Saturday, 2 November 2019

WANA GDSS WARAANI VIKALI MIFUMO DUME


Janeth John Mwanaharakati wa TGNP Mtandao ambaye anahuzulia semina za GDSS amewataka Watanzania kuachana na mifumo dume kwani mifumo hii imekuwa kandamizi kwa wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na katika kujikwamua kiuchumi amepongeza semina za GDSS kwani zimemjengea uwezo mkubwa katika maswala ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.



Naye mshirki wa semina za GDSS Nepo Musenti amesema semina za GDSS yeye ameweza kuelimisha jamii anapoishi kuachana na maswala ya ukatili wa kijinsia hivyo ameiyomba TGNP Mtandao waendeleza kuzitoa semina hizi za GDSS kwa kasi kubwa kwani zimeweza kuleta mafanikio makubwa kwa jamii ambako kumepelekea kupungua kwa maswala ya ukatili wa kijinsia nchini ambako kila jumatano kuanzia saa 9 mpaka saa 11 semina hizi za GDSS zinatolewa Mabibo kwenye ofisi za TGNP Mtandao.


Pichani ni washiriki wa semina za maswala ya jinsia na jinsi za GDSS kutoka Temeke, Makumbusho, Mabibo, Chanika na maeneo mengineyo ya Dar es Salaam.

Habari picha na 
ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment