA UPEPO SHINYANGA

 Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa shilika la umeme TANESCO MAALAGE CHANDE amesema lengo la kuzindua umeme wa upepo mjini shinyanga kwenye vitongoji vyake na vijiji ili wananchi wapate nishati ya umeme iliyo raisi.

Habari na Ally Thabiti

NAIBU WAZIRI WA KILIMO AIMIZA LISHE BORA

 Antony Mavunde naibu waziri wizara ya kilimo amewataka watu kuzingatia lishe bora amesema haya mkoani dodoma kwenye kilele ya siku ya lishe duniani ambako taasisi ya TAA iliandaa.

Habari na Ally Thabiti

UVCCM TAIFA YAUNGA MKONO MRADI WA DP WORLD

 
























Habari na Ally Thabiti