Tuesday, 29 October 2019

MKURUGENZI WA TIC AFICHUA SIRI NZITO


Geofrey Mwambe Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) amesema TIC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuwavutia wawekezaji na kuja kuwekeza hapa nchini ambako mpaka sasa kwanzia mwezi wa Kwanza hadi wa Tisa 2019 wamesajili makampuni 227 huku sekta ya viwanda inaongoza kwa uwekezaji ambako viwanda 128 vimesajiliwa, amesema siri kubwa ya mafanikio haya kutoa elimu ya uwekezaji, kuishauri serikali katika kuondoa vikwazo vya uwekezaji, kuondoa tozo za uwekezaji, kupatikana kwa TIN namba bure na upatikanaji wa vibali vya ujenzi kwa haraka pamoja na usajili wa makampuni kwa haraka kupitia brela hii ndio ambayo imefanya wawekezaji kuwa na imani na Raisi John Pombe Magufuli. Taasisi ya AFS group imeipongeza TIC kwa kukizi vigezo kumi na moja katika uwekezaji ambako Tanzania imeshika nafasi ya 105 mwaka huu kati ya nchi 190 ukilinganisha na mwaka jana ambako ilikua nafasi ya 131 kwa wafanyabiashara kuwa na sauti pia imeshika nafasi ya 165 mwaka huu kati ya nchi 190 ukilinganisha na mwaka jana katika kuondoa vikwazo vya kodi ambako mwaka jana imeshika nafasi ya 167 kwa upande wake EFC group imeipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya 7 kati ya nchi 20 ukilinganisha na mwaka jana ilishika nafasi ya 15 katika kuwavutia wawekezaji hapa nchini, mikoa inayoongoza katika uwekezaji hapa nchini ni Dar es Salaam na Pwani.
Geofrey Mwambe ametoa wito kwa watanzania kuwekeza hapa nchini, Makampuni 227 yaliyosajiliwa ya thamani ya dora za kimarekani Bilioni 2.0093 ambako ajira zilizo tengenezwa kwa watanzania kupitia TIC ni 38856.

Habari picha na Ally Thabith

No comments:

Post a Comment