Sunday 28 June 2020

TGNP MTANDAO YATOA SOMO KWA WANDISHI WA HABARI

 Mkurugenzi wa TGNP mtandao ametoa msisitizo kwa waandishi wa habari kuwa makini na taaluma zao na kuandika kwa weledi sana.
Ameonya kuwa waandishi wanapaswa kuacha kuandika habari ambazo hazina maana katika jamii. Pia wanatakiwa hasa kipindi hiki cha bajeti 2020/2021 kuonyesha ukomavu wao katika kufundisha jamii kupiq taaluma waliyo nayo
 Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliya mafunzo hayo katika ukumbi wa TGNP MTANDAO mabibo
Habari picha na Ally Thabit

Wednesday 24 June 2020

Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimepokea wanachama wapya 80 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Kibamba jijini Dar es salaam kwa lengo la kuungana na chama hicho ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika Hafla ya kuwapokea wanachama hao wapya iliyofanyika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema amesema wanachama hao wameamua kujiunga na chama hicho baada yaTLP kutangaza nia ya kumuunga mkono Rais Magufuli kama mgombea wa Urais ktk uchaguzi mkuu ujao baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake.
Nao kwa upande wao, wanachama hao wapya wamezungumzia lengo la kuhamia TLP ambapo wamesema sababu kubwa ni Mbunge wa Chadema katika Jimbo la Kibamba kushindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati akiomba kura katika uchaguzi uliopita ikiwemo kero ya maji pamoja na mikopo kwa Vijana

Monday 22 June 2020

MUONGOZO WA ASASI ZA KIRAIA NI MWIBA MKALI


Mratibu wa Watetezi wa Asasi za Kiraia kutoka THRDC Onesmo Eli Ngurumo amesema muongozo uliotolewa na serikali Kwa asasi za kiraia umekuwa kikwazo na tatizo kubwa  Kwa asasi za kiraia kutekeleza majukumu Yao kwani muongozo huu unafanya asasi zisiwe huru katika kutekeleza majukumu Yao ya miradi ambako inarazimisha kupata kibari cha fedha zaidi ya milioni 20 kutoka Wizara ya fedha kulekebisha Cheri Kwa miaka 10 hii no tatizo,  ukitaka kusajili asasi za kiraia shariti wawepo watanzania wawili uku no kuuwa sekta ya asasi za kiraia  ametoa wito Kwa serikali kutozirazimisha asasi za kiraia kufanya miradi ya serikali kwani Kila asasi inamipango yake yakutekeleza miradi Onesmo Eli Ngurumo ameitaka serikali waweze kufanya malekebisho ya muongozo waliotoa  Kwa kushirikiana na asasi za kiraia ili Uhuru,Haki na usawa amesema haya jijini DSM


Habari picha na Ally Thabit

THRDC YATOA TAMKO KUHUSU MONGOZO WA URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Katherine Lingo ni Wakiri  wa THRDC kwaniaba  ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wenye jimla ya Mashirika  Wanachama 200 nchini Tanzania wameitaka serikali kuweza kufanya mabadiliko kwenye Muongozo waliotoa Chetii kisiboreshwe ndani ya miaka 10 Pia kibari cha fedha kisitoke Kwa Waziri WA fedha na mikataba yote ya fedha itoke Kwa msajili wa  asasi  za kiraia

Wameitaka serikali wakiwa wanafanya mabadiliko kwenye asasi za kiraia zishirikishwe Katherine amesema muongozo huu Unamambo mengine mazuri

Habari picha na Ally Thabit

Friday 19 June 2020

WAZIRI UMMY AZINDUA MWONGOZO WA MATIBABU YA SIKOSELI

Waziri Ummy Mwalimu akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi wakikata utepe kuzindua muongozo wa tiba ya wagonjwa wa Sikoseli nchini

Waziri Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa watoto waliozaliwa na Sikoseli wakati wa maadhimisho ya siku ya sikoseli duniani.

Waziri Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru muongozo wa matibabu ya sikoseli mara baada ya kuzindua.



Picha ya Pamoja na Madaktari wa Watoto

Picha ya pamoja na Watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli


Serikali imezindua mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa watu wenye ugonjwa wa sikoseli, huku ikiagiza kuanzishwa kwa kliniki maalumu za kuchunguza ugonjwa huo katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuhakikisha watu wengi hasa watoto wanafikiwa.

Akizindua mwongozo huo leo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuanzishwa kwa kliniki katika ngazi za wilaya na mikoa itasaidia watu mbalimbali kupata huduma ya utambuzi ya ugonjwa wa sikoseli karibu na maeneo wanayoishi.

“Naagiza vipimo vya utambuzi kupelekwa kwenye ngazi ya wilaya na mikoa ili kila mtu aweze kuchunguzwa kama ana tatizo la sikoseli". Amesema Waziri Ummy.

Pia, Waziri ameshauri upatikanaji salama wa damu kwa ajili ya watu wenye tatizo la ugonjwa sikoseli ili kuondoa changamoto ya tiba kwa wagonjwa mbalimbali.

Waziri wa Ummy ameshauri wananchi kufanya uchunguzi wa afya zao mapema ili kubaini kama wana ugonjwa huo kwani endapo watabaini itawasaidia kuanza matibabu mapema.

 Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya amewataka wadau wa ugonjwa huo kupunguza gharama za dawa kwani wagonjwa wengi hawezi kuzinunua.

“Naagiza pia dawa ya sikoseli ziingizwe katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili iwe rahisi kupatika kwa wagonjwa wengi". Amesema Waziri Ummy.

Nae Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi amesema Serikali imefikia hatua kubwa ya kuanzishwa kwa mwongozo wa Taifa wa matibabu kwa wagonjwa wa sikoseli kwa kuwa utazuia vifo vingi.

Amesema vifo vingi vinavyotokana na ugonjwa wa sikoseli, vinaweza kuzuilika endapo utagundulika mapema kwa watoto wachanga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema katika kliniki ya wagonjwa wa sikoseli, watoto 50 hadi 70 wamekuwa wakipatiwa matibabu ya ugonjwa huo wakati kwa mwezi ni wagonjwa 211 hadi 300.

“Katika kliniki ya watu wazima, kwa siku wanaonwa wagonjwa 30 hadi 40 na kwa mwezi wagonjwa 160 hadi 200 wanatibiwa hapa Muhimbili". Amesema Prof. Museru.

Prof. Museru amesema watoto wenye ugonjwa huo wamekuwa wakipata tatizo la kupumua, damu kuganda mwilini na kiharusi.

Kauli mbiu ya mwaka huu, “Huduma Bora kwa Kila Mhitaji; Chukua hatua, panua wigo.”
Picha na Reuben mauya

Wednesday 10 June 2020

VETA YAPEWA MAAGIZO MAZITO

Waziristan wa Elimu,Sayansi na Tekinolojia prof Joyce Ndalichako amewataka viongozi na wajumbe wapya wa chip cha Veta kuweza kusimamia kiasi cha bilioni 40 kwaajili ya ujenzi wa vyuo vya Veta 29 na kiasi kingine cha fedha cha bilioni 6 kwaajili ya ukarabati WA vyuo vilivyopo uku akiwataka kuongeza hudaili Kwa watoto wa kike,watu wenye ulemavu,ujenzi wa madarasa na mabweni katika Kila Halmashauri nchini ametoa Rai Kwa vyuo vya Veta vyote nchini kutoa elimu na mafunzo ambayo yatasaidia kupata Wataalam katika Viwanda vyetu na katika kuunga juhudi za Rais Magufuli kwenye kuelekea Uchumi wakati na viwanda


Habari picha na Ally Thabit

MENEJA MASOKO WA UHUSINO NA MAWASILIANO WA HOTEL YA KILIMANJARO AWATOA OFU WATEJA WAO

Liliani Kisasa Meneja Masoko Mausino na Mawasiliano wa Kilimanjaro Hotel tarehe 10 Mwezi 6mwaka 2020 wamefunguwa hotel Yao Kwa kuzingatia kanuni,Sheria na taratibu za Afya  kwaajili ya kuepusha wateja wao wasipate virusi vya ugonjwa wa CORONA Kwa kuweka barakoa,na vitakasa mikono  ivyo amewataka watu wote kwenda kupata huduma kwenye hotel Yao Nae mkuu wa Mkoa DSM ameupongeza uongozi wa hotel ya Kilimanjaro Kwa kufungua hotel Yao leo na kuchukua hatua na jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa CORONA huku akiwataka Watanzania na wasio watanzania kujitokeza kupata huduma mbalimbali


Habari picha na Ally Thabit

CHAMA CHA MAARBINO CHATOA YA MOYONI

Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Uarbino Musa Kabimba ameitaka serikali kuweza kutoa huduma ya Kansa ya Ngozi kwenye ospitali za rufaazote hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na Kansa Kwa watu wenye Uarbino kwasasa huduma hii inatolewa kwenye Mikoa ya Singida ,Tanga,Iringa,Mara Dsm,Morogoro na Lindi pamoja na ospitali ya Unguja mnazimmoja katika kuelekea siku ya watu wenye Uarbino tarehe 13 Mwezi wa sita wamefanikiwa kuamasisha uandikishaji wa watoto wenye Uarbino kujikinga na shule ya msingi ,kushirikiana kwenye shughuri mbalimbali za kiuchumi kupitia tasafu na kupata asilimia 2 kutoka kwenye Halmashauri kuweza kupatikana muongozo wa mpango mkakati kuusu watu wenye Uarbino ambako Lauri mbiu ya mwaka huu inasema haki Sawa Kwa wote boresha afya,elimu na Ajira Kwa watu wenye Uarbino


Habari picha na Ally Thabit

DIWANI WA KATA YA MCHAFU KOGE AFANYA MAZITO

Konslata Kristofa Diwani wa kata ya Mchafu koge kupitia chama cha Chadema ameweza kutekeleza Irani ya Chadema Kwa asilimia kubwa    ameweza kujenga soko la kisutu Kwa shilingi bilioni 13.5 ,Ofisi ya mchafu koge Kwa shilingi milioni40. Ujenzi wa vyoo vya shule ya sekondari ya Jamuhuri na kuboresha majengo ya shule hii pia diwani Konsolata ameviwezesha vikundi vipatavyo 5 vya mama wajane,vijana,watoto na wazee kupata pesa kwaajili ya kuishughurisha na ujasiliamali uku akiwezesha kukarabatiwa barabara za mitaa kwenye kata ya mchafu koge ametoa wito Kwa wakazi wa kata ya mchafu koge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka2020 wamchague Kwa maraingine tena ili aendeleze kufanya mambo makubwa na mazuri kwenye kata ya mchafu koge

Habari picha na Ally Thabit