Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimepokea wanachama wapya 80 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Kibamba jijini Dar es salaam kwa lengo la kuungana na chama hicho ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika Hafla ya kuwapokea wanachama hao wapya iliyofanyika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa TLP Augustine Lyatonga Mrema amesema wanachama hao wameamua kujiunga na chama hicho baada yaTLP kutangaza nia ya kumuunga mkono Rais Magufuli kama mgombea wa Urais ktk uchaguzi mkuu ujao baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake.
Nao kwa upande wao, wanachama hao wapya wamezungumzia lengo la kuhamia TLP ambapo wamesema sababu kubwa ni Mbunge wa Chadema katika Jimbo la Kibamba kushindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati akiomba kura katika uchaguzi uliopita ikiwemo kero ya maji pamoja na mikopo kwa Vijana
No comments:
Post a Comment