Wednesday, 6 November 2019

TUNU YA AMANI NA USALAMA KUTOWEKA KWA SABABU YA UCHAGUZI


Mwenyekiti wa chama cha CUF Professorial Ibrahim Aruna Lipumba amemtaka Rais Magufuli kuingilia kati uchaguzi wa serikali za mitaa kwani watendaji wanavuruga utaratibu wa uchaguzi pamoja na kanuni zinazowekwa kwa kuwaengua wagombea wa vyama vingine na kuwabambikia kasi ambako katika mkoa wa Lindi, Bagamoyo, Kinondoni, Kigamboni, Tabora wagombea wa chama cha CUF, CHADEMA na vyama vyengine wameondolewa kuwania nafasi za wenyekiti wa serikali za mitaa vitongoji na vijiji. 

Hivyo wamevunja kanuni ya kumi na tano B Lipumba amewataka marais wastaafu akiwemo kikwete, Mkapa na Mwinyi kuingilia kati swala hili ili kunusulu amani na usalama visitoweke, Pia ametaka urejeshwaji wa fomu uwongezwe waliokatwa walejeshwe CUF inaraani vikali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kuwepo kwa ufisadi na rushwa kwa watendaji wa kata. 


Naye aliyetoka CCM kuingia chama cha CUF Mwalami Gundumu amewataka watendaji kuacha kufanya ubazilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ameingia chama cha CUF kwa ajili ya kufwata haki na amehipata kwani ndani ya CCM kata ya kijichi vimejaa vitendo vya Rushwa ufisadi pamoja na ubadhilifu anakishukuru chama cha CUF kwa kumpokea kwa mikono na moyo mmoja.


Naye Mzee Uredi amesema ametoka chama cha CCM kata ya Kijichi ameingia chama cha CUF kwani viongozi wa CCM amejaa Ukilitimba ikiwemo kukatwa kwa viongozi wizi wa kura ndani ya CCM.


Naye Mzee wa CUF kutoka Mlali Mkoa wa Morogoro Mzee Abdallah amemlani vikali mtendaji msaidizi wa kata ya Mlali kwa kuwafanyia ubadhilifu ambako wamekata majina ya wana CUF hivyo wamemtaka Rais Magufuli kutofumbia macho vitendo hivi kwani vitaleta machafuko makubwa nchini ikiwemo kumwagika kwa Damu za Watanzania amesema haya kwenye makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.

Habari picha na 
Victoria Stanslaus 

No comments:

Post a Comment