Saturday 30 November 2019




TUME YA USHINDANI YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURUSA

PROF Humphrey P .B Mosh amesema katika kuelekea maazimisho ya ushindani wa kibiashara ambako yatakuwa tarehe 3 mpaka5 mwezi wa 12 viwanja vya mnazi mmoja wajitokeze kwa wingi kuonyesha biashara zao TASAC itakuweepo,TRRC ,TTCR,na TCAA  tume ya ushindani  inaendana na kauli mbiu ya Magufuli kueleekea Tanzania ya viwanda ivyo amewataka watanzania kuwa wabunifu tarehe 4 mwezi12 kutakuwa na kongamano la kujadili maswala ya biashara za mitandaoni na ushindani wa biashara

habari picha na Victoria Stanslaus

TUME YA USHINDANI YAWATAADHARISHA WATANZANIA BIASHARA ZA MTANDAONI

Mkurugenzi wa tume ya ushindani ya biashara amewataka watanzania kutoamini biashara za mitandaoni ivyo amesema  makampuni ya Ally Baba na mengineyo ivyo waache kuttumia makampuni mengineyo watatapeliwa  amesema haya wakati akitambulisha kuwa kutakuwa na maonyesho ya ushindani wa kibiashara tarehe 3 mpaka 5 mwezi wa12 viwanja vya mnazi mmoja

habari  picha na Victoria Stanslaus

KAMISHINA WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWARA BORA ATEMA CHECHE

Kamishina wa haki za binadamu na utawala bora Nyanda Shuri amezitaaka asasi za kiraia kuwafikia watu wa pembe zoni kwa kuwapa elimu  ya maswala ya jinsia na haki

habari picha na Victoria Stanslaus

RUSHWA YA NGONO NITATIZO

Mkurugenzi wa TGNP mtandao Riliani Riundi amesema swala la rushwa yya ngono ni tatizo kwa wanawake hapa nchini maofisini,viwandani pamoja na vyuoni ivyo amewataka wanawake na wanaume kupaza sauti

habari picha na Victoria Stanslaus

WIZARA YA AFYA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA NHIF

Mkurugenzi wa wizara ya afya  Gresi Magembe amesema wizara ya afya inawaunga mkono NHIF walivyo amua kuja na vifurushi vya watu wa hali ya chini ivyo amewataka watanzania kuchangamkia furusa zilizo tolewa na NHIF kwaajili ya kunusuru afya zao ivyo amesema serikali itazidi kuboresha huduma za afya na kutoa dawa zakutosha na vifaa tiba

habari picha na Victoria Stanslaus

MKURUGENZI WA HUDUMA NA UFUNDI WA NHIF WANAKUJA NA MIKAKATI MIZITO

Mkurugenzi wa huduma na ufundi wa NHIF amesema vifurushi walivyozindua  vipya vya huduma ya afya watatoa elimu kwa kila mtu pili kila mtu ajiunge na bima ya afya ili wanusuru maisha ya watanzania amesema haya viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam

habari picha na  Victoria Stanslaus

MKURUGENZII WA NHIF AWATTOA OFU WATANZANIA

Mkurugenzi wa NHIF Bernald Kongwa ameesema kuwa vifurushi vya bima walivyozindua  kila mtanzania anavimudu kwani ni vya bei nafuu
habari picha na  Ally Thabiti

MKURUGENZI WA NHIF AWATOA OFU WAATTANZANIA

NHIF KUNUSURU VIFO VYA WATANZANIA

Mwenyekiti wa bodi ya bima ya afya Taifa  ANA MAKINDA amezindua vifurushi vya bima ya afya ambavyo vitawafikia hadi watu wenye vipato vidogo kwa bei nafuu zaidi lengo kumuunga mkono rais Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda

habari picha  na Victoria Stanslaus

Tuesday 26 November 2019

MBUNGE CHADEMA AJITOSA KUWANIA NAFASI YA UENYEKITI TAIFA

Mbunge wa Ndanda ndugu Cecil David Mwambe hii leo amezungumza na waandishi wa Habari kuhusu mipango mikakati yake ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, akibainisha kuwa akipata nafsi hiyo atahakikisha kunakuwa na Ugatauzi wa madaraka ambapo itatoa nafasi ya kimaamuzi kuanzia ngazi ya kata hadi taifa ndani ya chama hicho jambo ambalo kwa hivi sasa hakipo.
Aidha Mwambe amebainisha kuwa atakuwa muwazi na muwajibikiaji katika suala zima la mapato na matumizi ya chama hicho kikubwa cha upinzani nchini Tanzania.
pia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 amesema atahakikisha anaunganisha vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha wanaleta ushindani ikibidi kuchukua dola katika uchaguzi huo.
Akiwagusia wanachama ambao wametoka Chadema kwenda CCM amesema kuwa sio wasaliti bali ni matishio ya kisiasa na kutotekelezwa kwa hoja zao za msingi ndani ya chama.
akiongelea suala la mwenyekiti wa chama hicho freeman Mbowe mbunge huyo wa ndanda amesema hatishiki na wananchi kumchukulia fomu mbunge huyo. HABARI PICHA NA ALLY THABITI

AGA KHAN YAELEZA SABABU ZA WATOTO KUZALIWA KABLA YA MUDA WAO

pichani ni miongoni mwana mama ambaye amezaa mtoto ambaye hajatimia miezi Bi. Saraha John. ambaye ampongeza hospitali ya aga ghana kwa kudhibiti tatizo hilo na kufanikisha kunusuru tatizo la mwanae, pia ameitaka serikali pamoja na taasisi binafsi za afya kupunguza gharama za kuwahudumia watoto wasio timiza miezi.

kwa upanmde wake Kiongozi wa Hopsitali ya aga khan (Hayupo pichani )amesema matumizi ya sigara, pombe ni chanzo cha wanawake wengi kujifungua kabla ya wakati hivyo kupata watoto ambao hawajatimiza miezi tisa, Pia ugonjwa wa jkisukari pamoja na presha huchangia kwa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake. HABARI PICHA NA ALLY THABITI

Friday 8 November 2019

SIDO YAFUNGUA MILANGO KWA WABUNIFU


MACDONAD MAGANGA meneja mkowa wa Dar es salaam amewataka Watanzania ususani ni wabunifu kujitokeza kwa wingi kupeleka maandiko yao yanayohusiana na maswala ya ubunifu kwenye uoande wa Teknolojia na kuongeza samani ya mazao kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ambako washirki kuanzia 25 mpaka 30 ndiyo wanatakiwa kushiriki ambako leo tarehe 8 mpaka tarehe 21 mwezi huu 11 ndiyo mwisho wa kupeleka maombi yao ambako wanatakiwa kupeleka maombi yao SIDO kwa mkono au kwa S.L.P 22151, Dar es salaam au kupitia kwenye barua pepe daressalaam@sido.go.tz au kupitia tovuti hii http://www.ubunifu.or.tz na waombaji wote wanatakiwa kulipa kiasi cha pesa kisicholejesheka cha shilingi 50,000/= kupitia namba 0767 270 111 huku akisisitizi kuwa malipo haya yafanyike kupitia Control No. ambayo muombaji utapewa 

Amesema haya jiji Dar es Salaam kwenye ofisi  za Sido


Naye Gosbart Baitwa Mkurugenzi wa kampuni ya KRBF food Supplies ambako ofisi zake zipo geti rumo ameipongeza sido kwa kuanzisha ushindani kwa wabunifu kwani hii itasaidia kuchochea kwa ukuwaji wa viwanda kwa kasi na huku ndiyo kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuelekea uchumi wa kati na ukuwaji wa viwanda.

Gosbert Baitwa anawapongeza SIDO kwakutoa mafunzo mbalimbali ya kuongeza samani ya mazao hii inawasaidia wajasilia mali kutengeneza bidhaa zenye ubora amesema haya kwenye mafunzo yaliondaliwa na SIDO ya siku tano yenye jumla washirki arobaini makao makuu ya SIDO. 


  Nae Jonathan Afisa Biashara wa SIDO amesema kuwa wanakabiliwa na uwaba wa maeneo kwani ni machache ndiyo maana wameamua kuchukua wabunifu 20 mpaka 30 hivyo changamoto hii ingetatuliwa wangechukua wabunifu zaidi ya miamoja hilindiyo lengo lao.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus

TAASISI YA UTAFITI YA AFYA YA IFAKALA YAJA NA MIKAKATI MIZITO YA KUTEKETEZA MALERIA


Mkurugenzi wa Taasisi ya afya ya Ifakala inayoshughulika na maswala ya utafiti wa Afya Tanzania Onorati Masanja wameamua kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano ili kupunguza vifo juu ya Maleria juu ya watoto hao pia wanatoa vyandalua kwa wamama wajawazito  bure ili kutokomeza vifo vya maleria kwa mama wajawazito na sasa wanafanya tafiti ya matumizi ya ndala pamoja na langi mbalimbali ambako itasaidia kuondoa maleria nchini.

Taasisi ya Utafiti ya Afya Ifakala inatawi Dar es salaam, Ifakala Mkoani Morogoro na Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Mkurugenzi amesisitiza kuwatafiti zao juu ya Maleria zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa ugonjwa wa Maleria nchini na kuokoa maisha ya watu wengi.

Amesema haya Mjini Bagamoyo kwenye semina ya wanahabari.  


Nae mwnahabari wa gazeti la mwananchi Lilian Timbuka kwa niaba ya wanahabari wote ameshukuru taasisi ya Utafiti ya Afya ya Ifakala kwa kuwapa mafunzo yanayousiana na maswala ya utafiti upande wa afya na namna ya kuandika habari za utafiti wa afya.

Lilian Timbuka ameitaka Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala tafiti zao kuandika kwa lugha ya Kiswahili pia na amewahasa wanahabri mafunzo waliyoyapata wayatumie vizuri hii itawasaidia kuandika habari za afya kwa uweledi zaidi, ametoa wito kwa watafiti hapa nchini kutoa ushirikiano kwa wanahabari katika kutolea ufafanuzi maswala ya Afya.


Nae Dr. Shubis Kafuruki ambaye Principal Research kutoka taasisi ya utafiti wa afya ya Ifakala amewatoa ofu wanahabari kuwawakiitaji taarifa zozote kutoka taasisi ya afya ya Ifakala milango ipo wazi na wanakaribishwa amesema taasisi yao aifanyi tafiti kwa ugonjwa wa Maleria tu inafanya utafiti na ugonjwa wa HIV na magonjwa mengineyo ikiwemo TB.

Dr. Shibis Kafuruki amesema katika malengo yao matano kwenye utafiti maswala la kufanya semina na mafunzo kwa wanahabari ni moja ya malengo yao ivyo wameahidi kudumisha umoja, Ushirkiano na kuweka nguvu kwa pamoja katika maswala ya afya na wanahabari.

Amesema haya wakati akifunga semina kwa wanahabari mjini Bagamoyo kwenye mkoa wa Pwani kwenye Taasisi ya Afya ya Ifakala.


Pichani wanahabari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Taasisi ya utafiti ya afya ya Ifakala mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus 

Wednesday 6 November 2019

MWANACHAMA WA CUF ATOA SHUTUMA MZITO KWA CCM


Rahma Ally Mkasi ni mwanachama wa CUF kutokea manzese ameraani vikali kitendo cha CCM kuvuruga uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani na yeye jina lake limehenguliwa katika kugombea nafasi ya ujumbe kwa upande wa wanawake hivyo ameitaka CCM kuacha kuingilia uchaguzi kwani watasababisha machafuko makubwa nchini amesema haya Makao Makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.

Habari Picha na
Ally Thabiti

TUNU YA AMANI NA USALAMA KUTOWEKA KWA SABABU YA UCHAGUZI


Mwenyekiti wa chama cha CUF Professorial Ibrahim Aruna Lipumba amemtaka Rais Magufuli kuingilia kati uchaguzi wa serikali za mitaa kwani watendaji wanavuruga utaratibu wa uchaguzi pamoja na kanuni zinazowekwa kwa kuwaengua wagombea wa vyama vingine na kuwabambikia kasi ambako katika mkoa wa Lindi, Bagamoyo, Kinondoni, Kigamboni, Tabora wagombea wa chama cha CUF, CHADEMA na vyama vyengine wameondolewa kuwania nafasi za wenyekiti wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji. 

Hivyo wamevunja kanuni ya kumi na tano B Lipumba amewataka marais wastaafu akiwemo kikwete, Mkapa na Mwinyi kuingilia kati swala hili ili kunusulu amani na usalama visitoweke, Pia ametaka urejeshwaji wa fomu uwongezwe waliokatwa walejeshwe CUF inaraani vikali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuwepo kwa ufisadi na rushwa kwa watendaji wa kata. 


Naye aliyetoka CCM kuingia chama cha CUF Mwalami Gundumu amewataka watendaji kuacha kufanya ubazilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ameingia chama cha CUF kwa ajili ya kufwata haki na amehipata kwani ndani ya CCM kata ya kijichi vimejaa vitendo vya Rushwa ufisadi pamoja na ubadhilifu anakishukuru chama cha CUF kwa kumpokea kwa mikono na moyo mmoja.


Naye Mzee Uredi amesema ametoka chama cha CCM kata ya Kijichi ameingia chama cha CUF kwani viongozi wa CCM amejaa Ukilitimba ikiwemo kukatwa kwa viongozi wizi wa kura ndani ya CCM.


Naye Mzee wa CUF kutoka Mlali Mkoa wa Morogoro Mzee Abdallah amemlani vikali mtendaji msaidizi wa kata ya Mlali kwa kuwafanyia ubadhilifu ambako wamekata majina ya wana CUF hivyo wamemtaka Rais Magufuli kutofumbia macho vitendo hivi kwani vitaleta machafuko makubwa nchini ikiwemo kumwagika kwa Damu za Watanzania amesema haya kwenye makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus 

Saturday 2 November 2019

TBS YATANGAZA VITA KARI KWA WAINGIZAJI NA WASAMBAZAJI WA VIPODOZI FEKI


Shirika la viwango Tanzania TBS limepiga marufuku vipodozi vyovyote kutoka nje kuingizwa nchini bila kufanyiwa maombi kupitia njia ya mtandao ya tovuti ya anuani ya  shirika hilo

Hatua hiyo  ni  mkakati wa TBS  kutaka kuviifanyia uhakiki vipodozi vyote vinavyoingizwa  nchini Kama ambavyo vimeruhusiwa kwa   matumizi  ya Tanzania ama  la

Marufuku hiyo imetolewa na  mkaguzi mwandamizi wa viwango TBS Donald Manyama wakati wa  zoezi la ukamataji wa vipodozi vyenye viambata sumu linaloendelea kwenye maduka ya jumla na rejareja jijini Dar es Salaam.

Amesema  kumekuwa na  wimbi la uingizwaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku ambapo wafanyabiashara wengi wanadai wanapoagiza hawajui vimeruhusiwa ama lah hivyo uhakiki  utasaidia kutoa  taarifa ni vipodozi vipi vinarusiwa vipi haviruhusiwa.

Pia Donald Manyama Mkaguzi Mwandamizi TBS akaelezea walivyojipanga kukabiliana na wale wote wasio waaminifu watakapenyeza vipodozi hivyo kwa njia ya panya.

Yamesema haya na  Donald manyama mkaguzj mwandamizi TBS.


Pichani maafisa wa TBS wakikagua vipodozi vyenye viambata vya sumu.

Habari Picha na 
Ally Thabiti

WANA GDSS WARAANI VIKALI MIFUMO DUME


Janeth John Mwanaharakati wa TGNP Mtandao ambaye anahuzulia semina za GDSS amewataka Watanzania kuachana na mifumo dume kwani mifumo hii imekuwa kandamizi kwa wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na katika kujikwamua kiuchumi amepongeza semina za GDSS kwani zimemjengea uwezo mkubwa katika maswala ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.



Naye mshirki wa semina za GDSS Nepo Musenti amesema semina za GDSS yeye ameweza kuelimisha jamii anapoishi kuachana na maswala ya ukatili wa kijinsia hivyo ameiyomba TGNP Mtandao waendeleza kuzitoa semina hizi za GDSS kwa kasi kubwa kwani zimeweza kuleta mafanikio makubwa kwa jamii ambako kumepelekea kupungua kwa maswala ya ukatili wa kijinsia nchini ambako kila jumatano kuanzia saa 9 mpaka saa 11 semina hizi za GDSS zinatolewa Mabibo kwenye ofisi za TGNP Mtandao.


Pichani ni washiriki wa semina za maswala ya jinsia na jinsi za GDSS kutoka Temeke, Makumbusho, Mabibo, Chanika na maeneo mengineyo ya Dar es Salaam.

Habari picha na 
ALLY THABITI