Friday, 8 November 2019

SIDO YAFUNGUA MILANGO KWA WABUNIFU


MACDONAD MAGANGA meneja mkowa wa Dar es salaam amewataka Watanzania ususani ni wabunifu kujitokeza kwa wingi kupeleka maandiko yao yanayohusiana na maswala ya ubunifu kwenye uoande wa Teknolojia na kuongeza samani ya mazao kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ambako washirki kuanzia 25 mpaka 30 ndiyo wanatakiwa kushiriki ambako leo tarehe 8 mpaka tarehe 21 mwezi huu 11 ndiyo mwisho wa kupeleka maombi yao ambako wanatakiwa kupeleka maombi yao SIDO kwa mkono au kwa S.L.P 22151, Dar es salaam au kupitia kwenye barua pepe daressalaam@sido.go.tz au kupitia tovuti hii http://www.ubunifu.or.tz na waombaji wote wanatakiwa kulipa kiasi cha pesa kisicholejesheka cha shilingi 50,000/= kupitia namba 0767 270 111 huku akisisitizi kuwa malipo haya yafanyike kupitia Control No. ambayo muombaji utapewa 

Amesema haya jiji Dar es Salaam kwenye ofisi  za Sido


Naye Gosbart Baitwa Mkurugenzi wa kampuni ya KRBF food Supplies ambako ofisi zake zipo geti rumo ameipongeza sido kwa kuanzisha ushindani kwa wabunifu kwani hii itasaidia kuchochea kwa ukuwaji wa viwanda kwa kasi na huku ndiyo kumuunga mkono Rais Magufuli katika kuelekea uchumi wa kati na ukuwaji wa viwanda.

Gosbert Baitwa anawapongeza SIDO kwakutoa mafunzo mbalimbali ya kuongeza samani ya mazao hii inawasaidia wajasilia mali kutengeneza bidhaa zenye ubora amesema haya kwenye mafunzo yaliondaliwa na SIDO ya siku tano yenye jumla washirki arobaini makao makuu ya SIDO. 


  Nae Jonathan Afisa Biashara wa SIDO amesema kuwa wanakabiliwa na uwaba wa maeneo kwani ni machache ndiyo maana wameamua kuchukua wabunifu 20 mpaka 30 hivyo changamoto hii ingetatuliwa wangechukua wabunifu zaidi ya miamoja hilindiyo lengo lao.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment