Sunday, 18 June 2023

TAARIFA KWA UMMA

Kamati ya Pamoja (Joint Committee) ya Bunge ya Miundombinu na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023 (Intergovernmental Agreement – Iga, between the United Republic of Tanzania and the Emirate of Dubai concerning Economic and Social Partnership for the Development and Improving Performance of Ports in Tanzania). Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Jumanne tarehe 06, Juni saa 7:30 mchana katika Ukumbi wa Msekwa ‘D’, Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma. Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

Azimio hilo linaweza pia kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, DODOMA


habari kamili na Ally Thabit

No comments:

Post a Comment