Tuesday, 26 November 2019

MBUNGE CHADEMA AJITOSA KUWANIA NAFASI YA UENYEKITI TAIFA

Mbunge wa Ndanda ndugu Cecil David Mwambe hii leo amezungumza na waandishi wa Habari kuhusu mipango mikakati yake ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, akibainisha kuwa akipata nafsi hiyo atahakikisha kunakuwa na Ugatauzi wa madaraka ambapo itatoa nafasi ya kimaamuzi kuanzia ngazi ya kata hadi taifa ndani ya chama hicho jambo ambalo kwa hivi sasa hakipo.
Aidha Mwambe amebainisha kuwa atakuwa muwazi na muwajibikiaji katika suala zima la mapato na matumizi ya chama hicho kikubwa cha upinzani nchini Tanzania.
pia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 amesema atahakikisha anaunganisha vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha wanaleta ushindani ikibidi kuchukua dola katika uchaguzi huo.
Akiwagusia wanachama ambao wametoka Chadema kwenda CCM amesema kuwa sio wasaliti bali ni matishio ya kisiasa na kutotekelezwa kwa hoja zao za msingi ndani ya chama.
akiongelea suala la mwenyekiti wa chama hicho freeman Mbowe mbunge huyo wa ndanda amesema hatishiki na wananchi kumchukulia fomu mbunge huyo. HABARI PICHA NA ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment