Wednesday, 19 June 2019

MOI WAJITOLEA KUWAFANYIA UPASUAJI WATOTO 15

 Madaktari bingwa wa MOI wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye kichwa kikubwa katika kambi maalum iliyofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akikagua jalada na kuzungumza na mgonjwa anayesubiri kufanyiwa upasuaji katika chumba cha upasuaji MOI.
 Kaimu mkurugenzi wa huduma za Uuguzi MOI Elizabet Mbaga akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Uhusiano na elimu kwa Umma mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Bi. Laura Kunenge
   Watumishi wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya MOI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari katika vyumba vya upasuaji MOI katika kambi maalum ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongowazi ambayo imefanyika kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma na kuanzishwa kwa taasisi ya MOI miaka 23 iliyopita.
Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt Hamis Shabani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vyanzo na matibabu ya kichwa kikubwa na mgongo wazi katika vyumba vya upasuaji MOI.

NA KHAMISI MUSSA
Watumishi wa Taasisi ya tiba ya Mifupa ya MOI leo wamejitolea kuendesha kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma pamoja na  miaka 23 toka Taasisi ya MOI kanzishwa.

Shuguli nyingine zimehusisha uchangiaji wa damu kwa hiari, usafi wa mazingira katika maeneo ya hospitali pamoja na kutoa zawadi na misaada ya kijamii kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa wodini.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface aliwaongoza watumishi katika shughuli zote za usafi, kuchangia damu pamoja na kambi ya upasuaji.

“Leo tunafanya kazi kwa kujitolea ikiwa ni sehemu ya wiki ya utumishi wa Umma na pia ni wiki ya maadhimisho ya miaka 23 ya kuanzishwa kwa Taasisi yetu ya MOI mwaka 1996, hivyo nimeshiriki kikamilifu na watumishi wenzangu ili kuonyesha mfano kama kiongozi” Alisema Dkt Boniface
Aidha, watumishi wa MOI wamepata fursa ya kupata mafunzo maalum kutoka kwa wataalamu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kufanya kazi katika mazingira salama.

Pia, watumishi kutoka mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) wameshiriki katika kufanya usafi katika mazingira ya Taasisi ya MOI pamoja na kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment