Monday, 10 June 2019

WAZIRI UMMY AZINDU KAMBI YA MIGUU BANDIA MOI

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akimkabidhi Pascal Patrick mguu bandia unaotolewa kwa ushirikiano kati ya MOI na Taasisi ya BMVSS y India. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)





NA KHAMISI MUSSA
Dar es Salaam ,10/06/19. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) leo amefungua kambi maalum ya kupima na kutengeneza miguu bandia zaidi ya 600 kwa watu wenye uhitaji ambao walijiandikisha.

Waziri Ummy amesema Kambi hiyo ya utoaji miguu bandia bure inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya BMVSS ya Nchini India na itaendeshwa kwa siku 40.

 “Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mh. Dkt John Pombe Magufuli imefanya mageuzi makubwa hapa MOI, maboresho makubwa yamefanyika na kama Waziri mwenye dhamana nawapongeza madaktari, wauguzi na watumishi wote wa MOI naridhishwa na utendaji wenu”Alisema  Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema baada ya kufanya uchambuzi wa watu waliojiandikisha kupata miguu bandia , takwimu zinaonyesha kwamba chanzo kikubwa cha watu kupoteza viungo vyao ni ajali na Kisukari.

“Vyanzo vikuu vya ulemavu ni ajali za barabarani  na ugonjwa wa Kisukari hivyo nitumie wasaa huu kuwakumbusha watanzania wenzangu kufuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali na pia kuepuka mitindo ya maisha ambayo inaweza kupelekea kupata magonjwa yasioambukiza kama kisukari na pia tujenge utamaduni wa kufanya mazoezi” alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Balozi wa India hapa Nchini, Mh. Balozi Sandeep Arya amesema kambi hii ni sehemu ya kumbukumbu ya muasisi wa Taifa hilo Mahatma Gandhi ambaye aliamini katika upendo, ubinadamu ambapo mwaka huu zoezi la utoaji miguu bandia litafanyika katika mataifa mbalimbali na Tanzania ikiwemo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Prof. Charles Mkonyi  ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya MRI, CT-SCAN, Digital X-ray ambavyo kwa kiasi kikubwa vimeasiadia kupunguza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment