Saturday 29 June 2019

MWENYEKITI WA CUF AINYOSHEA KIDOLE SERIKALI


Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba ameitaka serikali ya Tanzania kuongeza pesa Bank kuu ya Tanzania lengo mzunguko wa pesa uwe mkubwa kwa wananchi pia ameitaka serikali kuviacha vyama vya siasa vitoe elimu kwa wananchi umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftali la wapiga kura pia amelitaka Jeshi la Polisi kutoingilia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili watu washiriki bila ofu.
amesema haya makao makuu ya CUF Buguruni wakati akiwasilisha tamko la baraza kuu la chamacha CUF.

Habari Picha na

Ally Thabiti

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI AWAPIGA MKWALA WARIRI WA VYOMBO VYA HABARI


Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi wa Taifa Jaji Kaijage amewataka wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa Habari watumie taaramu yao na karamu zao katika kuwandika na kuwabalisha umma katika kujiandikisha katika daftali la kudumu la wapiga kula pia amewataka watoe elimu ya kujiandikisha kwa udilifu na uweredi zaidi lengo wajitokeze katika kupata vitambulisho vya kupigia kura kwa wingi zaidi.
Amesema haya jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere wakati mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Kaijage akiwapa mafunzo wariri na waandishi wa Habari.

Habari Picha na
Ally Thabiti.

MKURUGENZI WA MTENDAJI WA TOL GASES LIMITED AHANIKA MIKAKATI MIZITO


Mkurugeinzi mtendaji wa Tol Gases Limited amesema katika kumuunga mkono Raisi Magufuli katika kuelekea Tanzania ya Viwanda kampuni yao inampango wa kununua mitambo miwili ya Gas ya Nitrogen na Oxgen lengo kumuunga mkono Raisi Magufuli kuelekea Tanzania ya Viwanda kwani gas yao inatumika kwa kiasi kikubwa kwenye viwanda na pia amewapongeza wana hisa na wafanya kazi,
Pia amesema  kuwa watatanua huduma ya Gas kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati na wataongeza magari mengi zaidi kwa ajili ya kusambaza gas, anawapongeza Azam, Muhimbili, Mruganzila, Agakani na Mgodi wa Buyamkuru kwa kutumia Gas yao hawa wato pia amewapongeza nchi ya Congo, Malawi, Zambia na Burundi pamoja na Tanzania kwakuwa wateja wa Gas yao amesema haya wakati wa kutoa gawio kwa wanahisa jijini Dar es Salaam Mkumbi wa Mwalimu Nyerere Posta.

Habari Picha na
Ally Thabiti

MABOSI WA TOL GASES LIMITED WATETA NA WANAHISA


Viongozi wa Tol Gases Limited wamewataka wana hisa kuwaamini katika kupewa gawio hii inazihirisha baada ya miaka ishirini iliyopita kampuni ya Tol Gases Limited akutowa gawio na sasa hivi wameamuwa kutoa gawio kwa wanahisa wake wote, Ambako kila mmoja atapata 17.37 la gawio lake.
Mwenyekiti wa bodi amesema jumla ya kiasi cha fedha bilioni moja zinatolewa hamesema haya kwenye mkutano wa wanahisa ulifanyika jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere. Kwa upande wa wanahisa wameupongeza uwongozi wa kampuni ya Tol Gases Limited  kwa uwaminifu na uwadilifu baada ya kukonga nyoyo zako kwa muda mrefu sana.

Habari Picha na
Ally Thabiti

MWENYEKITI WA BASATA ANENA MAZITO


Abi Gunze mwenyekiti wa bodi ya basata amewataka wasanii waendeleze umoja na mshikamano walio nayo kwani wakiendelea kufanya hivi sanaa itakuwa na kutambulika duniani kote na pia amesema kuwa tarehe 25/06/2020 Baraza la sanaa nchini Tanzania litaitisha kongamano lingine la wasanii lengo kupata mrejesho wa changamoto zilizohibua kwenye kongamano lililofanyika tarehe 28/06/2019 huku akiwataka maraisi wa mashirikisho ya sanaa na pamoja na maafisa utamaduni kufanya kazi pamoja na kuwa na ushirikiano amesema haya kwenye viwanja vya Basata jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la wasanii.

Habari Picha na
ALLY THABITI

MJUMBE WA BODI YA BASATA AWATOA OFU WASANII


Singo Mohamed Mtambalike amesema kuwa changamoto zinazowakabili wasanii basata itazifanyia kazi lengo kukuza sanaa zao amesema haya kwenye viwanja vya Basata vilivyopo jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano.

Habari picha na
Ally Thabiti

Wednesday 26 June 2019

THRC









TLHRDC YA WAONGEZEA CHACHU MAWAKILI

TLHRDC imekutana na baadhi ya mawakili ili kuwapa semina mawakili hao juu ya kuzijua  sheria za uchaguzi na wakatikati hapo pichani ni Augustino Ramadhani ni jaji mkuu wa Tanzania mstaafu ambaye alikuwa mgeni na amewataka mawakili kusoma zaidi masuala ya sheria na kuto kata tamaa kwenye masomo ya yao na kwa shirika hilo kuwapa mafunzo.

naye mwanamama wa juu amewapongeza kwa kutoa mafunzo hayo kwa mawakili na yeye ni wakili pia na huyo kana wa mwisho ametoa elimu na ataenda kutoa elimu kwa ufasaha juu ya masuaka ya uchaguzi.


Habari picha na ALLY THABITI


DAR RUNNING MARATHON

DAR RUNNING MARATHON wapewa TANO


Mshiriki wa Dar running Marathon amewapongeza waandaaji wa mashindano hayo kwani wamewakutanisha na watu mbalimbali pia wameweza kujifunza na kupata uelewa juu ya umuhimu wa kushiriki mashindano ya riadha na pia amewataka waweze kutanua wigo mkubwa zaidi wa mashindano hayo hayo yamesema jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya coco beach kwenye bwalo la maafisa wa jeshi la polisi na mmojab wa washiriki hao.

Habari Picha na ALLY THABIT

DAR RUNNING MARATHON

Mshindi wa Dar Running Marathon atoa neno
Manywele ni mshindi wa mbio za kilometa 21 ambaye ameshinda nafasi ya kumi amewataka watanzania kushiriki kwenye mbio za Dar RUNNING MARATHON kwakuwa ni moja ya sehemu tya mazoezi na kuimarisha afya pia amewapongeza waandaji wa mashindano hayo kwani yeye ameweza kuonyesha kipaji chake na uwezo wake na anaamini kupitia mashindano hayo ataweza kushiriki mashindano ya kit6aifa na kimataifa.

Mashindano hayo yalikuwa na washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka afrika mashariki kwa kilomita 21 nafasi ya kwanza hadi ya tatu ilishika na watanzania.

Habari picha na ALLY THABITI


Friday 21 June 2019

KUELEKEA AFCON 2019: CAF YAZITAHADHARISHA TIMU KUJIANDAA KUCHEZA KWENYE JOTO KALI

Ikiwa leo michuano ya Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2019 ndio inaanza kutimua vumbi nchini Misri, mataifa 24 yatakayoshiriki mtanange huo yameonywa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kwamba yajiandae kwa mashindano yatakayochezewa kwenye joto kali.

Taarifa kutoka nchini Misri ambako mashindano haya yatafanyika kuanzia leo Juni 21 hadi Julai 19 zinasema kwamba Kamati ya mashindano inayojihusisha na masuala ya afya kwenye CAF imeitisha mapumziko ya lazima ya dakika tatu baada ya dakika 30 za kwanza na pia itakapogonga dakika ya 75, mbali na yale ya kawaida ya dakika 15 kipindi cha kwanza kinapomalizika.

Mashindano haya makubwa barani Afrika yalihamishwa kutoka tarehe zake za kawaida za Januari na Februari hadi Juni na Julai kwa mara ya kwanza kutokana na mivutano kati ya klabu na nchi. Hali ya joto nchini Misri wakati huu inatarajiwa kufikia kati ya nyuzi joto 35 na 38.

SERIKALI YA TANZANIA YAJIPANGA KUTEKA SOKO LA WATALII CHINA

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii,  suala la  kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo  ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo  waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu  wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS.

Amesema  lengo mkutano huo ni  kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.

Mkutano huo  umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao.

Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora  kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda  ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili  kujengeana uwezo  baina ya Serikali ya  Tanzania na China.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 21, 2019.














Wednesday 19 June 2019

MOI WAJITOLEA KUWAFANYIA UPASUAJI WATOTO 15

 Madaktari bingwa wa MOI wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye kichwa kikubwa katika kambi maalum iliyofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akikagua jalada na kuzungumza na mgonjwa anayesubiri kufanyiwa upasuaji katika chumba cha upasuaji MOI.
 Kaimu mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MOI Elizabet Mbaga akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Uhusiano na elimu kwa Umma mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Bi. Laura Kunenge
   Watumishi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya MOI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari katika vyumba vya upasuaji MOI katika kambi maalum ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongowazi ambayo imefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma na kuanzishwa kwa taasisi ya MOI miaka 23 iliyopita.
Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt Hamis Shabani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vyanzo na matibabu ya kichwa kikubwa na mgongo wazi katika vyumba vya upasuaji MOI.

NA KHAMISI MUSSA
Watumishi wa Taasisi ya tiba ya Mifupa ya MOI leo wamejitolea kuendesha kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma pamoja na  miaka 23 toka Taasisi ya MOI kanzishwa.

Shuguli nyingine zimehusisha uchangiaji wa damu kwa hiari, usafi wa mazingira katika maeneo ya hospitali pamoja na kutoa zawadi na misaada ya kijamii kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa wodini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface aliwaongoza watumishi katika shughuli zote za usafi, kuchangia damu pamoja na kambi ya upasuaji.

“Leo tunafanya kazi kwa kujitolea ikiwa ni sehemu ya wiki ya utumishi wa Umma na pia ni wiki ya maadhimisho ya miaka 23 ya kuanzishwa kwa Taasisi yetu ya MOI mwaka 1996, hivyo nimeshiriki kikamilifu na watumishi wenzangu ili kuonyesha mfano kama kiongozi” Alisema Dkt Boniface
Aidha, watumishi wa MOI wamepata fursa ya kupata mafunzo maalum kutoka kwa wataalamu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kufanya kazi katika mazingira salama.

Pia, watumishi kutoka mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) wameshiriki katika kufanya usafi katika mazingira ya Taasisi ya MOI pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.